BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, November 28, 2009

DAZ NUNDAZ KURUDI TENA KWENYE RAMANI YA BONGO FLAVA!!

Kama unalikumbuka ni kundi lililowahi kutamba sana miaka ya 90 ambalo lilikuwa likiundwa na wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wawili Ferouz na Daz Baba ambao ndio walichangia kwa kiasi kikubwa kundi hilo kujipatia umaarufu wametangaza rasmi kumaliza tofauti zao.
Wakizungumza kwa pamoja, wasanii hao walidai kuwa kwa sasa wako tayari kufanya kazi pamoja na hata kulirejesha upya kundi lao la Daznundaz.

“Unajua tofauti zetu zilikuwa ndogo tu, ingawa vyombo vya habari vilichangia sana kuzikuza,hivi sasa tuko pamoja na mimi niko tayari kufanyakazi na mshkaji Daz Baba,” alieleza Ferouz, ambaye anaonekana kufulia kinoma kimuziki na kimaisha tofauti na alipokuwa na kundi la Daz nundaz.

“Mimi na msanii mwenzangu Larumba ambaye tulikuwa pamoja tulianzisha kundi letu la Tanzaniano , lakini hili halituzuii kukaa pamoja na Ferouz na washkaji wetu wengine ili kulirejesha kundi letu la Daznundaz. Ferouz ni mtu wangu na niko tayari kufanya naye kazi,” alisema Daz Mwalimu .
Kundi la Daznundaz lilisambaratika siku chache baada ya baadhi ya wasanii wake wakiongozwa na Ferouz kumtimua kundini msanii mwenzao Dazbaba kwa madai kuwa alikuwa akitumia dawa za kulevya ‘teja.’

Kundi hilo lilipata kutamba na nyimbo zake kali kama vile; Maji ya shingo, Kamanda, Barua, Jahaz la Daz na nyingine





Friday, November 27, 2009

MAKAMUZI KWANZA, MAMBO MENGINE BAADAE- ASEMA BLUE


Baada ya kutamba na single zake za ‘Tabasamu’ na ile inayotamba
kwasasa ‘Tupo pamoja’ Dogo mwenye uwezo mkubwa wa kuishi kistaa,
Heri Samir ‘Blu’ amesema kuwa hivi sasa akizungumzia ishu ya shule
atakuwa anadanganya kwa sababu haipo kwenye programu yake.

Blu, staa wa Bongo Flava asiyefunikika, alisema kupitia kipindi
kimoja cha kinachorushwa na Radio moja Tanzania kuwa ana mambo mengi yanayomkip busy lakini ishu ya elimu haipo kwenye ratiba yake.

Dogo huyo ambaye anajulikana pia kwa jina la Kabayser, alizungumza
hivyo kama jibu la swali aliloulizwa na presenta wa kipindi hicho.

Mbali na ishu ya elimu, Blu alisema kuwa sasa hivi hayupo kwenye
mikakati ya albamu, isipokuwa atakachokuwa anakifanya ni kudondosha
singo kali kila mara ili kuwapa raha mashabiki wake.

Aidha, Blu alimpa shavu Dogo Hamidu a.k.a Nyandu Tozz kuwa ndiye
mtu aliyempeleka studio kwa mara ya kwanza, MJ Record ambapo
alifanya singo yake ya kwanza inayoitwa Kwa Mama.


ANKO MO NA VIJIMAMBO VYA TANGA INAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA EID EL HAJJI

Kupitia blog hii, Anko Mo anawatakia waislamu wote na wale wasio waislamu sikukuu njema ya Eid El Hajji na mungu awabariki sana. Libeneke linaendelea kama kawaida jamani...!!

Thursday, November 26, 2009

MIRIAM AANZA VIZURI MISS WORLD HUKO AFRIKA KUSINI


Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald ambaye yupo Afrika Kusini katika kuliwakilisha Taifa kwenye mashindano makubwa kabisa ya Miss World usiku wa jana alifanikiwa kuingia Fainali ya vazi la ufukweni baada ya kuingia kwenye 40 bora katika hatua za awali za mashindano hayo makubwa, fainali ambazo zinataraji kufanyika usiku wa leo.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya dunia, mrembo atakayefanikiwa kuibuka mshindi katika taji hilo la mavazi ya ufukweni anakuwa tayari amepata tiketi ya kuingia katika hatua ya 20 Bora ya shindano kubwa la kumtafuta malkia wa dunia.

Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, Miriam amepata nafasi hiyo ambayo imeshuhudia warembo wengine 80 wakichujwa.

Lundenga alisema kuwa hiyo ni moja ya mafanikio kwa mwakilishi huyo wa nchi kwa sababu ameonekana kuwa ni bora katika vazi hilo.

Alisema pia wanaomba Miriam aendelee kufanya vizuri leo na kupata nafasi ya kuingia hatua ya 20 Bora ya fainali ya mashindano hayo ambayo imepangwa kufanyika Desemba 12 katika jiji la Johannesburg.

Alisema kuwa warembo wote wanaoshinda katika mataji madogo madogo, wanaingia moja kwa moja kwenye hatua hiyo ya 20 Bora ambayo inakuwa rahisi zaidi kushinda taji la Miss World.

Mrembo mwingine aliyeingia katika hatua ya 20 Bora ya mashindano hayo ni kutoka Japan ambaye aliibuka kidedea katika taji la michezo. Mrembo huyo ambaye aliwahi kushiriki katika michuano ya Olimpiki, aliwashinda wenzake katika mbio fupi.

Warembo hao pia walishindana katika kupiga penati.


JB MPIANA KUFANYA ONYESHO TANZANIA

Kwa mujibu wa Secretary General Mbuta Kisolokele tayari jb mipana ameachia single ya generic kutoka katika album yake mpya ya Kis, "Be serious" ambayo inamjumuisha huyo kuingia Tanzania kwa show mwezi ujao .

Jean-Bedel Mpiana Tshituka ni miongoni mwa wanmuziki wanao subiriwa kwa hamu kubwa sana na mshabiki wake wa wenge bcbg inakadiriwa kuwa mwisho wa mwaka huu 2009 mwanmuziki , JB Mpiana atakuwa ameachia album yake hiyo ya "Let’s be serious." Ambayo ndani ina track 15 na moja tu ambayo ndio ya generic alieifanyia katika studio za CEO na kuwa atazindua album hiyo December.


JB Mpiana kiongozi wa kundi kubwa la wenge BCBG pamoja na group yake wanataraji kutua Tanzania kwa show akiambatana na Thsla muana pamoja na bill Clinton ingawa tarehe haijatajwa na kuwa wanaletwa na nani hawakusema ni kwa mujibu wa mtandao wa africanhit.com.




Wednesday, November 25, 2009

BONGODJS PROUDLY PRESENTS CELEBRATION OF TANZANIA INDEPENDENCE

BONGODJS PROUDLY PRESENTS CELEBRATION OF TANZANIA INDEPENDENCE DAY ON SAT 5TH DECEMBER 2009 @PRESTIGEOUS LA ROYALE BANQUENTING SUITES 819-821 HIGH ROAD TOTTENHAM LONDON N17 8ER FRM7PM-3AM FOR ONLY£15 COME AND ENJOY LIVE BAND BONGODJS ON THE MIX,
PS PASS THE MESSAGE AROUND!SPECIAL NITE NOT TO BE MISSED!!!SPONSORED BY SWIFT FREIGHTS UK,TZUK.BONGOTIMES



TOP FIVE BONGO STAR SEARCH KWENYE ALBAMU MOJA


Unawakumba jamaa hawa alitinga kwenye ile top five ya wakali wa BSS kwa mwaka huu, hapa namzungumzia Mshindi namba moja Pascal Cassian, Jackson George, Peter Msechu, Beatrice William na Kelvin Mbati.

Basi yule meneja na kiongozi wa kundi la Tip Top Connection Babu Tale ameamua kuwaingiza studio wakali wote hao kwa pamoja waweze kufanya album ya kufa mtu.

Akiitonya VIJIMAMBO VYA TANGA Babu Tale alisema anaamini jamaa wana uwezo mbaya hivyo hawezi kuacha vipaji vya vijana hao vipotee hivi hivi hivyo basi anatarija kuwaingiza studio waweze kurekodi nyimbo zao ambazo ataziweka kwenye album moja.

Tuesday, November 24, 2009

ALBAMU HAZILIPI BONGO- ASEMA DULLY

Ukipenda muite Handsome, Mr Misifa anakwenda kwa jina la Dully Sykes mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipyaa,ameibuka na kusema kwamba hatarajii wala kutegemea kutoa albam tena kwakuwa albam hazilipi.

Dully aliweka bayana baada ya kumtwanga na swali la kwamba lini ataachia albam na kusema ya kwamba kwake misumari itakuwa ni kuachia wimbo baada ya wimbo na sio kutengeneza albam.

“Albam hazilipi,siwezi kukaa chini na kufiki kutengeneza albam,nitakuwa naachia nyimbo zangu kama navyofanya sasa” alisema Star huyo anayetamba na nyimbo zake kali kama vile Shekide.

D'BANJI WA NIGERIA KURUDI TENA TANZANIA!!!

Coco Master a.k.a D’Banj mwanamuziki anayetamba na nyimbo yake kali ya Fall in Love anatarajiwa kuanguka mwishoni mwa wiki tayari kwa tamasha kubwa kabisa la Str8 Muzik Inter Collage Special linalotarajiwa kurindima ndani ya viwanja vya Tanganyika Packer maeneo ya Kawe.

Akiongea mmoja wa waratibu wa onyesho hilo alisema madhumuni halisi ni ya onyesho hilo ni kuwaleta karibu wanachuo wote kwa pamoja ambao kwa muda mrefu walikuwa likizo pamoja na kuwapa burudani ya kutosha.

“Unajuwa walikuwa likizo ndefu kabisa na juzi juzi tu ndio wamefungua vyuo kwahiyo ni katika utaratibu wa kawaida kabisa wa Str8 Muzik kuwaleta karibu wanachuo hao na pia kuwapa burudani ya kutosha, zaidi ya D’Banj wengine watakaopamba jukwaa ni kutoka nchini Kenya Nonini,Jua Cali, wakati Tanzania atakuwepo TID, Mangwea, na wengine wengi” alisema mratibu huyo.

Katika onyesho hilo ambapo kutakuwa na usafiri wa wanavyuo kwenda na kurudi uwanjani kiingilio ni Tsh 3,500/- tu.

Tuesday, November 17, 2009

MISS UTALII 2009 TANGA- NANI KUIBUKA MNYANGE..??




Shindano la kumsaka mnyange wa Miss Utalii 2009 jijini Tanga linzaidi
kupamba moto huku kila mshiriki akipania kuibuka kidedea. Shindano hilo
lililo na dhana ya kutangaza utalii nchini Tanzania, linatarajia
kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 20 mwaka huu.

Katika pita pita za VIJIMAMBO VYA TANGA kunako baadhi ya mitaa ya
jijini hapa, tayari waaandaji wa mashindano hayo makubwa wameshabandika
matangazo kila kuna ili kuwapa watu habari kuhusu tukio hilo.

Shindano hilo ambalo linatarajiwa kushirikisha karibu warembo tisa,
litafanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort, hoteli mpya na yakisasa
mkoani Tanga iliyopo maeneo ya Sahare.

Kwa mujibu wa waandaji wa mashindano hayo ambao ni RAHA ENTERTAINMENT
pamoja na BREEZ FM RADIO,onyesho la miss utalii linatarajiwa kuanza
majira ya saa mbili usiku huku kiingilio kikiwa ni 25000.
Hata hivyo shindano hilo linatarajiwa pia kupambwa na burudani safi
kutoka wa Kassim, Maunda Zorro, Steve aliyewahi kutamba kwenye wimbo wa
Blue wa tabasamu pamoja na Price Mwinjuma Muumini akiwa na kundi zima
la Bwagamoyo International band lenye maskani yake jijini Tanga
Tanzania.

Pamoja na shindano hilo la Miss Utalii 2009 kuletwa na RAHA
ENTERTAINMENT NA BREEZ FM RADIO, lakini pia kuna wadhamini wengine
ambao ni Tanga Beach Resort, Aurora Security,Silvarado Hotel, Saska
Digital Lab, Tanga Middle Age Veterans.

Gari inayotumika kubebea warembo wa Miss Utalii jijini Tanga

Watangazi wa Breez Fm radio ya jijini Tanga ambao ni moja ya waandaji wa Miss Utalii Tanga, Ben aliyevaa shati jeupe na Tin Daddy mwenye fulana wakiwa kwenye Pozzz

Mkali wa milazo, Dj Bob Nass akiwa na Tin Daddy na Ben





Saturday, November 14, 2009

MH TEMBA, CHEGGE KUPIGA SHOW DUBAI

Machizi wanaoifanya TMK Wanaume Family iwe juu kwa sasa, Amani James Temba ‘Mheshimiwa’ na Said Juma ‘Chegge’ wanatarajiwa kudondoka pande za Dubai na kufanya shoo ya ukweli.

Chegge na Mh. Temba watakuwa Dubai ambapo jukumu lao ni kutoa shoo zitakazofanyika Mwezi huu, mwaka huu lakini Novemba 21 watakuwa Dar na kufanya vitu vikali na kuinogesha Fiesta 2009.

Temba amesema kuwa kila kitu kipo confirmed na kwamba tayari wameshaanza maandalizi ya kupiga shoo hiyo ambayo wamekwishavuta mzigo nusu.


Mbali na hilo, kupitia hapa unaweza kupewa information kuwa video ya wimbo Running Low ya Wahu ambaye ni mtoto wa Kenya na Chegge a.k.a Mtoto wa Mama Said siku chache zijazo itakuwa kideoni.


HAYA NDIO MAISHA YA ELIZABETH BAADA YA BBA REVOLUTION

Aliyekuwa mshiriki wa BBA REVOLUTION Elizabeth akijimwaga kisawa sawa kunako Club ya Billcanas siku ya jana. Nini kitafuata baada ya star huyu kutua bongo..?? Je ataingia kwenye Filamu ili kukuza kipaji chake..? Vipi kuhusiana na skendo za ngono kunako magazeti ya udaku...Hebu tuone itakuwaje.

Wednesday, November 11, 2009

MR PRESIDENT YA ROMA MPANGO MZIMA REDIONI!!


Msanii kutoka jijini Tanga, Tanzania ROMA ama Rymes Of Magic Attraction ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la MR PRESIDENT. Roma ambaye alishawahi kutamba na ngoma ya TANZANIA iliyovuma karibu kila nchi na Afrika Mashariki kwa ujumla amekuja na ujio mpya uliowaacha midomo wazi mashabiki wa muziki wa bongo flava.

Akizungumza na Blog hii, msanii huyo amesema kuwa ngoma ya MR PRESIDENT ilimchukua muda hadi kuifanikisha toka alipotangaza kwani alishafanya kazi producer Duke wa M- Lab Record na ngoma kukamilika. Lakini hata hivyo msanii huyo aliahirisha kui'riliz ngoma hiyo na kuamua kufanya kazi na J Marder wa Tongwe Record iliyopo Masaki jijini Dar Es Salaam.


Roma akipiga story na Anko Mo, alitabanaisha kuwa alichonga na J Marder na kupenda kufanya nae kazi ya MR PRESIDENT- kama moja ya hatua ya kusonga mbele katika maendeleo ya muziki wa bongo flava nchini Tanzania.

Mkali huyo wa Hip Hop kutokea Tanga, Tanzania ameongeza kuwa hadi sasa yupo Tongwe Record chini ya mmiliki wake J Marder na tayari kuna ngoma nyengine anazitayarisha kwa ajili ya kutoka na albamu hapo baadae.


Roma amewataja baadhi ya wasanii ambao anatarajia kuwapa shavu kwenye ngoma zake mpya ni pamoja na Izzo B na Nick Wa Pili ambazo ataziachia very soon.

Mchizi wangu wa ukweli alimalizia kuwa, bado yupo na YUDDI ambaye ni Mixing Producer wake aliyefanya ngoma ya TANZANIA. Mnoma alizitaja baadhi ya redio ambazo hadi sasa zinagonga ngoma yake kuwa ni Mwambao Fm ya Tanga, Breez Fm, Clouds Fm, Times Fm, E.A Radio, Coconut Fm, Magic Fm pia imefika Mtwara, tabora na karibu nchini nzima.


Dizaini mnoma kama amebanwa na skuli, bt amesema kuwa yupo mbioni katika mpango mzima wa albamu punde tu atapokuwa free.

Sunday, November 8, 2009

YOSSOU N’DOUR NA ANGELIQUE KIDJO KUFANYA ONYESHO NCHINI TANZANIA

Wasanii wakubwa kabisa barani Afrika na Ulimwenguni kote, Angelique Kidjo kutoka Benin na Yossou N’Dour wa Senegal, wanatarajia kufanya onyesho lao moja jijini Dar litakalofanyika katika viwanja vya Karimjee, Novemba 15 mwaka huu.

Wasanii hao ambao watatua hapa bongo kwa mwaliko mkubwa wa kampuni ya simu ya Zain Tanzania.

Meneja masoko wa kampuni hiyo Costantine Magavila alisema kuwa onesho hilo ni maalumu kwa wakazi wa Dar, pamoja na watumiaji wa mtandao wa Zain.

Magavila alisema kuwa wasanii hao watakuwa jukwaani kuanzia saa moja usiku hadi saa sita usiku na wanatarajia kuwasili nchini Novemba 13 mwaka huu tayari kwa onesho hilo.

Magavila alibainisha kuwa onesho hilo litatoa nafasi kwa watumiaji wa huduma ya ZAP, kupata punguzo la bei kuwashuhudia wasanii hao ambapo watakaonunua tiketi kwa huduma hiyo watalipia sh 20,000/= badala ya sh. 25,000/= kama watu wa kawaida.

ENJOY VIJIMAMBO VYA TANGA

Saturday, November 7, 2009

FID Q MKALI WA HIP HOP KUPITIA VIJIMAMBO VYA TANGA



Katika shindano lisilo rasmi la kumsaka mkali wa Hip Hop nchini Tanzania kupitia blog hii, limemalizika huku msanii Fid Q akiibuka kidedea.


Shindano hilo lililochukua takribani mwezi mmoja huku ikiruhusu mashabiki na wadau kupiga kura, lilikuwa likiwashindanisha Joh Makini, Langa, Prof Jay, Mabovu, Chid Benz pamoja na Fid Q aliyewafunika wenzake.




Fid Q, mwanamuziki machachari wa muziki wa kizazi kipya alifanyiwa mahojiano na jamaa wa Channel O. Kumbe jamaa wanamnyaka sana tu huyu mshikaji. Safi sana Fid

Prof Jay na Chid Benz walitoka sare kwa kupata kura 3, huku Joh Makini akipata kura 2- Mabovu alipata kura 1 wakati Langa aliambulia patupu. Ni Fid Q pekee ndie aliyeibuka na kura 5 zilizompa ushindi ambao sio rasmi kwa mujibu wa blog hiii. Anko Mo Blogspot imekuwa ikishindanisha wasanii ama kundi la muziki ili kuwapa chachu wadau wa VIJIMAMBO VYA TANGA waendelee kupata burudani. Asanteni wote mliopiga kura, endeleeni kuhabarika.

MPIGIE KURA ELIZABETH ILI UMUOKOE KWENYE JUMBA LA BBA



Africa nameingia kwenye ‘Danger zone’ baada ya kuwekwa ndani ya mchujo,
kitendo kinachoashiria huenda akaaga Jumba la BBA wiki hii (Jumapili).
Eliza ameingia ndani ya mchujo baada ya mkubwa wa jumba wiki hii,
Edward kumuokoa rafiki yake kipenzi na mvuta sigara mwenzake Mzamo,
ambaye alikuwa kwenye orodha ya mstari mwekundu.

Big Brother aliwatangaza washiriki waliopigiwa kura wiki hii na kuingia
kwenye mchujo kuwa ni Nkenna, Emma aliyenusurika kutoka wiki iliyopita
na Mzamo ambaye ameokolewa na rafiki yake.

Hali ilibadilika pale Edward alipoitwa katika chumba cha mahojiano na
Big Brother na kuulizwa ni nani anayetaka kumuokoa, bila kusita
alimtaja rafiki yake Mzamo na kumweka Elizabeth aondoke badala yake.
Kwa hatua hiyo, huenda Eliza akaaga Jumba la BBA wiki hii. Ili
kumuokoa, mpigie kura kwa wingi ili aendelee kutesa na mwisho wa siku
aibuke na ushindi.
Mpige kura Eliza kwa kuandika jina lake (VOTE ELIZABETH) kisha kutuma
kwenda namba 15726.




Thursday, November 5, 2009

MCHUMA UNAUZWA WADAU! WAHI SASA

Hapa kwa nyuma, itazame kwa makini!

Kwa ndani

Kwa mbele ikibinua.

Kwa maelewano contact Mr ABOUBAKAR
E-MAIL:abou73us@yahoo.com
Cell: 0716 985055- 0754 683932
DARESSALAAM- TANZANIA