Wednesday, March 24, 2010
MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU YALIVYOFANYIKA PANGANI KIMKOA!
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Tuesday, March 23, 2010
MASOMO YAMPUMZISHA KEISHA JUKWAANI!
Hofu ya kudunda (kufanya vibaya) kwenye pepa yake ya kidato cha sita imemfanya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini na mwanachama wa Tip Top Connection, Khadija Shaban ‘Keysha’ kuweka kando kidogo masuala ya muziki.Msanii huyo bora wa kike katika tuzo za muziki za Kili, ni mwanafunzi wa Shule ya kimataifa ya Cambridge, akichukua masomo ya Historia, Jiografia na Lugha (HGL), anatarajiwa kufanya mtihani wake wa mwisho Juni mwaka huu.
Akilonga kwa njia ya simu katika kuhusiana na kutoonekana kwake kwenye majukwaa ya muziki, Keysha alisema kunatokana na kutingwa na masomo na hasa ikizingatiwa amebakiza miezi michache kabla ya kufanya mitihani yake ya mwisho.
“Nimetingwa sana na masuala ya kitabu, hivyo imenibidi niweke muziki pembeni, si unajua mshika mawili...hivyo mashabiki wangu wasihofu, nitakapomaliza mitihani nitaingia jukwaani kama kawaida,” alisema.
Keysha ambaye amejipatia umaarufu mkubwa tangu ajitose kwenye ulingo wa muziki wa kizazi kipya, ambako nyimbo alizotoa zimeweza kufanya vizuri, huku tayari akiwa ameishatoa albamu mbili, ‘Usinitenge’ na ‘Keysha’.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
MIKOANI TUNAVYOKUJA KASI KWENYE ANGA ZA BLOG!
Tazama blog ya Mtwara na ujue mambo yote yanayotokea mkoani humo. http://www.mtwaraleo.blogspot.com/ au bonyeza hapa kutembelea blog hiyo.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Monday, March 22, 2010
TIP TOP MZIGONI KWA ALBAMU YA PAMOJA!
Kundi la Tip Top Organization, lipo mbioni kuingia studio kwa ajili ya kufanya wimbo wa pamoja ambao hapo baadae utaingia kwenye albamu yao moja itakayowashirikisha wasanii wote wa kundi hilo.Meneja wa kundi hilo Hamisi Tale a.k.a Babu Tale amesema kuwa, ameamua kufanya hivyo ili kuonyesha upendo wa kutosha kwa wasanii wake ili mashabiki wa wajue kuwa wana upendo wa kutosha katika kukuza sanaa ya muziki wa Bongo Flava.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Friday, March 19, 2010
MITAA YA TANGA TOWN LEO MCHANA!
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Thursday, March 18, 2010
WASANII WENGI WA BONGO FLAVA NI MAJUNGU- Q CHILLAH!

Mwanamuziki mwenye vituko kwenye muziki wa Bongo Fleva Athuman Shaaban Katwila a.k.a Q Chilla ameibuka na kutangaza hata siku moja hatataka urafiki tena na wanamuziki wa kibongo.Q Chilla aliyasema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Radio nchini kwa kuulizwa yeye kumtuhumu T.I.D kuwa anamroga hivyo kushindwa kufanya kazi zake vizuri, habari ambazo ziliripotiwa na vyombo vya habari siku za nyuma.
“Mi nasema sitaki urafiki na mwanamuziki hawa wanaoimba imba kwasababu wengi wao wana majungu na ni wanafiki, wamekaa kimbea mbea tu” alisema Q Chillah bila kufafanua anamlenga nani zaidi.
Hivi siku za karibuni kumekuwa na habari za kutokuelewana baina ya wawili hao ambao walikuwa wakiunda Band moja. Haya wadau wa muziki wa Bongo Flava- kwa mtindo huu tutafka kweli..?
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Tuesday, March 16, 2010
ROMA ATAJWA TUZO ZA TEEN EXTRA AWARD 2010!
Msanii kutoka Tanga City Rymes Of Magic Attraction (ROMA) ametajwa kwenye tuzo za Teen Extra Awards 2010 zinazoendeshwa na kituo cha redio Clouds Fm cha jijini Dar Es Salaam.Roma ametajwa kwenye category ya 15. Lyricist Of The Year ambapo anachuana na wasanii wengine kama Fid Q, Niki Wa Pili, Ngwea, Joh Makini, Jay Moh na G Nako.
I know Tanga tunaweza na ROMA ndie msanii pekee anayestahili kuwa Lyricist wa mwaka kutokana na tungo za ukweli zinazopatikana kwenye ngoma zake zote!
Unachotakiwa kufanya ni kufungua hii website http://www.nipe5.com Utakapoifungua angalia mkono wako wa kushoto kuna sehemu imeandikwa Teen Extra Award hapo utabonyeza kwa ajili ya kuona washiriki wote halafu utaingia kipengele cha 15. Lyricist Of The Year na hapo utabonyeza jina la ROMA.Make it happen kama wewe ni fan wa ukweli wa ROMA kutokea Tanga City! Kumpigia kura Roma bonyeza hapa
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Monday, March 15, 2010
MAZINGAOMBWE YALIVYOTAWALA UWANJA WA TANGAMANO JIJINI TANGA!
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Subscribe to:
Posts (Atom)
