Wednesday, July 29, 2009
HAYA NDIO MAMBO YA TANGA JAMANI- TAZAMA HII NYUMBA!!!
Saturday, July 25, 2009
CP KUTOKA NA PWAA III- KAA TAYARI!!!
Ikaja Pwaa Part ngoma iliyosimamiwa na Mtu mzima Lucci ambapo ilimpeleka CP katika Level nyingine kabisa, Level za kimataifa, kwani kiukweli ukiangalia au kusikiliza ngoma ya Pwaa Part2 utakubali ya kuwa CP alifanya kazi ya ziada kuanzia utunzi wake mpaka shooting ya Video yake ilikuwa katika “another Level”, ili kuwapa wapenzi na washabiki wake mautamu zaidi na kuonyesha nini amekusudia mchizi muda si mrefu ataachia songi lake la Pwaa Part3.
Bila kuweka kazi ni nani na nani watakaokuwa wamesimama kwenye ngoma hiyo, Cp alisema ya kuwa huo ni mwendelezo wa ngoma yake hiyo ambapo kwa madai yake mwenyewe mchizi amesema anatarajia kuifanya tofauti zaidi, na habari za ndani zinasema kuna Pwaa kibao zinakuja, sasa mpenzi na mshabiki wa CP na muziki wa Bongo Fleva kwa ujumla kaeni mkao wa kula kumsikiliza na kumuona jamaa ubunifu zaidi na zaidi.
THE NGOMA AFRICA BAND WAPATA TENA DILI- SASA KUPIGA SHOW UJERUMANI.
Ras Makunja, kiongozi wa bendi hiyo akionyesha makeke yake.
The Ngoma Africa Band aka FFU! Kukiwasha cha moto kingine ndani ya
AFRILU Festival, Ludwigshafen City,Germany siku ya Ijumaa 24.7.
Kamanda Ras Makunja atakiongoza kikosi cha The Ngoma Africa Band aka FFU katika jukwaa lingine la onyesho la AFRILU .Onyesho hilo litakalo fanyika siku ya ijumaa 24.07.2009 jioni katika uwanja wa Ebert Park,mjini Ludwigshafen,huko Ujerumani,ambako washabiki wengi wanasubiri kucheza gwaride na ffu wa Ngoma Africa band.habari za uhakika zinatonya kuwa Karandinga la FFU hao linapiga misele na kwenda kwa kasi kuelekea katika maonyesho hayo!
ambapo washabiki watapata burudani ya aina yake.
Usikose kupata mziki hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica pia unaweza kuwasiliana na ffu at ngoma4u@gmail.com
Monday, July 20, 2009
WAGOSI WA KAYA NA TANGA KUNANI...!! JAMAA WAPO KIMYA SANA JAMANI
Kwa wale ambao wamekuwa wafatiliaji wakubwa wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, hakika watakuwa wanawafahamu WAGOSI WA KAYA- vijana mahiri wa muziki huo kutokea hapa jijini Tanga.
Kwa hakika walibamba sana na staili yao ya ki'lugha....kwa maana ya kisambaa na kidigo, hawa wa Dr John na mwenzake Mkoloni. Unakumbuka ngoma zao kama TANGA KUNANI, WAUGUZI, TRAFIKI HAYAAAA!!, KEROOO, SOKA LA BONGO na nyengine kibao tu!!
Baada ya kukumbuka nyimbo hizo, jiulize ni kiasi gani zilikubamba na je sasa hivi wapo wapi na wanafanyanini...!!??? Ukimya wao umeonekana kuwagusa watu wengi ambao kwa namna moja ama nyenigne walikuwa tayari wameshazama kwenye dimbwi la upendo wa nyimbo zao ambazo zilikuwa zinagusa moja kwa moja jamii ya kitanzania.
Kwa hapa Tanga jamaa walikuwa kama akina P Square wa kule nchini Nigeria, si mtoto wala mkubwa- kila kona utasikia TANGA KUNANI kama vilivyo VIJIMAMBO VYA TANGA kwa sasa. Duh....jamani mmekaa kimya sana wagoshiiiii, tunaomba mrudi tena ili tufurahie tena ladha zenu za kisambaa na kidigo.
HAYA NI MASHAIRI YA WIMBO WA TANGA KUNANI!!
Wagosi wa Kaya - Tanga kunani?
(verse 1)Tanga kwa kweli ni kijimji kidogo, na pia kuna mambo ya uswahili si kidogo. lakini habari zake kwa kweli ni kubwa, na mji ule ukiuvamia kwa papara palee, mengi yatakukumba! Ukifika Tanga utatambuaje kama kweli huu nd'o mkoa wa Tanga?Utaona wanawake wengi palewamejifunika mabaibui na vijikanga. Waume makanzu baraghashia, mkononi tasibihiwanakuhesabia.
Baiskeli ndiyo teleeee, mpaka zawakera wenye magari barabaraniHalafu hali ya sasa sii kama ile yazamani, ukaenda ovyo tu utauza kila kitu chako cha thamani.Matajiri wa enzi zile ukiwaonaleo hii tena hawana thamani Enzi zile bwana mkoa wa Tanga kilakitu mambo yalikuwa swafi. Mijikazi ilikuwa tele, na kulikuwa hakuna mambo yaukorofi, lakini sasa hivi thubutu, twendelea kuchakaa mpaka tutoke ukurutu, hakuna ndimaa, kilo mtuambiwa ajifanya mvuvi ati, na ukamshauri mtu akushushia varangati, astaghafirullai laadhim!Watu waongea peke yao kamavile wendawazimu, labda tutambikemizimu huenda kidogo pale mamboyakany'oka. Palikuwa na viwanda na mashamba ya mkonge telee. Haviwapi sasa? Utafikiri mamiye mwali aliyefunga kizazi bwana, maana havizalishi ati, vyote viko, nyang'anyang'a. Hali hii kutupa vitu njia panda, yaonyesha kabisa tayari maisha yeshatushinda. Watu kilo siku waenda kwa waganga, ukipita pale mara kumevunjwa nazi, mara huku nako kule kumetupwa hirizi, mwatakani basi nyiye wana msiotulia?
KIITIKIO
Tanga, kunani paleee, mbona kila kitu pale kimekufa, Tanga, kunani paleee, mbona maisha pale yanasikitisha.
(verse 2)lshi Tanga lakini kuwa makini,watu wajua mpaka siri zako za ndani, sijui habari hizi huwa waambiwa na nani?
Hospitali ya Bombo ya leo ni vichekesho,ukienda pale hata kama utumbo uko nje, utaambiwa tu matibabu kesho. Tanga, Tanga jamani yarabi toba.Ndege pia kwa mwezi twaona mara moja, basi balaa hili watu tumekuwa twaishi maisha yatumbiri, sijui tusomeane alubadili,ili tumkamate alotu filisi utajiri.Bandari nayo sasa yachungulia shimo, zamani waweza ona miji meli palee wala haina kipimo, lakini! sasa hivi si meli tena, wala hazina uwezo wa kubeba hata kontena. Ukiondoa Wahindi na Waarabu, Waswahili wenye pesa ni wa kuhesabu, halafu wikiendi angalia nyendo zao, kuchukua wake za watu na kutaka mambo nje ya uwezo wao.
Saruji ndo kiwanda arnbachokimebakia, panga pangua makaburu wameingia ubia. watafanyabiashara miaka mitano haifiki nao wale pia watajiondokea
Railway kimyaa, zamani wenyewepale tulishaizoea mijihoni, sasa hivibehewa moja la abiria hatulioni,mwawekani basi mabehewayaloozana pale. Si muondoe jamayaleta mafico wezi yale.
KIITIKIO
(verse 3)Hatijawahi kulalamika sisi hatasiku moja,najuu ya maisha ya Tanga MC natoa hoja, msije mkaona mzaha jamani hivi si vioja, kucheka mtacheka lakini mkoa unadodaViongozi wetu kazi yao hawajui hata moja, vikao vyao n'vingi wanakutana Mkonge Hotei,na agenda za huko hawatiambii ukweli.
Promise zao ni za uongo haziambiiki, sijui wametuona mma'bahau ama m'visiki,Tinapomichagua majukumu yenu mnayatambua? Au mnaona raha dada zetu kuuza vitumbua?
Titabeba zege mpaka lini na kujitutumua? Inaelekea mmetisahau halafu pesa mnazitumbua.Na huu mpango mpango wa Tanga wa vipande vya baiskei,titakuja kutoana roho mchana mchana aisee, tinashikwa na mgambo ili tilipie manispaa, wakati wagosi wa kaya wenyewe ti nakufa na njaa. asalam alekum wallahiNdio maana akili zetu mnasema hazifai, na asubuhi ni mnazi badala ya chai.Pamoja na viwanda na upuuzi huo kufa, elimu tinaichezea halafu kingereza n'cha ugoko. Tisibishane hapoo!Sasa tirudi katika suala ya maendeleo, tinapataje mtaji kwa ajili ya haya maendeeo? Kama si kupakiza magunia kwenye Shengena, tinalipwa hela kidogo haafu tinasengenywa.Chai asubuhi ni kavu hakuna cha kutafuna, watoto wamezoea ubwabwa siku huna hela wananuna,
Wake zetu wamekakamaa utadhani wanafanya diet, haku nacha diet hapo ukapa umepanda chatiNa ukitaka kujua n'balaa kwa haya tinayosema,uwanja wa sabasaba umekufa, hata jumba ya sinema.Msije mkani kumbusha mimi hapa naweza kulia.Oh Tate none wa Tanga tushikamane.Mike Byanaku ni fundi mzuri wa baiskeli, anasaidia sana lazima niseme ukweli. Anapogonga nyundo Wahindi wanasema n'kelele,nntafutieni nyundo yasailensa aondoe hizo kelele.
Na nyie na magari yenu msipige honi wala misele, hapo titaelewana.Tanga tina barabara maarufu na ziko ishirini na moja, na hizi zimejipanga panga na ni hatari kwa vioja, tega sikio usikie ni kitu gani kinakuja.
Tinao akina kaka wanaoshikishwa ukuta, wengine wanajifanya waswalihina wanakula kitimoto, hatiwasemi tinaogopa mkong'oto.Tanga Wahindi wamejazana kwenye maghorofa ya msajii,tunabaki kuhangahanga Kwanjeka sisi waswahii, ukipita chini ya ghorofa wanakutemea mate ya palikiUkiuliza hivi n'kwa nini matusi yake hayaambiiki. Weee Master J!Kuna siku n'tampandia mtu ghorofani nimtoe roho, halafu n'pelekwe kwenye gereza la Maweni n'kanyee ndoo.Timeshachanganyikiwa mnatiletea ubishoo.Juhudi zako zinaonekana sana Kapteni Mkuchika. Afadhali sasa kidogo Tanga tinahema na kucheka.Maneno tinayoongea hapa hatumpigi mtu kamba, Wagosi tinamalizia na salamu kwa Makamba.Baba yetu Makamba, hawa akina matonya hawako tu pekee Daisaama, hata kule Tanga wamejazana ni kiama.
KIITIKIO
PATA NGUO ( PAMBA) ZA UKWELI KUTOKA KINA KLOTHING..!!
Kina ni kampuni mpya ya nguo ambayo inawakilisha Bongo na Afrika kwa ujumla. Kwa utambulisho tumetoka na kollektion inayoitwa Uhuru St. kwa sababu neno uhuru linabeba sababu nzima ya sisi kuanzisha Kina.
Vilevile hii ni lebo ya mavazi ya kitaa na Uhuru ni mtaa wa kwanza katika mfululizo wa kollektion zitakazobeba majina ya mitaa mbalimbali ya Bongo na Afrika kwa ujumla.
Kama kauli mbiu yetu inavyosema “Vitu vyetu. Kivyetu” basi ndio tunavyotarajia kuendesha lebo yetu, yaani full uhuru wa kutengeneza kazi zinazotuwakilisha, kwa namna tunayoamua wenyewe.
Tshirt hizi zimesanifiwa mahsusi kwa ajili ya wabongo na marafiki zao ili kuonyesha kuwa wabongo nao tumo katika medani hii ya design; lakini si hivyo tu, ujumbe unaobebwa na nguo kina ni mchango wetu katika harakati za kujenga madaraja kati ya waafrika barani na diaspora kwa kusambaza na kusheherekea yale yanayotuunga pamoja kama waafrika.
Hata hivyo, katika kollektion hii ya kwanza tumeamua “kucheza kwetu” zaidi, tunatumai utatutunza.
Tutembelee www.kinaklothing.com na tuambie mawazo yako.
Kaa mkao wa kula kwa kollektion inayofuatia, Samora avenue. Iko jikoni.
Amani.
Mkuki na Susan (Kina Klothing)
Friday, July 10, 2009
HII NDIO TANGA CITY- KWA WALE WASIOIJUA VIZURI!!!
Hapa maeneo yaTunakopesha Ltd, kama unaelekea Tanesco!
Eneo hili ni nyuma ya Club maarufu jijini Tanga Lacasa Chica. Lakini ukisogea kwa mbele utakutana na jengo la TTCL na jengo la Benki ya Posta.
Huku ni maeneo kama unaelekea Splendid Hotel, moja kati ya hotel maarufu jijini Tanga.
Hilo jengo la rangi ya pinki, ni jengo la Benki ya Exim. Moja kati ya benki zinazotoa huduma nzuri.
Maeneo ya jengo la TTCL likiwa limepakana na jengo la chuo cha Engusero hapa jijini Tanga.
Jamani eeh, hili ni moja kati ya majengo maarufu Tanga. Lipo maeneo ya Four Ways. Kuna huduma nyingi za kijamii zinatolewa hapo.
Hili ni jengo la Toyota, kama unahitaji magari ya aina hiyo utayapata jijini Tanga pia. Uliposikia Tanga ni jiji, sio masihara mdau!!
Makutano ya barabara ya Tanesco kwa magari yanayofanya mizunguko ya mji kuelekea Raskazoni.
Hili ni jengo la Benki ya Baclays hapa jijini Tanga. Moja kati ya mabenki ambayo yameamua kutoa huduma zake kwa wakazi wa hapa.
Stendi tena, tazama dada na ushungi wake akikatiza mitaaa!!
Kwa wale wapenda starehe, naweza kusema MAMBO IKO HUKU!!! Jengo la klabu Lacasa Chica- Club maarufu jijini Tanga kwa starehe. Wasanii wote wa muziki hufikia hapa kwa ajili ya kukonga nyoyo za wapenda raha- TANGA RAHA!!!
Maeneo ya Four Ways, hili pia ni jengo ambalo kwa hakika linatia fora. Kwa pembeni kama unaelekea barabara hiyo, kuna bonge moja ya Bar maarufu sana kwa nyama choma!!
Tazama bustani zilivyonakshiwa vizuri. Hili jengo linatazamana
na viwanja vya Tangamano ambavyo ni maarufu sana kwa soko huria.
Jamani...hii yote ni Tanga. So enjoy ili na wewe siku moja uje kupaona!
Jengo refu kuliko yote jijini Tanga la Bandari, ambalo kwa hakika ni moja kati ya vivutio. Ukipanda jengo hili utaiona Tanga nzima, na pia kwa upande wa pili utaiona bahari ya Hindi ambayo watu wa Tanga pia tumebarikiwa.
Next time nitawawekea picha za vivutio vya asili ambavyo vipo Tanga kama mapango ya ambaoni n.k.- Hii ni zawadi kwa wadau wangu popote pale mlipo. Karibuni Tanga jamani, tule raha na kufurahia upepo wa pwani!!!