Friday, February 12, 2010
MITAA YA TANGA CITY LEO MCHANA!
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
MPANGO MZIMA WA FELLA KWA MWAKA 2010!
Meneja na mlezi wa kundi la TMK Wanaume Family Said Fella a.k.a Mkubwa Fella amesambaza maelezo na malengo yake kwa mwaka huu 2010 kwa kundi zima la watoto wa Kiumeni. Fella alisema kuwa malengo makubwa kwa mwaka huu kwenye briefcase yake ni kama ifuatavyo.“Kwanza kabisa nitahakikisha naitangaza na kuiuza album ya Saidi Juma a.k.a Chege album yake aliyoitoa siku za hivi karibuni ya karibu kiumeni, pia nitasimamia kama ilivyo kwa Chege album ya kundi ya Wanaume Kazini.
Fella ni mdau mkubwa wa muziki wa bongo fleva ndiye anayesimamia kazi zote za kundi la TMK Family.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Thursday, February 11, 2010
NGUZA VIKING NA PAPII WAFUNGWA MAISHA- WAWILI WAACHIWA HURU!!
Mahakama ya Rufaa Tanzania mapema leo imewaachia huru watoto wawili wa Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi hapa nchini Nguza Viking (Nguza Mbangu wa pili kulia na Francis Nguza wa mwisho kulia) huku yeye mwenyewe pamoja na mtoto wake Papii Kocha wakifungwa maisha.Baadhi ya Watu wamesema kuwa kutokana na kutolewa kwa hukumu hiyo mpaka sasa njia inayoweza kuwaokoa ni kwa Mh. Rais kutoa msamaha kwa makosa waliyoyafanya ya kubaka. Rufaa hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Jaji Masati wa mahakama kuu ambapo hukumu hiyo imesomwa na Neema Chusi Naibu msajili wa mahakama ya Rufaa hukumu.
Aidha hali ya Mahakamani hapo kwa ndugu na jamaa zao walishikwa na butwaa kwa kile kilichotokea huku wengi wao wakilia kwa uchungu.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
TAPA TAPA YA DULY SYKES LIVE JIJINI TANGA TAREHE 26/02/2010
Mkali wa Bongo Flava nchini Tanzania Dully Sykes ambaye anatarajiwa kupiga show jijini Tanga siku ya Ijumaa ya tarehe 26/02/2010 kwenye Club mpya ya Ibiza Carnivore iliyope maeneo ya Donge, amesema kuwa yupo tayari kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa mujibu wa mratibu wa onyesho hilo Ally Mohammed (Bra A) amesema kuwa, siku hiyo kutakuwa na wasanii kibao watakaopiga show wakiwemo Omega Boys, Dula Wa Michano, Bab Lee, Untouchable na wengine kibao. Hivyo anawataka mashabiki na wapenzi wa muziki waweze kufika kunako pande hizo. Kiingilio ni 3000/= tu.
Kwa upande mwengine Bra A amesema kuwa, Dully atapiga live ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Tapa Tapa.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
SMS ZA VALENTINE KWA MPENZI WAKO!
---------------------------------------------------
My soul is shattered without your arms to hold me,
Like a mirror without a reflection. I Love U my Valentine
-----------------------------
My eyes are blind without your eyes to see,
Like a rose without color. Always be there in my life sweetheart.
-----------------------------
Without Love -- days are sad day, moan day, tears day, waste day, thirst day, fright day, shatter day. So be in love everyday...Wish you a Happy Valentine's Day.
-----------------------------
I am opening an emotional bank account for u sweetheart, so deposit your love in it and you will get the interest.
---------------------------------------------------
"I'm enthralled by your beauty, mesmerized by your charisma and spellbound by your love. No wonder I am always thinking about you. I wish to celebrate every Valentine with you. Happy Valentine's Day!
---------------------------------------------------
If I could die early I would ask God if I could be your guardian angel, so I could wrap my wings around you and embrace you whenever you feel alone.
---------------------------------------------------
Love so much my heart is sure. As time goes on I love you more, Your happy smile. Your loving face no one will ever take your place. Wish you a Happy Valentine's Day!
---------------------------------------------------
I ask God for a rose n he gave me flowers;
I ask God for water n he gave me an ocean;
I ask God for an angel n he gave me the best love ever!
---------------------------------------------------
Love can be expressed in many ways. One way I know is to send it across the distance to the person who is reading this.
---------------------------------------------------
To be honest with you, I don't have the words to make you feel better, but I do have the arms to give you a hug, ears to listen to whatever you want to talk about, and I have a heart; a heart that's aching to see you smile again.
---------------------------------------------------
May this Valentine bless us with the cupid of love and warmth of romance. Happy Valentine's Day Honey!
---------------------------------------------------
My heart for you will never break. My smile for you will never fade. My love for you will never end. I love you!
---------------------------------------------------
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
RACHEL MLAKI AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI!!
Rachel ambaye hivi sasa ni mwanafunzi wa chuo cha UDOM, yupo mkoani Kilimanjaro kwa kwa ajili ya kumalizia mazishi ya mama yake, ameonekana ni mtu mwenye majonzi kutokana na tukio hilo la msiba.
"Asante kaka, mama alitokewa na uvimbe kwenye mguu wakamwambia ni Cancer. Wajua hata siamini, leo ndio tumemzika na sijui hata nitaishijie. Nameomba Mungu aniongoze kwani kaniachia wadogo zangu wawiliniwatunze" alisema Rachel ambaye ni mdau mkubwa wa VIJIMAMBO VYA TANGA
Anko Mo Blogspot inakupa pole sana dada yetu mpendwa Rachel kwa msiba uliokukuta, mshukuru Mungu sana kwani msiba hauna mmoja kwani imandikwa kuwa kila nafsi itaonja umauti. Pigana kuhakikisha unatakeleza yale ambayo mama amekuachia.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Wednesday, February 10, 2010
MADEE, TUNDA MAN KUTOKA NA NGOMA MPYA JUMAMOSI!!

Msanii wa kutoka katika kundi la Tip Top Organization la jijini Dar Es Salaam ambaye pia ni raisi wa Manzese Ahmad Ally a.k.a Madee anatarajia kutoa ngoma yake mpya kutokaa kwenye Album yake inayoitwa IT'S ALL ABOUT MADEE ambayo amemshirikisha Ngwear.
Kwa mujibu wa meneja wa kundi hilo Babu Tale ambaye aliipasha VIJIMAMBO VYA TANGA , ngoma hiyo inatarajiwa kutoka siku ya Jumamosi ya wiki hii ikiwa imetengenezwa pale Mj Record producer akiwa ni Makochali.
Wimbo huo utakuwa unaitwa "It's all about Madee' ambao umebeba jina la album.
Kwa upande mwengine Babu Tale amesema kuwa, msanii mwengine anayetokea kwenye kundi lake ambaye ni Tunda Man nae anatarajia kutoa ngoma mpya katika album yake inayoitwa HALI YANGU wimbo ukiwa ni 'hali yangu' ambao kamshirikisha Chegge na Madee ambapo Jumamosi hii wimbo huo unafanhyiwa Video pale kwa Adam Juma.Kundi la Tip Top Organization linasifika kwa kuibua vipaji vya wasanii hasa wa Bongo Flava ambapo hadi sasa linawashikilia wasanii nguli kama Keisher, Kassim, Tunda Man, Madee, na wengine kibao.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
UNAFANYAJE UKITAKA KUIBIWA KWENYE ATM!!

Dear Friends,
Use of ATM Card!
VERY IMPORTANT!!! !
WHEN A THIEF FORCES YOU TO TAKE MONEY FROM THE ATM, DO NOT
ARGUE OR RESIST, YOU MIGHT NOT KNOW WHAT HE OR SHE MIGHT DO
TO YOU. WHAT YOU SHOULD DO IS TO PUNCH YOUR PIN IN THE
REVERSE, I.E IF YOUR PIN IS 1254, YOU PUNCH 4521.
THE MOMENT YOU PUNCH IN THE REVERSE, THE MONEY WILL COME OUT BUT WILL BE STUCK INTO THE MACHINE HALF WAY OUT AND IT WILL ALERT THE POLICE WITHOUT THE NOTICE OF THE THIEF. EVERY ATM HAS IT;
IT IS SPECIALLY MADE TO SIGNIFY DANGER AND HELP. NOT EVERYONE IS AWARE OF THIS.
FORWARD THIS TO ALL YOUR LOVED ONES, FRIENDS AND THOSE YOU
CARE.
Nimeipata kwa dada yangu Jay Dee mtembelee
JAYE DEE
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
STUDIO YA KIMATAIFA YAFUNGULIWA MWANZA!
Katika kuhakikisha kuwa wasanii wa Kanda ya ziwa wanabaki pande zile za Mwanza bila kutoka mkoani humo kwa kuanzisha Studio ya nguvu ya kurekodi.Studio hiyo ambayo ina sifa zote za kuitwa studio ya kimataifa imefunguliwa pande za mitaa ya Rufiji Mkoani kwa Kamanda Rwambow ikiwa na dhana zote za kisasa kabisa ambazo mwanamuziki yeyote anaweza akarekodi kwasasa.
Wanamuziki wengi toka pande hizo za Rock City wamekuwa wakitoka Mkoani humo na kuja Kurekodi anga hizi za kwa Lukuvi (Bongo).
“Unajuwa niliona kuwa wanamuziki wengi Mwanza ni makini hivyo basi nikaona kwanini wasumbuke kila siku kwenda kurekodi Dar ndipo nilipopata wazo la kufungua studio hizi ili niwarahisishie na kweli lengo langu limetimia, sasa wanamuziki wakubwa na hata wale wadogo wataweza kurekodi hapa” alisema mmiliki wa studio hizo Studio hiyo inakwenda kwa jina la ATP, wanamuziki wakubwa kabisa waliotokea pande hizo ni kama Fid Q, Mad Ice, PNC na wengine wengi.
Mpaka sasa wanamuziki waliokwisha kutengeneza nyimbo zao ndani ya studio hiyo ni kama Z-Anton, Bwana Misosi, Geez Mabovu, Chelea Man
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Tuesday, February 9, 2010
LORD EYES APONEA CHUPUCHUPU MIKONONI MWA POLISI
Mwanamuziki toka kundi la Nako 2 Nako lenye maskani yake mkoani Arusha Lordeyez alimaliza weekend yake kwa misukosuko mara baada ya askari polisi kumtia pingu kwa nia ya kumpeleka kituo cha Polisi.Timbwili lenyewe lilikuwa hivi, Lordeyez na mchumba wake mrembo Ray C walikuwa wameharibikiwa mitaa ya MK Bar maeneo ya Mwananyamala na Kinondoni, mara ghafla wakapita Polisi ambao walikuwa kwenye doria ya kawaida ndipo msela akastuka ghafla na kufunga kioo na hapo ndipo polisi wakastuka kujiuliza kulikoni.

Jamaa wakageuza gari na kwenda walipo wapenzi hao wawili na kuwakuta na kuomba kuwafanyia upekuzi ndani ya gari yao ambapo Lordeyez alitia ngumu na ndipo polisi hao walipomkamata kwa nguvu na kumtia pingu kisha kumpeleka kituoni kwa upekuzi zaidi.
Lakini bila kupata chochote polisi hao hawakuambulia kitu na kumwachia mshikaji huru.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Monday, February 8, 2010
DULLY SYKES KUPIGA SHOW TANGA 'KAA TAYARI!!'
SIKU: IJUMAA YA TAREHE 26/01/2010
CLUB:IBIZA CARNIVORE MAENEO YA DONGE
KIINGILIO: 30000/=
INALETWA KWENU KWA UDHAMINI WA ANKO MO BLOGSPOT NA OMEGA PAMBA SHOP
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
AMERICANS PROVIDE 7 BILIONI SHs FOR TANGA- HOROHORO ROAD
The American people are supporting the upgrading of the 65km Tanga-Horohoro road. The project is being implemented through the Millennium Challenge Account (MCA-Tanzania).The road will be covered with bitumen. The work on the Tanga � Horohoro
road is the first of six different road segments that will be rehabilitated
and upgraded under the Mainland Trunk Roads project, which is part of the $698.136 million MCC Compact.
According to the press release by the US Embassy, representatives from the Millennium Challenge Corporation (MCC), regional and local officials and representatives from the Tanzania Roads Authority (Tanroads) visited the site.
Last December, Sinohydro won the tender for construction works contract after an open international competition. The total value of the contract award was nearly Sh69.9 billion ($ 53.8 million).
The work will be conducted under the overall supervision of MCA-Tanzania and Tanroads, assisted by personnel from the International Consultants and Technocrats Pvt (ICT).
ICT was awarded its construction supervision contract by MCA-Tanzania
in September 2009. Other roads being financed under the Compact includes Tunduma to Laela; Laela to Sumbawanga; Peramiho Junction to Mbinga; and Songea to Namtumbo.
Construction contracts for all these roads are in place and the procurement
process for the remaining work contracts is now well underway. "Top quality firms from around the world have already passed the first procurement phase and been pre-qualified for the second and final bidding stage," the statement read.
MCC and MCA-Tanzania expect to award the five remaining works contacts
for the Mainland Trunk Roads project over the next few months. The Mainland Trunk Roads project is only one of several important transport sector activities underway under the MCC Compact between the United States of America and the United Republic of Tanzania that went into effect in September 2008.
Other projects in the transport sector include an upgrading of up to 36 km of rural roads in Pemba and the improvements to Mafia island airport.
The MCC Compact also includes major components that will provide significant assistance in the energy and water sectors. The American people will provide
a total of $698.1 million in US assistance under the Compact through September 2013.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Sunday, February 7, 2010
HAPPY BIRTHDAY DJ BOB NASS!
Nasir Thabit a.k.a Dj Bob Nass wa Breez Fm Radio ya jijini Tanga, leo tarehe 7/02 anatimiza miaka kadhaa. Happy Birthday kaka!! Endelea kufurahia maisha na uzidi kumuomba mungu.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Friday, February 5, 2010
Thursday, February 4, 2010
KAA CHONJO NA AINA MPYA YA WIZI WA MKONONI!!
Wizi wenyewe huwa hivi unapigiwa simu na watu ambao wanajidai wao ni ajenti wa kusajili number za simu toka kampuni fulani ya simu halafu wanakuambia uwape details zako kama vile ni watu wangapi unapenda kuwapigia mara kwa mara ili kuhakiki, sasa basi ukishawapa wao wanakwenda kwenye kampuni za simu na kudai warudishiwe line zao kama vile simu zao ziliibiwa.
Baada ya sakata hilo ndipo wanasubiri simu zako zinapoita wao huzikata na kutuma meseji ya kuomba watumiwe kiasi fulani cha pesa kwa madai kuwa watarudisha kama hivi “Nipo kwenye Kikao siwezi kuongea, hebu nitumie laki 1 nitakurudishia mara nitakapotoka hapa”.
Au anaweza kupokea na kudai mwenye simu katoka kidogo akirudi atampigia, au wakati mwingine watatumia ubabe kwa kudanganya mwenye simu hiyo ametekwa hivyo watume hela upesi ili aachiwe.
Kaa Chonjo usikubali kutapeliwa.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Wednesday, February 3, 2010
UNAPENDA MOVIE ZA KUTISHA!!?? TAZAMA HII "SILENT HILL"
Wadau, jana usiku baada ya kazi nikachukua DVD ya hii movie na uitazama. Kwa kweli ilinivutia sana kwa namna ambavyo ilichezwa, ila inatisha sana!
Star katika hii movie ni huyu dada katika picha, anaitwa Radha Mitchell ila humu alicheza kama Rose Da Silva, ameonyesha ujasiri wa hali ya juu baada ya kwenda kwenye mji wa Silent Hill ambako kuna mambo ya kutisha
Radha akiwa kwenye action. Movie hii imetengenezwa mwaka 2006 ikiwa imeongozwa na Roger Avary
Huyu mtoto anaitwa Jodelle Ferland, ila alicheza kama Sharon DaSilva na Alessa Gillespie. Washiriki wengine katika movie hii ya Silent Hill ni Laurie Holden ambaye alicheza kama Cybil Bennett, Sean Bean alikuwa mume wa Rose, alicheza kama Chris DaSilva, Tanya Allen kama Anna pamoja na Alice Krige yeye alicheza kama Christabella.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
"MAUMIVU YA MIAKA 10"- WAGOSI WA KAYA
Wakali wa kutoa vidonge vya ukweli katika kuleta chachu ya maendeleo katika Taifa Letu Wagosi wa Kaya toka hapa Tanga wamerudi tena kwa spidi ile ile kipindi hiki wakiwa na jiwe jipya linalokwenda kwa jina la “Maumivu ya miaka 10”.Wakiongea na VIJIMAMBO VYA TANGA Wagosi wakaya kundi linaloundwa na wakali wawili, walisema huo ni moja ya ujumbe wao kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
“Unajuwa ndio kipindi cha watu kudanganyika lakini sisi tuko karibu na wananchi tutawaweka sawa na kuelewa wapi pakwenda, tunajulikana kama wazee wa Displini basi tunaendelezea” alisema Mgosi.Wagosi wa Kaya walijulikana zaidi kwa nyimbo kama Tanga Kunani, Trafiki, Kero, Wauguzi na nyingine nyingi.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Tuesday, February 2, 2010
PROPAGANDA YA FID Q MTAANI FEB 25!
Mwanahiphop makini Farid Kubanda 'Fid Q', anatarajia kuingiza kitaani albam yake ya pili inayokwenda kwa jina la Propaganda Februari 25 mwaka huu.Kubanda alisema kuwa amekuwa kimya kwa muda mrefu hivyo alikuwa katika maandalizi ya albamu hiyo ambayo anatarajia itakuwa ya aina yake kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya.
Alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu hiyo kuwa ni pamoja na Propaganda, Usinikubali Haraka aliyoimba na Matonya, Ripoti za Mtaani aliyomshirikisha Zahir Zorro, Mtaua Gem aliyomshirikisha Juma Nature, Juhudi aliyoimba na Bi. Kidude, Kila Siku aliyomshirikisha QJ, Wananiita King aliyomshirikisha Nailon wa Manzese Crew, na Mwana Malungi.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
"ALBUM IPO TAYARI"- PIPI
Mwanadada anayefanya Kolabo pengine kuliko mwanamuziki yeyote yule wa Kike kwasasa Doreen Aurelian a.k.a Pipi ametanabaisha ya kuwa album yake iko tayari na soon wapenzi wake wakae mtaani kuisubiri.Akiongea katika mahojiano maalumu Pipi alisema album iko tayari na ina jumla ya nyimbo 10 lakini akasema bado hajaipa jina album hiyo mpaka hapo atakapokubaliana na uongozi wa THT.
Zaidi akaongea yakuwa kwasasa soon ata-release single yake mpya inayokwenda kwa jina la Usinune ambao amefanya na mkali mwengine kutoka THT Barnabas ambaye alikula shavu nae kwenye songi lililowatoa la Njia Panda.
Alimaliza kwa kusema studio alizofanyia kazi ni Bongo Record, BHirtz, 59 Records na sehemu nyingine.
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
MWANDISHI WA HABARI "JERRY MURO" LUPANGO
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Jerry Muro (pichani juu kulia) kwa tuhuma za kudai fedha kwa njia ya vitisho.
Muro anadaiwa kumtisha aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo Michael Wage ambaye hivi karibuni alisimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa tuhuma za ubadhilifu pamoja na viongozi wengine wa Halmahauri ya Wilaya Bagamoyo.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Suleimani Kova alikiri jeshi lake kumshikilia Muro na kuwa alimtishia Wage kuwa yeye ni Ofisa wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) na kumtaka atoe fedha Sh milioni 10.
“Polisi inamhoji Muro dhidi ya tuhuma hizo na mahojiano yakikamilika taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na maelezo zaidi nitayatoa kesho wakati wa mazungumzo yangu na waandishi wa habari” Kova alisema.
Aidha blogu ya Watu ilimwona Bingwa huyo wa Tuzo za Uandishi wa Habari 2009 Tanzania akiwa polisi na mkononi ameshikilia bahasha tatu pamoja na kamera ya Video.
Ilipomhoji juu ya kuhusika na tuhuma hizo alikana na kudai kushangazwa kuwekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa alipigiwa simu na mtu kupewa taarifa kuwa kuna kazi katika Hoteli ya City Garden.
“Kaka nilitaarifiwa tu kama ujuavyo kazi zetu kuwa kuna kazi City Garden niakaamua kwenda, lakini baada ya kufika tu nilishangaa nawekwa chini ya ulinzi na askari kanzu ambao ndiyo walionifikisha kituoni hapa bila ya kunitajia kosa lanmgu. ” alilonga Muro.
Kwa upande wake Wage alidai kuwa mtuhumiwa anatumiwa na watu wengine ambapo juzi alimpandisha katika gari lake na kumfunga pingu kisha kumtaka atoe Sh milioni 10 na kwa kuthibitisha kuwa alikuwa ndani ya gari hilo alidai kuacha miwani yake yenye mikanda myeusi.
Polisi ilipomhoji Muro kama anazo pingu alikiri kumiliki pingu pamoja na bastola ambapo baada upekuzi katika gari lake lenye namba za usajili T 545 BEH polisi walikuta pingu hizo pamoja miwani iliyosemwa na mlalamikaji.
Muro ameibuka kuwa mtangazaji mahari kwa mwaka 2009 hadi kujinyakulia tuzo ya Mwandishi bora wa mwaka kupitia vipindi vyake vya Televisheni vya USIKU WA HABARI vinavyorushwa katika kituo cha TBC1 kila siku na kabla ya kuhamia hapo alikuwa kituo cha ITV na aliendesha kipindi cha RIPOTI MAALUM.
Miongoni mwa mambo aliyokuwa akirusha katika vipindi hivyo ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ukiukwaji wa sheria.
Polisi ni wahanga wakuu katika vipindi hivyo kwani mara mbili amewatoa Polisi Usalama barabarani wakiomba na kupokea rushwa hadharani kutoka kwa madereva wa malori na mabasi ya mikoani. Habari kwa hisani ya Father Kidevu
Labels:
Mwandishi: ANKO MO
Monday, February 1, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)



