BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, June 30, 2009

ROMA KUTOKA NA MR. PRESIDENT- GET READY MDAU!!!


Msanii kutoka Tanga, Tanzania ambaye ameonekana kuleta mapinduzi makubwa kunako game ya muziki wa bongo flava Rymes Of Magic Attraction a.k.a ROMA- amepiga story na Blog hii kutanabaisha kuwa yupo mbioni kutoka na ngoma nyengine atakayoiita Mr President.
Roma ambaye pia anatamba na wimbo Tanzania, ambao kwa namna moja ama nyengine umekuwa ukifanya vizuri karibu redio zote nchini.
Kama umepata bahati ya kusikiliza wimbo huo utakubaliana na mimi kuwa ROMA- sio mkali tu wa kwenye Ku'Burst hata kwa mashairi pia amekuwa akikimbiza sana.
Mashairi ya wimbo wa Tanzania umekuwa ukigusa hisiza za watu wengi sana, kiasi cha kufanya msanii huyo kupata mialiko tofauti tofauti hapa nchini.
Hata hivyo ROMA hakutaka kutaja ngoma yako hiyo mpya ya Mr. President ataifanyia wapi, ila amewataka mashabiki wake kote nchini kukaa tayari kwa jiwe hilo jengine.
Mwana'Hip Hop huyo ambaye anaamkini kuwa HARAKATI ZA MAPINDUZI NDIO JADI amedai kuwa, ili wasanii waweze kujikwamua kunako game ya muziki wa bongo flava nchini Tanzania basi wawe wabunifu kwani sanaa ni kazi!!
HAYA NI MASHAIRI YA WIMBO TANZANIA YA MSANII ROMA- LAKINI KWA LUGHA YA KIINGEREZA
Verse 1
I1961 kambaragle became a heroYess R.I.P Maria is crying for youIn soul you are with us but in body you are lost alreadyYou resigned when we still needed youYou didn’t wanted to long in powers, you left them to Ali HadjiNow they fight for presidential house with raw lustWords of their campaign is to get income to the citizenTZ is rough everything is zigzagGood people die early, why bad people don’t?Racism and corruption in offices are obviousHe was a vetenary, abrupt he is football secretaryThey bought certificate that they could get degreeAcademic with no future to people who studied scienceBuildings are falling due to engineers forgeryIm hustling, sweat is spilling just for money to buy food Mamy don’t cry daddy weep your tears stop cryingNay real stop cryingI see you much excited like morale of masai
Chorus
This is TanzaniaCountry with a sinful soilThey are looking for diadem of winningSay TanzaniaIm holding bible protesting who fights to be kings or queensThis is TanzaniaThey got endowments of reprobationThey do projects inside our religionsIm saying TanzaniaThe lost state, Tanzanian are crying for your fake promises
Verse 2
If only God could decide that we should attend funerals dailyI belive we could have learnt how to liveEva remember gomor, Adam remember SodomThen together lets pray, that wouldn’t happen as in nuru and safinaCoz in house of prayers they do sinsOpium in streets, that they could get winning diademThey use religion envelops to sell drugsRemoving demons with the power of darknessThey break the sixth commandment in churchsAnd worshiping gods inorder to get moneyInfront of Getrude Rwakatale’s altarOr bishop kakobe they fall infront of altareeeeeeeeeeeThey have given false testimonyReligion has become business, members of the church are corruptedThey wrote false proposal that they could get luckyThey pretend this reprobation as entrepreneurshipSee, police in streets their bosses are drug dealersHigh rank leaders gives out their phone numbers that would get corruptionStill they open places to aid people who have AIDSThey don’t have talents they establish them to get economy profit………………. There ustadh hold your heart Better the blessed one with clean heart,I don’t know what he knows about methewThey prepare robberies, broke in and rob the bankThey met to a bar to divide 10percent among themselvesMoney is too illicit it jeopardized even PetroAfter cock crowed he discovered he forsaken ChristIm recording my track with bible in my left handIm crying for Tanzania tears fill my eyes
Verse 3
I have been hearing about reprobationAnd as they increase is as more I get excitedThey use government fund to start their businessThey own mines and house like sinagogThey were set up that they raped childrenThey are convicted without evidence, Pilato’s like judgementThose who steal millions go unpunishedMy uncle’s son got two years in prison because of bhangi smoking…………….distress cause his deathWho deserved conviction? Him or friend of ……………….I hate entertaining cowards disciplineI cant ignore the sins i witnessI know who talks the truth dies early, I don’t careIf you killed Amina, here I stand strong1st I got permission from home and my grand slaughtered a cow for meI drank its blood and he blessed me that I come to town to stand 4 inferiorsPayment is in the world, now they die one by oneAnd they leave behind their wealth, they didn’t know “dunia mapito”Life is not fair, if was like CollinaDefenders are bullied like sarafina’s teacher Their drivers approach women for their safeKills a lot of innocent bloodsTheir wives go out with youth undisciplinedBecause their husband are busy with illegal dealsThe price of their cars can build a school in villageThere are illiterate children grazing cows in villagesIm standing still like sayuni mountainFor this strike I believe I won over satan .
Kaeni tayari kwa ngoma mpya ya ROMA ambayo itaitwa Mr. President

Friday, June 26, 2009

MICHAEL JACKSON AFARIKI DUNIA- REST IN PEACE!!

Mwanamuziki wa Pop ulimwenguni Miachel Jackson, amefariki dunia usiku wa jana wa tarehe 25/06/2009 huko nchini Marekani mjini Los Angeles baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi.



Bila kujua kwamba amebakiza siku 113 tu za kuishi duniani, Michael Jackson alipokutana na waandishi wa habari mjini London Machi mwaka huu, aliwaahidi mashabiki wake wa Uingereza kuwa onesho lake lililopewa jina la THIS IS IT TOUR lililopangwa kufanyika O2 Arena kuanzia July 09 mwaka huu, lingekuwa onesho kali la kufungia pazia katika historia yake ya maonesho!


Masikini, hilo halikutokea kama alivyotaka, kwani Mungu naye tayari alikuwa na mipango yake isiyobadilika. Inaelezwa kuwa tiketi za onesho lake zilikuwa zikiuzwa kati ya paundi 50 na 75 na zilitararajiwa kumuingizia jumla ya paundi milioni 175!!!! Hii ingekuwa imemaliza kabisa matatizo yake ya kifedha aliyokuwa nayo

katika press hiyo, Michael aliahidi kwa kusema maneno yafuatayo kwa wanahabari wa Uingereza: “I’ll be performing the songs my fans want to hear. This is really it. This is the final curtain call. I’ll see you in July.” (Nitaimba nyimbo wanazopenda mashabiki wangu kuzisikia, huu ni uhakika. Huu ni wito wangu wa mwisho, tutaonana mwezi wa saba)


Michael Jackson amecha watoto watatu - Michael Joseph Jackson, Jr., Paris Michael Katherine Jackson and Prince "Blanket" Michael Jackson II


HAKIKA KIFO HAKINA HURUMA- PUMZIKA KWA AMANI NDUGU YETU MICHAEL JACKSON A.K.A WACKO JACKO





Mashabiki wa Michael Jackson wakiomboleza msiba kwenye mitaa mbalimbali huko nchini Marekani.




Watu wakitazama Video za msanii Michael Jackson mara tu baada ya kupata habari juu ya kifo chake.


Njemba ikiomboleza


Kweli Wacko Jacko alikuwa ni mtu wa watu!

Jamani eeh, Think- How many stopped breathing since the year started..? How many had bad accidents which left disabled?? Tunapaswa kumrudia Mungu.

Kila hatua katika maisha yako ifanye kama funzo, yeyote atokae upeoni mwako kwa njia ya kifo chukulia kama ndugu yako kwani ipo siku yatakufika pia, wahenga wanasema KIFO HAKINA MWENYEWE!!

RAMBIRAMBI KWA WADAU

DJ CHOKA: Ur the best Michael.....1 in a million....truely amazing. RIP. Condolences to your family. And all the mother %$^&% who dont like michael.....die in hell.

3232 Dar:i grew up listening to ur songs michael....cant believe ur gone....peace be on ur soul.... ur the King ...ur the King...!!

LETH: Rest in peace. Just saw his wife's profile on milllionaire personals site """"" W e a l t h y D a t e r . c o m """""" last week. I am wondering what kind of relationship she is looking for on that site.

LUCY NGOWI:condolence to the family of Michael Jackson,we are saddened for the untimely death of a great artist,may you rest in peace mike,we will never forget you,we will surely miss yo

CUTE:weve lost the best singer and dancer and i think no one can be as good as him.HES THE BEST. safia Dubai UAE

HASNA: sikutegemea kama mwisho ungekuwa kama mshumaa unaozimika kwenye upepo, RIP Wacko!

IDDA ELIAS:AFTER DEATH IS JUDGEMENT.LET US ALL LEARN FROM THIS MAN.I WILL NOT LIKE TO JUDGE HIM BUT MY HEART GOES OUT TO HIS FAMILY


ANKO MO: Michael you are great hero and we love you but God love you most, may your soul rest in perfect peace.

Sunday, June 21, 2009

BENNIE MAN KUPIGA SHOW TANZANIA- ARE YOU READY.!!!

Msanii Bennie Man kutoka nchini Jamaica, anatarajiwa kutua nchini Tanzania kunako jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kupiga show moja ya ukweli. Kwa mujibu wa Str8 Music Entertainment moja ya wadhamini wa show hiyo, Binnie Man atasindiizwa na T.I.D, Makaumua na Q Jay, Hussein Machozi, TMK Wanaume Familiy, CP, Mangwear pamoja na wa vipaji kutoka Tanzania House of Talent (THT). Wazeeeeya kaeni mkao wa kula pande za DSM!!


JAMANI! TUNAELEKEA MISS TANZANIA.

Nawakumbusha tu wadau wangu hususani wakazi wa Tanga kuwa tunaelekea Miss Tanzania, Je dada yetu Glory Chuwa atapenya hapa..? Tumuombeeni heri na baraka.

Saturday, June 13, 2009

MWAMBAO FM ILIVYOVUMBUA VIPAJI VYA UWIMBAJI!!


Dj Shago 66 na Dj Bob Nas wa Mwambao Fm wakiweka mambo sawa kuhakikisha muziki unatoka vizuri ili kuwapa shangwe mashabiki pamoja na wasanii.


Msanii kutoka kundi la Street Coulor akiwakilisha vya kutosha kwenye stage. Fainali hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa La Club Tanzanite.

Star B akiwa kama ni solo artist, akijituma ipasavyo kuhakikisha anaibuka bingwa!


Masotojo kutoka Tanga alipiga show katika harakati za kuchuja wasanii watakaoingia mkataba na Mwambao Fm kupitia Mwambao Record.


Mshiriki anayejulikana kwa jina la The Drama, akionyesha kipaji chake jukwaani.

Wazee wa Shino Style- Shomy Luv pamoja na Big Smart wakitoa burudani kali kwenye ukumbi wa La Club Tanzanite siku hiyo ambapo wasanii wanne waliweza kuingia mkataba na Mwambao Record.


Baadhi wa Presenters wa Mwambao Fm, Mamaa Nusura Abdalah wa kwanza- Dj Rach Kuty aliyevaa fulana ya kijani pamoja na Benedict Kaguo a.k.a Father K wakifuatailia kwa makini fainali hiyo.


Usipiime!! Kulijaa watu sio mchezo. Hakuna aliyetaka kupitwa- wadau wote wa muziki wa bongo flava waklikutana hapa.



Majaji walikuwa na kazi nzito!! Wa kwanza ni Jaji Anko Mo kutoka Mwambao Fm na aliyevaa kofia ni Dr Leader ambaye pia ni msanii- pamoja na Sam Chad Producer kutoka King Falcon.


Dr Leader na Sam Chad wakiteta jambo.

Leader akaona haitoshi- akamgeukia Anko Mo kwa kuteta mengine zaidi.


Dj Bob Nas akijaribu kumueleza jambo mshereheshaji wa fainali hiyo Ahmed Khatibu (wawoo)- Shindano hilo la kutafuta vipaji lilidhaminiwa na redio Mwambao Fm kwa lengo la kuwapa vijana ajira kupitia tasnia ya muziki. Washindi walikuwa ni Razy Flava, Chabo, Star B pamoja na The Drama.


Tuesday, June 9, 2009

GLORY CHUWA AIBUKA MSHINDI MISS TANGA 2009


MREMBO Glory Chuwa(20) ameibuka kuwaMiss Tanga Vodacom 2009 baada ya kuchaguliwa na jopo la majaji kuwamshindi katika mchuano mkali uliofanyika usiku wa jumamosi kwenyeuwanja wa Mkwakwani Jijini hapa.


Glory ambaye ametokea kitongojicha Miss College, alifanikiwa kupita katika chekeche la mchujouliowashirikisha warembo 20 waliokuwa wameshinda kwenye vitongoji vyaWilaya za Mkoa wa Tanga na kuingia kambi ya Miss Tanga kwa kipindi chawiki tatu.


Baada ya Mkurugenzi wa Five Brothers Enterteinment,Nassa Makau, kumtaja Glory kuwa ndiye mshindi,mrembo huyo alivikwarasmi taji na Miss Tanga 2008,Nadia Ahmed na amezawadiwa sh. 1 milioni.

Jopo hilo la majaji likongozwa na aliyewahi kuwa Mr College nchini MatukioChuma,lilimchagua Yasmin Zachari kuwa mshindi na miss Tanga namba tatuni Rachel Mlaki,wakati aliyeshika namba nne Alice Marcus na kufuiatiwana Neema Mbuya.

Shindano hilo liliandaliwa na Five Brothers Entertainment ikishirikiana na wadau wengine- Natumai dada yetu Glory Chuwa utatuwakilisha vyema mkoa wetu wa Tanga huko uwendapo. Ila nakuomba sana kwepa skendo!!


Sunday, June 7, 2009

FACTORS KUIWAKILISHA TANGA KWENYE MALTA GUINNES STREET DANCE AFRICA 2009!

Vijana wanaounda kundi la Factors, wameweza kuibuka kidedea kwenye mashindano ya Malta Guinnes Street Dance Africa 2009 kwa mkoa wa Tanga. Wakiwa kwenye pozi.



Wakiwa na nyuzo za furaha baada ya kulamba mshiko wa laki sita taslimu toka malta



Factors ambao ni wawakilishi wa Tanga, wakiwa na B12, B dozen wa Clouds Fm punde tu baada ya kutangazwa washindi.



Washkaji nao waliibuka kuwa washindi wa pili- wanaitwa Familia Bora. Walitoka na zawadi ya shilingi Laki tatu. I wish u colud be there madau wangu.


Wakiwa wanyoooonge- HB Group waliibuka washindi watatu huku wakilamba shilingi laki moja.




Yoote tisa- msanii Matonya alipiga show!!


Mtoto wa kitanga, akiwapa raha watanga wenzake.


Home ni Home tu wadau- mzazi alipiga show kwa hisia zote kuhakikisha anawapa burudani watu wake.

Kuuzaska ubingwa wa Malta ilikuwa si kazi ndogo- kundi la Factors likishambulia jukwaa


HB group wakionyesha Styles za ukweli- PLZ DONT TRY THIS AT HOME!!!!! hahahah




Ubunifu na ujanja- vilitawala kwenye stage!~




Waha walitoa fora na staili yao ya kubeba maiti- Mmh hata hivyo waliboa watu kimtindo!!

B12 akisherehesha mashindano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Tanga Hotel maeneo ya Chumbageni.

Panel of Judges, wa kwanza kutoka kulia ambaye ni Chief judge Aloyce Makonde kutokea Cheregrapher Dancer akifuatiwa na Rose kapingu kutokea Cheregrapher Dancer pia mwisho ni Mr Angelo Luhala ni kamisaa Barata la Sanaa Tanzania (BASATA). Walikuwa na kazi nzito!!



Abdul wa Maisha Plus alikuwepo, mwenyeji wake alikuwa Julieth Kulangwa kotokea Mwananchi na pia alikuwa Media Coordinator wa Maisha Plus.

Nje ya ukumbi wa Tanga Hotel- Anko Mo, Abdul pamoja na mdau mwengine wa habari william Mjema.



Zee la nyeti Henri Mdimu akiwa na Anko Mo- it was so good wadau wakikutana sehemu za raha kama hizi.


Jamani eeeh, Malta Guinnes Street Dance Africa 2009 kwa mkoa wa Tanga diyo hiyo imeishia- safari sasa inaelekea Zanzibar. Tunawashukuru Malta kwa ujio wenu, karibuni tena mwakani. nina imani kundi la Factors mtatuwakilisha vyema mkoa wetu wa Tanga- endelea kutembelea blog ya kijanja zaidi nchini Tanzania, Tanga.

Wednesday, June 3, 2009

NANI MKALI KATI YA BESTA, KYLNN NA RAY C..?

Anaitwa Besta- mwanadada ambaye anafanya vizuri sana kwenye ramani ya muziki Afrika Mashariki. Kama wewe ni shabiki wake, mpigie kura ashinde!!




Huyu anaitwa Rehema Chalamila a.k.a Ray C, aliwahi kutamba na wimbo wake wa MILELE- na staili yake ya kiuno bila mfupa. Kama ni shabiki wake, mpe kura yako.


Aliwahi pia kua miss Tanzania, Jackline Ntuyabaliwe au Kylln. Ukitaka kujua dada huyu ni mkali, sikiliza wimbo wake wa NIPE MKONO. Mpigie kura kama wewe ni shabiki wake.

Kumbuka! Mshindi kati ya dada hawa watatu, utaweza kuona video yake live kupitia blog hii. Mpigie kura mmoja wapo ili apate kushinda. Kura zote zitumwe kupitia E-mail ambayo ni

ankomo25@yahoo.com

Tuesday, June 2, 2009

TAMASHA LA FILAMU TANZANIA 2009 LAZINDULIWA TANGA


Mstahiki meya wa jiji la Tanga Salim Kisauji akiteta jambo na baadhi ya wadau wengine wa filamu mkoani hapa. Pembeni ni Aisha Kisoki au mama Sofia Production, ambao ndio wandaaji wakuu wa tamasha hilo la filamu Tanzania lililozinduliwa siku ya jana ya terehe 1/6/2009 kwenye viwanja vya Tangamano. Kisauji alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo

Kikundi cha Tumaini Arts kikitoa burudani ya ngoma aina ya Baikoko- moja ya midundo ambayo inapendwa sana na wakazi ya Tanga. Hapo dada Mwajuma akicheza ile staili ya "VIBRATION"




Kikundi chengine cha Channel O kutoka hapa hapa jijini Tanga, kikipagawisha na Baikoko ya nguvu.

Wakazi wa Tanga wakipata burudani ya kipekee siku ya jana wakati tamasha hilo lilipofunguliwa rasmi.

Hapa mwanzo mwisho- mashabiki na wadau wa filamu jijini Tanga wakifuatilia Tamasha.

Baadhi ya mitaa ya jijini Tanga

Walimbwende wa Miss tanga 2009 pia walipewa mwaliko


Miss tanga 2008, Nadya Ahmed aliwakilisha vya kutosha kwenye tamasha la filamu


Mkurugenzi wa Sofia Production, Musa Kisoki ambaye kampuni yake ndio imedhamini tamasha la filamu Tanzania kwa mwaka huu- akifungua ramsi tamasha hilo.


Kudadeki!! Wakurugenzi wamekutana- mkurugenzi wa Five Brothers Entertainment Nasa Makao akiteta jambo na mkurugenzi wa Sofia Production Musa Kisoki

Crew ya Sofia Production ikiwa makini kwenye mitambo. Tamasha hilo la filamu mkoani Tanga limezinduliwa siku ya jana, na kilele chake ni siku ya Jumanne ya tarehe 9/6/2009 wiki ijayo.