BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, August 9, 2011

MKAA TUFE- NISHATI MBADA ILIYOANZA KUTUMIKA LUSHOTO


MIONGONI mwa suala yanayotishia uhai wa viumbe na mimea duniani hivi sasa ni suala la mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa kwa ujumla. Mabadiliko hayo chanzo chake kimetokana na uharibifu wa mazingira asilia unaoendelezwa na binadamu wakati anapojishughulisha ili kutafuta maendeleo pasipo kuzingatia kanuni za uasilia. Matokeo ya jumla ya shughuli hizo ni kuongezeka kwa joto duniani linalosababishwa na kasi ya uzalishaji wa gesi ya ukaa katika anga na kuathiri uhai wa Binadamu, viumbe hai wengine na mimea pia.

Athari kubwa itokanayo na mabadiliko ya Hali ya Hewa ni kupanda kwa kiwango cha joto duniani ambako husababisha mabadiliko katika nchi na kuleta matukio yenye athari hasi kwa binadamu kiuchumi na kijamii. Athari mbalimbali zimeendelea kuonekana katika maeneo tofauti tofauti duniani ikiwemo hapa Tanzania na kuanza kufifisha matumaini ya kiuchumi ya wananchi wengi katika maeneo mbalimbali hasa ikizingatiwa kwamba wengi kati yao wanategemea sana shughuli za kilimo na uvuvi kupata kipato.

Pamoja na mambo mengine kimsingi zimepunguza kasi ya utekelezaji wa shughuli muhimu za kiuchumi ambazo katika maeneo mengi zimekuwa zikitegemea uwepo wa bahari, mito na maziwa, mvua za uhakika pamoja na misitu. Matokeo ya mabadiliko hayo yamevuta hisia tofauti kwa taifa na wanaharakati mbalimbali wa mazingira kuanza kujaribu kuhamasisha jamii kupunguza shughuli hasi za kiuchumi na kijamii kwa mazingira kama mbinu ya kupunguza kasi ya vitendo vinavyochochea.

Kutokana na uzito wa matokeo hayo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, kwa kushirikiana na wanaharakati wa masuala ya mazingira imeanzisha kampeni maalumu ya kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kama njia ya kukabili tatizo. Lushoto ndiyo wilaya pekee katika mkoa wa Tanga iliyokuwa ikiongoza kwa kuwa na msimu mrefu wa baridi kwa mwaka, ikilinganishwa na maeneo mengine ya wilaya saba zilizosalia ambazo kwa pamoja zinaunda mkoa huo. Wenyeji wa wilaya hiyo wanabainisha kwamba ilikuwa ni jambo la kawaida kwa Mvua ya Barafu kunyesha kwenye maeneo mengi ya wilaya hiyo.

Hapakuwepo na msimu wa joto kutokana na uwepo wa misitu minene, iliyokuwa imefunika Tao la Milima ya Usambara Magharibi. Wanasema ni katika miaka ya hivi karibuni ndipo waliposhangaa kuona hali ikianza kubadilika na kushuhudia ukame unavyokausha mazao katika baadhi ya mashamba, kuanza kwa msimu wa joto ambao awali haukuwepo kabisa sambamba na idadi kubwa ya wananchi kuugua ugonjwa hatari wa Malaria unaoenezwa na Mbu ambao wanapenda kuishi zaidi kwenye maeneo yanye joto kali.

Wanasema hayo yote ni matokeo ya wananchi kujihusisha na shughuli za kijamii na kiuchumi kama vile uchomaji ovyo misitu, ukataji wa miti kwa ajili ya kuni, kuchoma mkaa, mbao na magogo, kilimo katika vyanzo vya maji pamoja na uchimbaji wa madini shughuli ambazo licha ya kuwaongezea kipato, sasa zimewatumbukia nyongo na kuanza kuwataabisha. Tegemeo kubwa la wakazi wa wilaya ya Lushoto ni kilimo cha matunda, mboga mboga na biashara ambavyo tayari vimeanza kuathiriwa na mabadiliko hayo ya tabianchi.

Majira ya mwaka yanabadilika kiasi kwamba ratiba ya mvua haieleweki, hasa kwa vile wakati na kiasi cha mvua za masika na vuli kunyesha hakitabiriki kutokana na ujio wa Kiangazi ambacho sasa kimeingia kwa kasi katika maeneo mengi ya wilaya hiyo na kusababisha jua kuwa kali badala ya baridi na mvua za barafu. Aidha, shughuli za kijamii ikiwemo kuongezaka kwa idadi ya watu ambao wanahitaji maeneo zaidi ya makazi na kilimo kwa namna moja au nyingine kumechangia matokeo hayo kutokana na ukweli kwamba ujenzi wa makazi unahitaji ardhi pamoja na rasilimali misitu ili kukamilisha makazi.

Kutokana na kupanuka kwa mji na makazi kumeshawishi ongezeko la mahitaji ya kupata nishati ya uhakika kwa ajili ya kupikia ikiwemo kuni na mkaa yameongezeaka wilayani humo hali ambayo kidogo kidogo inaendelea kuchochea uharibifu wa mazingira hasa katika misitu. Hivyo basi, Katika kukabiliana na changamoto hizo za uharibifu wa mazingira taasisi isiyo ya kiserikali kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo ya wilaya wanatekeleza Kampeni hiyo maalum ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha jamii kupunguza athari hasi kwa kusisitiza matumizi ya Nishati Mbadala kwa kupikia.

Kampeni hiyo ki msingi inalenga kuwaelimisha wananchi wa wilayani humo namna ya kupokea mabadiliko hayo na kutafuta mbadala wa matumizi ya nishati za kuni na mkaa kuanzia ngazi ya kaya ili kusaidia kuwajengea wananchi uwezo zaidi kwa sababu bado wanategemea kuendesha maisha kwa kutumia uwepo wa misitu ya milima ya Usambara. Kupitia kampeni hiyo, wananchi wanaelewesha sera zilizopo, faida na umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuhimiza matumizi ya nishati ya mkaa mbadala wa kupikia maarufu kama mkaa tufe (briquettes), tofauti na mazoea yaliyojengeka miongoji mwa jamii ya watanzania ya kutumia kuni na mkaa kupikia.

Ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na kuenezwa katika maeneo mengi ya mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla Wanaharakati hao wa masuala ya Mazingira ambao ni Kampuni ya Environmental Engineering (EEco) Ltd, inaanzisha kiwanda cha kutengeneza kwa wingi Mkaa Tufe mjini humo. Aina hiyo ya nishati itakayozalishwa na kiwanda hicho, haina tofauti na ile inayotengenezwa sasa na baadhi ya vikundi vya wanawake wajasiriamali wadogo walioko wilayani humo, ambao awali walipatiwa teknolojia hiyo na kuanza kuzalisha mkaa tufe kwa matumizi ya kaya katika vijiji wanamoishi. Mkaa tufe uwezo mkubwa wa kuhifadhi mazingira kutokana na kumudu kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya kuni na mkaa nyumbani tofauti na hali ya mahitaji ilivyo sasa katika kaya nyingi za wilayani humo na katika makazi yaliyoko mjini.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo yenye makazi yake wilayani hapa, John Nshunju, akizungumza kwenye mahojiano maalum hivi karibuni amesema mkaa tufe ni rahisi kwa kuwa unatengenezwa kwa kutumia teknolojia rahisi ya kuchanganya takataka za shambani, majani, karatasi, vumbi la mbao au mpunga na maji kwa kutumia mashine maalumu iitwayo ‘divider’. “Ni aina ya mkaa tofauti na ule ambao tumezoea kuuona, Mkaa Tufe unaundwa katika umbo la vipande vya mviringo vyenye tobo katikati ili kuruhusu hewa kupita kwa urahisi wakati wa kuuchoma, mkaa huu unafaa kutumiwa kwenye jiko la aina yoyote likiwemo la kuni,” anaeleza.

Mkurugenzi huyo anabainisha kuwa kipande kimoja cha mkaa huo, ambacho kwa sasa kinauzwa kwa bei ya Sh 100 kina uwezo wa kumudu kuchemsha chai inayotosha kunywewa na watu watatu kwa wakati mmoja na kudai nishati hiyo licha ya kuboresha mazingira inasaidia kupunguza gharama za fedha kwa ajili ya kununua mkaa kwa matumizi ya kaya kwa siku. “Mkaa tufe pamoja na kutumika kuhifadhi mazingira pia unasaidia kupunguza gharama za kununua mkaa na kuni nyumbani mathalani kwa wastani kwa siku moja hapa Lushoto familia inauwezo wa kutumia mkaa wa kati ya Sh 800 hadi Sh 1,000 kupikia chakula cha familia lakini kwa kutumia vipande vinne tu vya mkaa tufe vinamtosheleza mama kuandaa chai na chakula cha familia ikiwemo kuchemsha maharage yanayoweza kuliwa na watu wanne,” anasema.

Anasema tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo miaka mitano iliyopita, wamefanikiwa kufundisha na kuwezesha mtaji midogo kwa vikundi vitatu vya wanawake, ambayo kwa kutumia mashine ndogo za mkono sasa wanazalisha na kuuza mkaa tufe kwa jamii zinayowazunguka. Kampuni ya Environmental Engineering (EEco) Ltd inaamini kwamba kupatikana kwa kiwanda hicho Lushoto, kutaongeza uzalishaji mara dufu wa nishati hiyo ili baadaye iweze kufikia wananchi wengi zaidi, kwa sababu malighafi ipo nyingi na inapatikana bure.




Thursday, August 4, 2011

MADAKTARI BINGWA KUFANYA UPASUAJI BURE TANGA

Jopo la madaktari bingwa tisa kutoka Shirika la Interplast la Ujerumani linatarajiwa kuendesha huduma za upasuaji wa kurekebisha sura na maumbile kwa wakazi wa mkoa wa Tanga wenye matatizo hayo.


Huduma hiyo itatolewa bure kwa siku 15 mfululizo kuanzia Julai 31 hadi Agosti 14 mwaka huu kwa kuhusisha madaktari hao watakaoshirikiana na madaktari wengine wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Tanga, mratibu wa upasuaji huo, Dk. Wallace Karata alisema utahusisha midomo iliyopasuka, kaa kaa lililopasuka, makovu sugu yanayozuia muonekano na utendaji kazi wa viungo mbalimbali pamoja na uvimbe mwilini.


Dk. Karata alisema, matibabu hayo yatatolewa bure kwa kuwa shirika hilo limegharamia vitu vyote muhimu kwa ajili ya kufanikisha matibabu hayo isipokuwa gharama za usajili wa mgonjwa pamoja na kulazwa.


“Kwa mara ya nne sasa shirika hilo litaleta jopo la madaktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha viungo mbali
mbali hapa mkoani kwetu Tanga, tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi tena mwaka huu kwa kuwa matibabu yatatolewa bure.


“Kila mgonjwa atachangia Sh 1,000 ya kusajili kadi pale hospitali ya Bombo,” alisema na kuongeza kuwa kwa wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji mkubwa, watalazimika kuendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa madaktari.


Tangu kuanza kutolewa kwa matibabu hayo kwenye Mkoa wa Tanga, mwaka 2008 hadi mwaka jana tayari wagonjwa 119 wamefanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbile yao huku wengi wao wakiwa ni watu wazima.


Na Anna Makange, Tanga

AUAWA KWA KUUA WATOTO WAWILI KWA SHOKA

MKAZI wa kijiji cha Misima, Rashidi Maglasi (35), ameuawa na wananchi akituhumiwa kuwaua watoto wawili kwa kuwakata kwa shoka vichwani na kuwajeruhi wazazi wao.


Tukio hilo lilitokea hivi karibuni baada ya Maglasi kuwaua Ridhiwan Bakari (6) aliyekuwa na baba yake Bakari Mokiwa (53) ambao walikuwa wakitokea hospitali kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo. Katika tukio hilo, muuaji huyo alimjeruhi baba wa mtoto huyo.


Habari zaidi zinasema kwamba baada ya tukio hilo, muuaji huyo alikimbia umbali mrefu kidogo ndipo alipokutana na Mwajiha Mwalimu akiwa na mtoto wake Gumbo Mukwagu (4) ambapo aliendeleza mashambulizi hayo na kumuua mtoto na kisha kumjeruhi mama yake.


Baada ya tukio hilo, Mwalimu alipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walipotokea na kuanza kumshambulia muuaji huyo hadi kufa. Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Masawe, alisema huenda muuaji alikua na matatizo ya akili, jambo ambalo bado halijapatiwa uthibitisho.


Hata hivyo wazazi wa watoto hao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Handeni wakiendelea na matibabu na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Auawa kwa kuua watoto wawili kwa shoka.

Na Bertha Mwambela, Handeni, Tanga

Wednesday, August 3, 2011

COASTAL UNION USO KWA USO NA MTIBWA SUGAR LIGI KUU


Timu ya Coastal Union ya Tanga iliyopanda daraja msimu huu itakutana na Mtibwa Sugar kwenye raundi ya kwanza ya mechi za ligi kuu kunako uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani. Mechi nyingine za raundi ya kwanza zitakuwa kati ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Kaitaba, Bukoba), Polisi Dodoma na African Lyon (Jamhuri, Dodoma) na Azam na Moro United (Chamazi, Dar es Salaam).

Raundi ya kwanza itamalizika Agosti 21 mwaka huu kwa mechi kati ya JKT Oljoro na Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha na Yanga dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mzunguko wa kwanza (first leg) wa ligi hiyo utamalizika Novemba 5 mwaka huu wakati mzunguko wa pili (second leg) utamalizika Aprili Mosi mwakani ambapo jumla ya mechi 175 zitachezwa.

Pambano la watani wa jadi kati ya Yanga na Simba litafanyika Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi ya mzunguko wa pili ambapo Simba itakuwa mwenyeji itafanyika Aprili Mosi mwakani kwenye uwanja huo huo.

NGORONGORO HEROES YAALIKWA COSAFA
Timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) imealikwa kushiriki michuano ya umri huo ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwaka Afrika (COSAFA) itakayofanyika kuanzia Desemba 1-10 jijini Gaborone, Botswana.

Wachezaji wanaotakiwa kushiriki michuano hiyo ni wale waliozaliwa baada ya Januari 1, 1992. Timu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kufikia Agosti 17 mwaka huu na ratiba itapangwa Agosti 24 mwaka huu jijini Gaborone. COSAFA itachangia sehemu ya nauli ya timu shiriki kwenda kwenye mashindano hayo.

Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Kim Poulsen akisaidiwa na Adolf Rishard hivi sasa inafanya mazoezi ya wiki moja kila mwezi.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Tuesday, August 2, 2011

FAIDA YA FUTARI YA TENDE NA MAJI


Assalam alaykoum,

Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) ametufundisha namna ya kufturu na vyenye faida katika miongoni mwa futari.
Kufuturu ni kitu cha kwanza kinachofungua kinywa cha mfungaji mara baada ya kumaliza muda wa kufunga katika siku husika. Kifungua kinywa hiki cha mwanzo ndio huitwa futari.
Nabii wa karne hii ya sayansi na teknolojia ametuhusia sana Waislaam tunapokuwa tumefunga, ni vyema kufturu kwa tende au maji.


Mafundisho haya ya Mtume Muhammas (S.A.W) yamekuwa kinyume kabisa na namna waislaam wengi wanavyofungua saumu zao.
Watu wengi wanapofungua saum zao hukimbilia kula vyakula vya nafaka kama vile uji, juice, tambi, katlesi n.k. Pamoja na kufuturu vitu hivo vizito katika tumbo, huwa mfuturuji wa vyakula vingi mwisho hushindwa kuhema uzuri.Kuhusiana na kula Mtume Muhammad ametuhusia sana tumbo tuligawe sehemu tatu kuu nazo ni:-MajiChakulaHewa.
Utaratibu huu wakulipa nafasi tumbo kwa chakula, maji na hewa unasaidia sana katika mfumo wa usagaji wa chakula.Tende na maji ni vitu vilivyotajwa sana kwa matumisi ya mfungaji wa saum na mzazi pia.


"Basi akachukua mimba yake akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali kisha uchungu ukampelekea katika shina la mtende, akawa anazaa huku anasema laiti ningelikufa kabla ya haya na ningelikuwa niliyesahaulika kabisa, mara ikafika sauti chini kutoka chini yake ikamuambia usihuzunike Maryaam hakika Mola wako amejaalia kijito cha maji chini yako. Na litikise shina la mtende kwako litaangusha tende nzuri zilizoiva basi ule, unywe na liulie jicho lako furahi na pumua moyo wako." (QUR-AAN 19:22-26)
Kutokana na mafundisho hayo ya Quraan inaonesha tumbo la mtu aliyezaa linahitaji tende au maji kama ilivyo mtu mwenye kufunga.


Jambo la kujiuliza hekima ipi Mtume ameitumia katika kutufundisha kula tende na maji na sio kula vyakula vizito.Vyakula vya nafaka kama vile mbaazi,viazi,maandazi n.k ni vyakula vizito husababisha maumivu katika tumbo.
Hali hii hutokana na ukweli kuwa katika ukuta wa tumbo la chakula na hata katika utumbo mwembamba kuna maji mazito mfano wake kama ute wa yai la kuku, maji hayo yanasaidia aina mbali mbali za acid zisifike katika ngozi ya tumbo na kufanya michubuko ambayo yanaweza kuleta ugonjwa wa vidonda vya tumbo.Kuta za tumbo zinapokutana na acid husababisha eneo hilo kutepeta na kulifanya liwe laini.


FAIDA YA TENDE NA MAJI: katika tende na maji kuna madini mengi yanayoambatana na sukari na hewa ya oxygen. Vitu vinapofika katika eneo hili vinasaidia kupunguza nguvu ya gas, gas ambayo ikizidi hatima yake huleta matatizo na magonjwa.
Kwahio Inshallah ftari yetu ya mwanzo iwe ni tende kwa maji kisha utafuatilisha machopochopo mengine ambayo machoopochopo hayo yasiwe yakushibisha kiasi ambacho mtu ukashindwa hata kuswali taraweh.


KUTOKUFUNGA MWEZI WA RAMADHANI

Kufunga Ramadhani ni nguzo ya nne katika nguzo tano za Kiislamu na kutokufunga Ramadhani bila udhuru wowote ule wa kisheria ni moja ya madhambi makubwa sabini. Mwenyezi Mungu S.W.T. kautukuza sana mwezi wa Ramadhani kuliko miezi yote mingine kwani imeteremshwa Qurani katika mwezi huu mtukufu na pia kajaalia kuwepo katika mwezi huu usiku wa Lailatul-Qadri usiku wa heshima, usiku ulio bora kuliko miezu elfu.


Kufunga katika mwezi huu mtukufu ni faridha wajibu kwa aliyetimiza masharti yake, kama ilivyokuwa faridha wajibu kwa wale waliokuwa kabla yetu. Na yule atakaeacha kufunga siku moja tu bila sababu yoyote ile ya kisheria kama vile ugonjwa au safari, basi atakuwa amefanya madhambi makubwa. Na akifa katika hali hiyo basi atakuwa amefanya dhambi kubwa na adhabu yake ni kubwa nayo ni Moto wa Jahannam. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Baqarah aya ya 183 na ya 184, "?يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمْ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ * أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ¦?


Maana yake, "Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumchaMungu. Siku chache (kufunga huko), basi atakaekuwa mgonjwa miongoni mwenu au katika safari (akafungua) basi (atimize) hesabu katika siku nyingine."Na pia Hadithi iliyopokelewa na Ibn `Umar R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari na Muslim, Mtume S.A.W. kasema, ""بُنِيَ الإسْلامُ عَلَى خَمْسٍ : شَهَادَةِ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ وَصَوْمِ رَمَضَانَ وَحَجِّ الْبَيْتِ."Maana yake, "Umejengwa Uislamu kwa nguzo tano, (nguzo ya kwanza):


Hapana mungu mwenye kupasa kuabudiwa ila Allah, na hakika Muhammad S.A.W. ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na (nguzo ya pili): Kusimamisha Sala, na (nguzo ya tatu): Kutoa Zaka, na (nguzo ya nne): Kufunga (mwezi wa) Ramadhani na (nguzo ya tano): Kuhiji (nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa yule mwenye uwezo)."Sahaba Ibn Abbaas R.A.A. kasema, ""عُرَى الإِسْلامِ وقواعد الدين ثلاث : شَهَادَةِ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ ، والصَّلاةُ ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ."Maana yake, "Uislamu pamoja na kanuni za dini zimefungamana na mambo matatu: Shahada ya kuwa hapana apasae kuabudiwa (kwa haki) ila ALLAH na Sala na kufunga mwezi wa Ramadhani."

Monday, August 1, 2011

ANKO MO BLOGSPOT INAKUTAKIA MFUNGO MWEMA WA RAMADHANI

Anko Mo Blogspot inakutakia mfungo mwema wa Ramadhan.

Thursday, July 28, 2011

VIJANA WA TANGA TOWN!

Msanii mashuhuri wa muziki wa Bongo Flava kutokea Tanga Dk Leader aliyevaa fulana nyeupe akiwa na washkaji zake. Katikati ni The Don pamoja na Producer wa Huruma Records ya jijini Tanga anafahamika kama Andrew.



Hapa ni maeneo ya Chumbageni wakati camera ya Anko Mo ilipowakuta wakibadilishana mawazo.

CLUB LACASA CHICA NI BURUDANI MWANZO MWISHO JIJINI TANGA!









WHITE PARTY



Wednesday, July 27, 2011

ALBINO KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

KATIKA kukabiliana na dhana potofu iliyojengeka katika jamii dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwamba hawana uwezo sawa na wengine, Josephat Torner ameamua kuvunja ukimya kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.

Anatarajia kuanza safari yake hiyo itakayomchukua siku nane, Jumamosi wiki hii kuelekea kileleni kwa lengo la kuithibitishia jamii ambayo bado inaendeleza vitendo vya ukatili na unyanyapaa dhidi ya albino kwamba wao wanaweza kufanya kila kitu.

Torner ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari na kusema lengo pamoja na kufikisha ujumbe huo muhimu ni kuwa albino wa kwanza Tanzania kufanya kitendo hicho cha kishujaa cha kufika kwenye kilele cha Kilimanjaro, mlima mrefu barani Afrika.

“Nipo mbele yenu hapa leo kuweka msimamo dhidi ya mawazo potofu yaliyopo katika fikra za baadhi ya Watanzania na Waafrika wengi ambao wanaamini kwamba albino hana uwezo sawa na watu wengine, fikra hizi ni hatari zimeendelea kusababisha ubaguzi, kutengwa, ukatili na mauaji dhidi yetu kwa muda sasa,” amesema.

“Jumamosi ya Julai 30, mwaka huu, nitaanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro lengo kuu ni kufikisha haki za albino kileleni mwa Afrika na kutangaza kwa sauti kubwa niwezavyo kwamba albino sio mtu wa kuogopwa, kubaguliwa, anayestahili kuwindwa kama mnyama wa porini akikatwa vipande kwa ajili ya biashara, bali ni binadamu kama wengine.”

Torner amebainisha kuwa, uamuzi wake huo umetokana na kasi ya vitendo vya ukatili na mashambulizi yanayoendelezwa na baadhi ya Waafrika kutokana na imani za kishirikina zilizochochea biashara ya viungo vya albino na kusababisha madhara mengi kwao hasa kulazimishwa kuishi kwa wasiwasi.

“Nitakapopanda mlima nitapanda kwa ajili ya albino wote waliolazimishwa kuondoka nyumbani kwao kwenda kuishi kwenye kambi maalumu zinazowatenga na familia zao na kuwapa upweke na kuwaambia iwe mwisho wa kujificha kwenye kivuli cha jua tena, ndoto yangu ni kuunganisha albino wote ili tuuthibitishie ulimwengu tuna uwezo sawa na binadamu wengine ila tunatofautishwa na mahitaji,” amesema.

Takriban miaka mitano sasa, hali ya albino nchini imekuwa si shwari kutokana na kasi ya ushambuliaji, uwindaji na mauaji ya kikatili yaliyosababisha vifo zaidi ya 60, huku Serikali ikilazimika kuhamisha wanawake na watoto 118 katika shule maalumu ili kuimarisha ulinzi na usalama wa maisha yao dhidi ya wawindaji.


Na Anna Makange, Tanga.

Monday, July 25, 2011

PROFESSOR JAY AND DITTO MEET WITH STUDNETS IN TANGA USING PERFORMANCE TO FIGHT MALARIA

On the 21stof July, students from ten schools came together at Usagara Secondary School in Tanga town to take part in malaria themed song, theatre and poetry competitions. The competition was a part of the Zinduka! club initiative, in which youth are empowered with the knowledge and tools to drive forward the fight against malaria in local communities.

The judges were treated to a spectacle of talent as they witnessed an array of performances including poetry readings, songs and even theatrical performances
On reaching the final round, Tanzanian artist, Ditto, took to the stage to talk to the students about how important it is to protect themselves from malaria to ensure they secure their future, before the artist sang the malaria he had written for the Zinduka! campaign which has now become an anthem for a generation fighting against malaria.
The students were then surprised when another guest Bongo fleva rapper and Zinduka! goodwill ambassador Professor Jay joined Ditto on stage to sing the anthem.

The artist has been a prominent figure in the fight against malaria, featuring in the launch of the Zinduka! campaign in 2010 and making regular appearances for the campaign in the field and on TV.Professor Jay then took time to hand out awards to the lucky competition winners.

Professor J had this to say, “I joined the Zinduka! campaign with the hope that through my music I could help to fight malaria in Tanzania. But to see kids wanting to get involved and using music as the platform to fight malaria in their communities, that’s what makes me most proud of the work we have done.
Professor Jay and Ditto then invited youth to join him as he visited a number of houses near Tanga town, where the youth spoke to households about what measures they use to protect themselves from malaria and what they think needs to be done to eradicate malaria in Tanzania.

The Malaria Haikubaliki Campaign is led by the Tanzanian Government behind the leadership of President JakayaKikwete. It is supported by partners including Malaria No More, Tanzania House of Talent (THT), Johns Hopkins University, Population Services International and United Against Malaria. The goal of the program is to achieve universal bed net coverage and eliminate malaria deaths by urging all Tanzanians to Zinduka! (“Wake up!”) to the threat of malaria and protect themselves against the disease

SERENGETI FIESTA 2011 NI FULL MAJOTROOOOO


Wananchi wa Tanga wakifurahia Serengeti Fiesta 2011 iliyofanyika jijini Tanga siku ya jana Jumapili ya tarehe 24/07/2011 kwenye uwanja wa Mkwakwani......hakika ilikuwa bonge moja la show! wakazi wa Tanga walijitokeza wka wingi na majatrooo yaliwabamba vilivyo.



Dayna akifanya vitu vyake jukaani

Mimi pamoja na mashosto wa kitanga


Mataaluma akitoa burudani



Sheta akionyesha umahiri wake wa kucheza



Mwana Fa akiangusha burudani.



Dj Bulla ndio alikuwepo kwenye moja na mbili



Belle ( kwa stage akitoa majotroooo


Mzee wa dushelele Ali Kiba kama kawa akiwakilisha



Thursday, July 21, 2011

HATIMAE JAIRO KIBARUA KIMEOTA NYASI!

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, amesimamishwa kazi rasmi kufuatia kutangazwa rasmi habari hizo na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemo Luhanjo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Kutimuliwa kazi kwa Jairo kumekuja baada ya Beatrice Shelukindo mbunge wa Kilindi Mkoani Tanga kulipua bomu Bungeni akimtuhumu Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini juu ya kutumia zaidi ya Sh 1 bilioni kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge.

Wednesday, July 20, 2011

HAWA NAO WATAKUWEPO KWENYE SERENGETI FIESTA 2011 PALE MKWAKWANI SIKU YA JUMAPILI

Msanii wa hip hop anafahamika kama Godzila, ni miongoni mwa wasanii watakaokuwepo siku ya jumapili ya tarehe 24 mwezi 7 pale Mkwakwani katika Serengeti Fiesta 2011.

Anaitwa Mataaluma wakazi wa Tanga wanaisubiri mama mubaya kwa hamu ndani ya Serengeti Fiesta 2011 Mkwakwani siku ya Jumapili.

Linex karibu sana Tanga.

Joh Makini atapiga show mwanzo mwisho.

Belle 9 kutoka Moro mpaka Tanga ndaani ya uwanja wa Mkwakwani siku ya Jumapili.

Bob Junior raisi wa Masharobaro kama kawa ndani ya Mkwakwani kwenye Fiesta.

Prof Jay. Msanii mkongwe kwenye Bongo Flava nae atakuwepo Tanga kwenye Serengeti Fiesta 2011 Mkwakwani.

Linah kutoka THT nae atakuwepo kuwakilisha Fiesta.

Ali Kiba pia atakuwepo kwenye Serengeti Fiesta 2011 kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Anaitwa Top C ni msanii wa Bongo Flava anayefanya vizuri hivi sasa. Nae atakuwepo siku ya jumapili. Top C asili yake ni mkoani Tanga, hivyo wakazi wa Tanga kaeni tayari kumpokea.

SHELUKINDO ALIVYOFUNGUKA BUNGENI!

Beatrice Shellukindo

Beatrice Shellukindo amelipua bomu Bungeni akimtuhumu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kwa kutumia zaidi ya Sh 1 bilioni kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge.

Tuhuma hizo nzito zinakuja kipindi ambacho tayari Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini wakiwa wameibua tuhuma kama hizo za baadhi ya wajumbe kutaka kuhongwa na maofisa wa wizara hiyo, ili kurahisisha upitishaji wa bajeti ndani ya kamati.

David Jairo

Takriban wiki tatu tangu wabunge wa kamati hiyo kuibua tuhuma hizo ambazo zilifika hadi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hivi juzi tena Shellukindo alikoleza moto huo wakati akichangia bajeti ya wizara.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikubaliana na tuhuma hizo. Akitoa hoja ya kuondoa bungeni hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini, Pinda alisema alikuwa akisubiri Rais Jakaya Kikwete afike Afrika ya Kusini alikokwenda katika ziara ya kiserikali ili aweze "kumshtaki" Katibu Mkuu huyo kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake. Pinda alisema hawezi kuchukua hatua dhidi ya Jairo kwani kwa mujibu wa sheria, mamlaka ya uteuzi ndiyo inayoweza kuchukulia hatua dhidi yake.

Beatrice Shelukindo ni mbunge wa jimbo la Kilindi mkoani Tanga kupitia chama cha mapinduzi.

Tuesday, July 19, 2011

SERENGETI FIESTA 2011 INAKUJA TANGA JUMAPILI YA TAREHE 24/07/2011

Roma ni mmoja kati ya wasanii wa Hip Hop wanaotokea Tanga ambaye atakuwepo kwenye Fiesta kuuwakilisha mkoa wa wake. Kupitia Anko Mo BlogSpot utapata kuwajua wasanii wote watakaopanda kwenye Serengeti Fiesta 2011 kunako uwanja wa Mkwakwani. Tunaanza na wasanii wanaotokea Tanga.

Mwana Fa ambaye asili yake ni kule wilayani Muheza. Pia atakuwepo siku ya jumapili kwenye uwanja wa Mkwakwani na atapiga show mwanzo mwisho. Wasanii wengine watakaopanda siku hiyo utawapata kuwaona hivi punde. Endelea kutembelea Blog.

KIJANA AANGUKA NA KUPOTEZA FAHAMU AKIJARIBU KUKWEPA NYAYA ZA UMEME

Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alianguka na kupoteza fahamu katika eneo la Gofu hapa jijini Tanga karibu kabisa na ofisi za mkuu wa mkoa. Kwa mujibu wa wapita njia wengine waliomuona wakati anaanguka, walidai kuwa kijana huyo alikuwa akijaribu kukwepa nyaya za umeme zilizokuwa zimeanguka barabarani. Tukio hilo lilitokea siku ya jana majira ya saa mbili asubuhi.

Wasamaria wema wakimtazama kijana aliyeanguka huku wakijadili namna ya kumsaidia.

Mzee huyu alijitoa mhanga kwa kuzitoa nyaya za umeme zilizoanguka barabarani na kufanya kijana huyo kuanguka na kupoteza fahamu. Mpaka naondoka eneo la tukio, kijana huyo aliweza kupata msaada na kupelekwa hospitali ya Bombo.

Monday, July 18, 2011

TIMU YA DALADALA ILIVYOFANYA KAZI YA KUREKODI VIPINDI MKOANI TANGA

Tayari timu nzima ya kipindi cha daladala kimeshafanya baadhi ya vipindi mkoani Tanga, ambapo vipindi hivyo utakuja kuviona kwa luninga yako kupitia televisheni ya ITV kila siku kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa moja jioni.

Maswala mbali mbali kuhusiana na mgao wa umeme, maendeleo ya bandari ya Tanga- wananchi wanaionaje. Swala la elimu na mmomonyoko wa maadili pia vimezungumziwa katika moja ya vipindi vilivyorekodiwa na timu ya daladala iliyotua jijini Tanga.

(Pichani mimi na Daniel Kijo, mtangazaji wa kipindi cha daladala)

Nikiwa mmoja wa watu walioshiriki kutoa maoni mbalimbali katika kipindi cha daladala, kwa kweli katika mijadala yote niliyoishuhudia wakati wa kurekodi vipindi- wananchi wa mkoa wa Tanga wameonyesha ushirikiano wa kutosha na wengi wamezungumza kwa hisia kwa kile ambacho kilikuwa kinawagusa moja kwa moja.

(Pichani Daniel akiwa na mdau wa kipindi cha daladala, barabara ya nane)

Safari ilianzia Mwahako mpaka eneo la stendi ambapo walipanda abiria wengine na mjadala kuendelea. Badae tena daladala ilikwenda eneo la Magomeni na kisha wanafunzi wa chuo kikuu cha Tanga cha Eckenford nao walipata nafasi ya kutoa maoni yao pia kuhusiana na swla zima la elimu huku bwana Kombo ambaye ni afisa wa elimu ya sekondari wilaya ya Mkinga akiwa chachu ya mada hiyo.

(Timu ya kipindi cha daladala wakiwa na afisa elimu Kombo wakati wa kuelekea kurekodi)

wananchi wa Tanga wakae mkao wa kula kutazama vipindi vilivyotengenezwa kutokea hapa Tanga kuanzia leo tarehe 19 siku ya jumanne kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa moja kujua mengi kuhusiana na mkoa wa Tanga.

(Daniel kwenye bustani za Tanga)

Eldad Mark Film Director akiwa na Deogratius Sizya Camera man wa kipindi cha Daladala pamoja na afisa wa elimu za sekondari wilaya ya Mkinga Bwana Kombo wakijiandaa na mahojiano.

Kipindi cha daladala pia kilikutana na rais wa Eckenford Tanga University bwana Amos Fide na kufanya nae mahojiano. Pichani ni Daniel Kijo, Eldad Mark pamoja na Fide.

Vijana wa Kazi.

Mimi nikiwa na Bibi Kiroboto. Bibi mcheshi huyu sijapata kuona. Hapa tukiwa Tanga Televisheni kwa ajili ya mahojiano na kuwapa taarifa wananchi wa Tanga juu ya ujio wa daladala. Ukiiona tu, unakimbilia na kupata kisha ukifika ndani unatoa maoni yako!! Daladalaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Daladala ni kila kona bwana! Hapa ni katika kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh. Bibi kiroboto akiwa na dereva wa daladala bwana Emanuel Zing pamoja mwenyeji wetu bi Winfrida Magawa aliyesimama.

Daniel Kijo akibadilishana contacts na baadhi ya wakuu wa kiwanda cha Tanga Fresh

Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo tulipofika Tanga Fresh.

Daladalaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Kwa mbali daladala ikionekana na jengo kubwa la kiwanda cha Tanga Fresh

Tulifika pia Eckenford Tanga University.

Huyu mama alitupa raha sana! Alistaajabu alipomuona bibi Kiroboto. wacha amkumbatie bwana! Raha kuwa na daladala!

Baadhi ya wanafunzin wa Eckenford Tanga Univertisty wakibadilishana mawazo za timu ya daladala.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Eckenford Tanga

Wanafunzi wakiingia kwenye daladala

(Timu nzima ya Daladala iliyokuwepo jijini Tanga ni pamoja na Dani Kijo na Bi Kiroboto ambao ni watangazaji. Wengine ni Eldad Mark Film Director, Emanuel Zing Driver, Deogratius Sizya Camera man, Tanya creative producer, Anton second driver na Steve Martin researcher.)