BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, April 12, 2010

NAKAAYA AJIUNGA NA CHADEMA!

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Nakaaya Sumari juzi alitangaza rasmi kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwa na nia ya kuwahamasisha vijana kujitambua zaidi na kutetea haki zao za msingi na demokrasia kwa ujumla.

Mwanamuziki huyo wa kike, aliyewashangaza watu wengi mkoani humo kwa kuwa wa kwanza kujiingiza katika masuala ya kisiasa, bila kuhofia ama kuogopa kazi zake zinaweza kushuka kiwango, alisema, ataweza kuendesha shughuli zake za muziki na siasa pia.

Nakaaya alijiunga mapema juzi, mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali na kusema kuwa kwa muda mrefu alikuwa na kiu kubwa ya kujiunga katika chama cha siasa chenye mwelekeo, dira na nia nzuri ya kusaidia wananchi wake, ambapo aliona CHADEMA ndicho chama pekee ambacho kinaweza kutimiza ndoto zake za kujiingiza katika masuala ya siasa.

“Kwa kipindi cha muda mrefu nimekuwa na kiu ya kujiingiza katika siasa, ili kuweza kuwahamasisha vijana wa Kitanzania kujitambua na kutetea haki zao za msingi, hasa kwa demokrasia bila kununuliwa ama kushurutishwa na vyama, ambavyo havina msaada wowote katika maisha yao,” alisema Sumari.

Alisema, kutokana na Tanzania kuwa na vivutio vya kutosha, kuwawezesha wananchi wake wote kuondokana na umaskini, lakini hadi hivi sasa, anashangazwa na chama kilichopo madarakani kushindwa kutatua shida na adha kubwa ya umaskini zinazowakumba Watanzania, ambao wengi wao ni maskini.


“Nchi yetu ina rasilimali za kutosha kabisa, hasa kwa upande wa madini ya Tanzanite ambayo yatosha kuwawezesha wananchi wote kuwa katika kiwango bora na kinachostahili kimaisha, mbali na vivutio vingine vya kitalii vilivyopo, lakini cha kushangaza mpaka hivi sasa, wapo Watanzania ambao wanaishi katika hali duni kimaisha na chini ya dola moja kwa siku,” alisema.

Alisema, amejiunga na chama hicho hivi sasa na si mwaka jana ama mwaka juzi, kutokana na kuona hivi sasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, jamii itamhitaji zaidi katika kuwahamasisha juu ya kujitambua katika haki zao za msingi, hasa katika masuala ya kisiasa.

Vyombo vya habari vilimhoji mwanadada huyo kwa nini katika hatua za kwanza kwa lengo lake la kuamua kuingia katika siasa, ameamua kujiunga na chama hicho badala ya kuingia Chama tawala (CCM), au Chama cha Jamii (CCJ), alijibu kwa mshangao kuwa hajaona kama ni vyama ambavyo vipo kwa ajili ya kusaidia watu, bali ni kwa maslahi yao binafsi.

Nao viongozi wa chama hicho mkoa, waliupongeza uamuzi wa msanii huyo kwa uthubutu wake wa kujiunga katika masula ya siasa bila woga wa aina yoyote ile, huku wakimuahidi kumruhusu kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi, pindi atakapotimiza masharti na taratibu zote ndani ya chama.

Viongozi hao walimkabidhi kadi ya uanachama na kumtaka kuwa makini sana, hasa katika kuhamasisha vijana wenzake, huku akiwashawishi wasanii wengine kuingia katika siasa na kuongea yale yote yanayostahili kwa haki kwa manufaa ya nchi yao.

"Ukiwa kama kijana mdogo sana na msanii ambaye ni kioo cha jamii, tunataka tuone bidii yako ya kuweza kufichua na kukemea maovu yote, utakayoyaona ndani ya vuguvugu la kisiasa ndani ya nchi yetu, ili jamii nayo iwe na imani na wanasiasa wake," alisema mmoja wa viongozi hao wa CHADEMA.

Aidha, waliwataka wasanii wote nchini ambao wana uchungu wa kweli katika nchi yao, kujiunga kwa wingi katika chama hicho, ili kuweza kufikia na kutimiza lengo la kuwakomboa wananchi walio wengi masikini na sauti za wanyonge kusikika, hasa katika suala zima la kutatua matatizo yao ikiwa ni pamoja na umaskini.

MISS TANGA 2010 YAZINDULIWA RASMI!

Wakurugenzi wa kampuni ya 5 Brothers Entertainment Asma Makau na Nassoro Makau wakizindua rasmi mashindano ya urembo ya Miss Tanga kwa ngazi ya vitongoji, ambapo kwa safari hii kutakuwa na vitongoji saba tofauti na mwaka jana. Vitongoji hivyo ni Miss Usagara, Miss NGamiani, Miss Chumbageni, Miss College, Miss Tanga City Central, Miss Lushoto na Miss Pangani ambayo inaandaliwa na Anko Mo Blogspot.

Wachangia mada mbali mbali wakati wa uzinduzi wa Miss Tanga. Bra A wa Mwambao Fm na Mimi (Anko Mo) wakati nawakalisha mchango wangu kunako Hoteli ya Kola Prieto iliyopo katikati ya jiji la Tanga.

Warembo wakifuatilia hoja za wajumbe wengine kwa makini zaidi.

Tina wa kwanza, ambaye anandaa Miss Usagara akiwa na Raymond Minja kutokea Mwambao Fm na huyo aliyekunja swala anaitwa Paulina Mgonja.

Wadau wa urembo wakiwa makini katika kusikiliza, mama Sophia Production na wadau wengine.

Mdau mkubwa Miss Tanga ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi Burhan Yakub akigawa mikataba kwa waandaji wa Miss Vitongoji.

Muandaaji wa Miss Chumbageni dada Suzy akiwa na mwandishi wa gazeti la Bingwa na mtangazaji wa Mwambao Fm Oscer Assenga, wakati wa uzinguzi wa Miss Tanga.

Warembo wakizungumza kitu punde baada ya uzinduzi huo kumalizika.

Watangazaji wa Breeze Fm Benson na Amir wakiiwakilisha redio yao. Breeze Fm inandaa Miss Ngamiani. Kauli mbiu ya Miss Tanga 2010 ni "Its Wonderful Event"

MITAA YA KOROGWE LEO ASUBUHI!

Maeneo ya stendi ya mabasi wilayani Korogwe leo asubuhi.

Hoteli maarufu ya High Way iliyopo Korogwe.

Soko la Korogwe.

Baadhi ya mitaa

Friday, April 9, 2010

SANAA INAVYOZIDI KUCHUKUA KASI JIJINI TANGA!

Muuzaji wa sanaa mbali mbali za michoro, ushanga, nguo, mabegi, mikanda, picha za ukutani n.k akipanga vitu vyake kabla ya kuanza kazi.

Baadhi ya sanaa zinazopatikana kwenye duka lake. Yupo chini ya jengo la Club La Casa Chica, karibu na ofisi za Zantel.

Vijago kama vinavyoonekana pichani. Inaonyesha ni jinsi gani alivyo mbunifu.

Ushanga na baadhi ya urembo mwenigne wa sanaa vikiwa dukani.

Nilipomuuliza imekuwaje hadi ukaamua kufanya biashara hii ya sanaa- akanambia kuwa Tanga ya leo sio ya kipindi hicho. Mji umekuwa na watu wanafurahia bidhaa zake.

Vyote hivi ni kazi ya mikono yake.

Wageni na wenyeji mnakaribishwa kununua sanaa za Tanga.

Picha safi kwa ofisini na nyumbani pia.

Karibuni Tanga!

Thursday, April 8, 2010

TULIPOTOKA NA TUNAPOKWENDA!

Tulichofanya ni kuongeza "SIFURI MBILI" (00). Kwahiyo miaka ijayo tukiongeza tena mbili basi tutakuwa na karatasi ya milioni moja!!! Na hii itakuja kama hatutajibihidisha kuuza pamba, kahawa, chai n.k. kwa wingi zaidi nje. Sasa hivi hakuna tena uwiano wa kati ya export na import kwa sababu tumeamua iwe hivyo baada ya kuwapuuzia wakulima wetu wa mazao ya biashara na kuviua hata vile viwanda vyetu, kama vile vya nguo.

Badala yake sasa tuna wajasilimali wengi wanaokwenda China na kwengineko kutuletea bidhaa ambazo tungeweza kuzitengeneza wenyewe kwa malighafi tuliyonayo. Ni aibu kila ninapoona hata vijiti vya kusafishia meno(toothpicks) tunaagiza nje... Kile kiwanda cha vibiriti cha Kibo vipi?

Ikiwa kama madini yote tumewapa wajanja, sisi tumebaki na nini cha kuweza kutuinua? Au utalii ambao bado kuutangaza ipasavyo?

Uchaguzi unaokuja uwe ni uchaguzi wa kuwauliza wagombea ni nini wataifanyia Tanzania?

Asante Fundi Wa Kombo

Wednesday, April 7, 2010

PANGANI INAVYOZIDI KUPIGA HATUA KATIKA ELIMU!

Sheikhe mkuu wa Baraza kuu la waislam Tanzania BAKWATA Sheikhe Isa Saabani Bin Simba akiweka jiwe la msingi leo katika ujenzi wa shule ya sekondari inayojengwa na BAKWATA eneo la Mkoma Wilayani Pangani kwa ufadhili wa benki ya dunia ya kiislam.

Sheikhe Isa Saabani Bin Simba akitazama kwa makini kibao kinachoonyesha kuwa ni yeye ndie aliyeweka jiwe hilo la msingi.

Sheikhe Isa Saabani Bin Simba akisindikizwa na baadhi ya viongozi wa BAKWATA mkoani Tanga wakati anakwenda kuweka jiwe la msingi.

Kama unavyoona pichani.

Viongozi wa BAKWATA wakimkaribisha naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mh Mwantumu Mahiza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika sekondari mpya wilayani Pangani mkoani Tanga.

Mh Mwantumu Mahiza akisema jambo kwa wakazi wa Pangani waliohudhuria hafla hiyo.

Sheikhe Isa Saabani Bin Simba nae akisema jambo.

Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa makini wakifuatilia yaliyokuwa yanasemwa na viongozi wao.

Karibu mgeni! Sheikhe Isa Saabani Bin Simba akikaribishwa Pangani.

Sheikhe Juma Luuchu akikaribisha wageni

Picha wa pamoja na baadhi ya viongozi wa BAKWATA!

SERIKALI YARIDHIA ALBAMU YA WAGOSI WA KAYA

Wakali wa maneno ndani ya Sanaa ya Muziki wa Kizazi Kipya, Fred Malick ‘Mkoloni’ na Dk. John wanaounda Crew ya ‘Wagosi wa Kaya’ wameibuka na kuipigia makofi hatua ya serikali kuruhusu kwenda kitaani kwa albamu yao mpya ya inayokwenda kwa jina la ‘Miaka Kumi ya Maumivu’ iliyokuwa imepigwa stop awali.

Akiongea hivi karibuni, katikati ya wiki iliyopita, Mkoloni ambaye ni mmoja wa wasanii wa kundi hilo, alisema sababu ya kufungiwa mwanzoni ilikuwa ni kuwepo kwa baadhi ya nyimbo ndani ya albamu hiyo, zenye mashairi yanayohofiwa kuchochea vurugu wakati wa Uchaguzi Mkuu, baadaye Oktoba mwaka huu.

“Tulilazimika kukubaliana na agizo la serikali na kubadili aina ya maneno tuliyokuwa tumeyatumia ili kupata baraka za kupeleka mzigo sokoni na hatimaye tumefanikiwa,” alisema Mkoloni.

Akaongeza: “Naamini hadi serikali imekuwa makini kuangalia albamu nzima, basi wanafahamu moto wetu.”

Tuesday, April 6, 2010

PANGANI SASA KIMEELEWEKA! KIVUKO KIPYA HICHOOOOOO!

Hatimae kero ya muda mrefu ya wa'Tanga waishio wilaya ya Pangani imekwisha baada ya kivuko kipya cha Mv Pangani kuanza kufanya kazi rasmi siku ya leo (asubuhi).

Nahodha wa kivuko kipya cha Mv Pangani akiwa kazini wakati kivuko hicho kilipoanza kufanya kazi rasmi ya kubeba abiria.


Wananchi wa Pangani wakisubiria kushuka kwenye kivuku hicho ambapo kwa siku ya leo walipata bahati ya kupanda bure ikiwa kama 'karibu mgeni'

Wakiteremka taratibu.

Shukrani kwa serikali kwa kutambua kero ya wananchi wake. Usalama wa watu na mali zao sasa ni wa uhakika.

AKUDO ILIVYOWASHA MOTO JIJINI TANGA SIKU YA PASAKA

Wazee wa masauti Akudo Impact wakipiga show kunako ukumbi wa Mkwakwani VIP...katika shamra shamra za sikukuu ya Pasaka.

Mimi (Anko Mo) na Matonya

Wadau wa muziki wa dansi- huyo mwenye miwani ni Oscar Assenga ambaye ni mwandishi wa habari gazeti ya Bingwa pia ni mtangazaji wa Mwambao Fm Radio akiwa na Mkali Luppa pia ni mtangazaji wa Mwambao Fm.

Wadau wengine jijini Tanga. Jamaa wa pembeni kabisa ni Matonya, alikuja kula raha za nyumbani na wana wa Akudo.

NO BEEF!! Benson wa Breeze Fm Radio na Bra A wa Mwambao Fm Radio, waki'show love na Akudo Impact.

Mpiga gitaa wa Akudo akiwa kazini.

Huyu dada tulikuwa nae nyuma ya stage- mnenguaji wa Akudo! Ana kipaji cha pekee, anaimba ile mbaya!

Mkurugenzini wa 5 Brothers Entertainment Nassoro Makau alikuwepo.

Tonya akiwa makini wakati show ya Akudo inaendelea. Alikuwa aki'show love kwa watanga wote coz ni mtu wa watu.

Wapenzi wa Akudo wakifuatilia show.

Bella na waimbaji wengine wa Akudo jukwaani.

Wanenguaji wakiwa kazini.

Bella alifanya kazi ya zidia coz baadhi ya rapa wa bendi hiyo kuwa na matatizo. Bella aliimba na ku'rap!

Hapa kazi tu! Mpiga gitaa wa akiwa makini.

Allan Kabasele
Mpiga ngoma akionyesha tabasamu na kufurahia kazi yake. Tanga ilikuwa raha tupu siku ya Pasaka.

Nyuma ya stage- madada wa Akudo

Hakika Akudo Impact iliweza kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Dansi kutokea jijini Tanga.