BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, July 26, 2010

'NO FEATURING KWA SASA'- Q CHILLAH!

Msanii kutokea mkoani Tanga Aboubakar Shaban Katwila a.k.a Q Chillah ambaye anafanya vizuri kunako anga za muziki wa bongo flava hapa nchini, amsema kuwa hivi sasa hataki tena kusikia habari za kushirikishwa (Featuring) katika ngoma za wasanii wengine. Chillah aliongeza kwamba ameamua kufiikia uwamuzi huo kwa sababu yupo tait na ujio wake mpya baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.
"Hivi sasa nipo kwenye mishemishe za kwenda levo nyengine, sihitaji kushirikishwa na msanii yeyote yule kwani nimeshawasaidia sana, kilichopo mble yangu muda huu ni kuangalia jinsi ya kuupeleka muziki wangu mbali" alisema Chillah.

Akiwa ametoka chimbo n ngoma yake ya 'Saba Mara Sabini' ambayo inafanya vizuri kila kukicha kunako redio tofauti tofauti nchini....msanii huyo pia hakusita kutaja jina la albamu yake mpya ambayo ni "A SING OF MATURENESS" kwa kuwa albamu hiyo imeshakamilika na kinachofuata ni video za ngoma kadhaa kabla ya kuwapelekea mahabiki wake.

Sunday, July 25, 2010

HILDA MTENZI AFARIKI DUNIA!

Aliyekuwa mtangazaji wa TBC mkoani Tanga Hilda Mtenzi amefariki dunia jana akiwa anasumbuliwa na kichwa ama hakika dada yetu ameacha pengo kubwa katika shirika la utangazaji nchini .

Marehemu anatarajiwa kuagwa leo mchana katika hospitali ya Taifa Muhimbili. Anko Mo Blogspot inatoa pole kwa ndugu na marafiki wote wa marehemu.

FIESTA JIPANGUSE 2010 PANDE ZA TANGA....YA UKWELI!!!!

Mkali wa Hip Hop kutokea Tanga R.O.M.A akikamua vilivyo usiku wa kuamkia jana kunako show ya Fiesta jipanguse iliyofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani hapa jijini Tanga. Fiesta huja kila mwaka na huandaliwa na kituo cha redio cha Clouds Fm.

Nyomi la watu likishuhudia show ya Fiesta. Ilikuwa shangwe za kutosha kwa wakazi wa Tanga.

Fid Q akimtemea mashairi binti mrembo....

Brother Juma Nature alikuwepo...alipiga bonge la show.

Mkali wa microphone akiwa kwa redio ama stejini...B12 akiongoza show ya Fiesta.

Kaaaaaaaaazi kweli kweli...wazee wa bata wakifanya makamuzi.

Kutoka TMK Wanaume Family.....Chege na temba waliwakilissha ipasavyo.

Joh Makini akipiga show.....

Wana wa Tip Top Connection wakishambulia jukwaaa. Karibuni tena mwakani wana wa Clouds Fm....mmefanikisha Fiesta Jipanguse rrrraaaaaaaaaaaaaaa!! 2010 kwa pande za Tanga.



Wednesday, July 21, 2010

BREAKING NEWS!!!!!! WAGOSI WA KAYA WATEMANA!!

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya hapa nchini kutoka katika kundi la Wagosi wa Kaya lenye makazi yake jijini hapa John Simba "Dr.John"amesema kuwa kundi hilo limekufa kutokana na msanii mwenzie Fredy Maliki "Mkoloni"Kujiingiza katika masuala ya Kisiasa hapa nchini kwa kujiunga katika chama cha chadema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,Dr.John alisema kuwa kwa sasa kila kitu ambacho kitakuwa kinafanyika katika kundi hilo ikiwa ni pamoja na kutoa nyimbo na kuimba itakuwa ni kama maagizo ya Chama cha Chadema.

Dr.John alisema kuwa kwa sasa hivi anaangalia mambo mengine ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwainua wasanii chipukizi katika mkoa wa Tanga ikiwemo mwanae mwenyewe Josephine "Phine".

Aidha alisema kuwa mikakati yake kwa sasa ni kufanya kazi peke yake kama solo artist kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali kutoka hapa nchini. "Ule urafiki uliokuwepo kati ya mkoloni na mimi upo pale pale lakini sio kwenye kazi "alisema Dr.John.

Aidha alitoa wito kwa wasanii chipukizi wa mziki wa kizazi kuangalia muziki na mambo mengine na sio wang"ang"anie kwenye muziku kueleza kuwa kwa sasa wanatakiwa kuandika mashairi ambayo yana ujumbe kwenye jamii na sio mapenzi.

Sunday, July 18, 2010

ROMA ANG'AA TENA FIESTA DODOMA!!!

Msanii kutokea Tanga ambaye ni mkali wa Hip Hop ROMA anazidi kuwakimbiza 'wachimba chumvi' kwenye show za fiesta zinazoandaliwa na Clouds Fm....safari hii funiko zaidi ya bovu pande za dodoma!!

Saturday, July 17, 2010

TUBURUDIKE KIDOGO LEO WADAU!!! ANAITWA VANESSA CARLTON

BAADA YA 'FIMBO YA BABA' UZIKWASA KUJA NA FILAMU NYENGINE!

Film Coordinator wa shirika la UZIKWASA Bi Rehema Kilapilo akiwa makini wakati wa mazoezi ya filamu mpya inayotengenezwa na shirika hilo lisilo la kiserikali. Mazoezi hayo hufanyika Pengadeco kila siku ili kuwaweka wasanii kabla hawajaanza kurekodi. Kabla ya kuja na filamu hii UZIKWASA (Uzima Kwa Sanaa) yenye maskani yake wilayani Pangani mkoani Tanga, ilishawahi kuandaa filamu nyengine hapo awali iliyoitwa FIMBO YA BABA na kufanikiwa kupata tuzo.

Msanii maarufu nchini Vitalis Maembe ni mmoja wa washiriki wa filamu hiyo mpya. Hapa akiwa kwenye mazoezi na mwanadada.

Dokta Hatar ambaye ni mmoja wa waongoza filamu hiyo, akiwa katika hatuo za mwisho za kuwasimamia wasanii ambao wamepata nafasi katika filamu.

Wasanii mazoezini.

Wasanii wakipiga tizi huku Dokta Hatar akiwasimamia.

Vitalis Maembe

Rehema, Bura, Chande wa TVZ na dada mwengine wakijadiliana jambo wakati wasanii wengine wakiendelea na mazoezi.

Wasanii wakiwa wametulia kwenye viti vyao wakiwatazama wenzao wanavyofanya zoezi.

Baadhi ya washiriki wa filamu hiyo mpya.

Wasanii wakipewa maelezo.

Friday, July 16, 2010

TANGA YETU YA LEO!!!!!

Chuo cha kiislam cha Zahrau cha jijini Tanga, kipo eneo la madina njia ya kwenda Sahare.

Eneo la soko la Ngamiani.

Soko la Ngamiani...wananchi wa Tanga wakiwa kwenye mahitaji yao ya kila siku.

Karibu na stendi kuu ya mabasi.....sehemu ya kuingia.

Taifa Road.......moja kati ya njia kuu inayopitiwa na barabara za namba zote.

Reli za Tanga zinavyoonekana sasa.

Bodaboda wa baiskeli Tanga kibao......hapa ni kituo cha reli.

Makutano ya barabara kutokea Chumbageni polisi...

Hapa ni eneo maarufu sana...linajulikana kama Tawakal! Tende Shake utazipata hapa

TOVUTI YA MKOA WA TANGA HADI LINI...!????

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa umekuwa katika michango mbalimbali ya kukuza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) katika ngazi ya mkoa na halmashauri za wilaya kwa lengo la kujenga serikali mtandao (e-government). Kuimarika kwa matumizi haya ya (TEKNOHAMA) kutasaidia sana kurahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika shughuli mbalimbali za kila siku kati ya serikali (mkoa), halmashauri za wilaya na wadau wengine.

Moja ya vitu ilivyoshughulikia ni uanzishwaji wa Tovuti za Mikoa kwa Mikoa yote ya Tanzania bara. Ambapo tovuti hizi zimezinduliwa rasmi na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda tarehe 19 Februari 2009 halfla hiyo imefanyika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro

Wasi wasi wangu ni kwamba hadi sasa mkoa wa Tanga hauna tovuti tangu waziri mkuu Mizengo Pinda atangaze nia yake hiyo Februari 2009. Pichani mkoa wa Morogoro ukiwa tayari umepatiwa tovuti yake....humo kuna kila kitu kinachohusu mkoa huo. Sisi Tanga hadi lini..>>????

Pichani tovuti ya mkoa wa Kagera, tovuti ya mkoa wa Tabora na tovuti ya mkoa wa Dar es salaam. Tunaomba mkuu wa mkoa wa Tanga Saidi Kalembo ulitazame hili. Mkoa wako hadi sasa haujapata tovuti.

Thursday, July 15, 2010

'TANZANIA' -YA MKALI ROMA

MUHEZA HIYO MZEEEEEEEEEEEEEE!!!

Restaurant maarufu wilayani Muheza WHITE HOUSE! Ipo barabarani kabisa.

Kituo cha kuweka mafuta.....ipo kona ya kuingia stendi kuu ya mabasi.

Mgahawa....

Kuelekea Amani....

Mchuuzi wa machungwa....twende kazi!!

Boda boda za pikipiki kila kona ya muheza na Tanga nzima.

Hapa ni kona ya kuingia stendi kuu kama ukitokea Segera.

Mitaa ya Muheza..

Wednesday, July 14, 2010

'BINADAMU' UNTOUCHABLE FT KASSIM- MKALI MWENGINE WA HIP HOP KUTOKA TANGA

'FIGHTER'- NGOMA MPYA YA ZAYUMBA

Jana nilitumiwa wimbo mpya na mshkaji kutokea hapa Tanga- Malick Zayumba! Sikiliza ngoma yake hapo pembeni kulia palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Ngoma inaitwa 'Fighter' imetengenezwa pale Bard Number record chini ya producer Riz Mocko. Tayari Zayumba anatamba na ngoma yake nyengine inayoitwa 'Najiamini' ambayo amemshirikisha Kaju kaju.......kichwa chengine cha Hip Hop kutokea Tanga City hicho.

Tuesday, July 13, 2010

BENEDICT KAGUO, OSCAR ASSENGA WAPEWA TUZO.

MWANDISHI wa gazeti la Majira Mtangazaji wa Radio Mwambao Fm ya jijini Tanga, Benedict Kaguo 'Father K' kulia akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Entertainment Nassor Makau ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kufanikisha Mashindano ya Miss Tanga yaliyoandaliwa na Kampuni hiyo.

Hafla hiyo fupi iliyofanyika juzi kwenye makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Ring street hapa jijini Tanga. Shindano la kumsaka mnyange wa Miss Tanga yalifikia tamati kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort ambapo Anna Kiwambo aliibuka kidedea.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Bingwa na mtangazaji wa Mwambao Fm Radio Oscar Assenga akikabidhiwa cheti cha ushiriki na kufanikisha mashindano ya Miss Tanga 2010 kutoka kwa Mkurugenzi wa Five Brothers Entertainment Nassor Makao ofisini kwake kwenye hafla hiyo ilifanyika na kuhudhiriwa na watu wachache

Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Entertainment Nassor Makau akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwaandaaji wa Miss Usagara 2010 Asia Msangi katika makao makuu ya Kampuni hiyo Mtaa wa Ring jijini Tanga.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Entertainment Nassor Makau katikati akijadiliana jambo na waandishi mahiri wa sanaa ya urembo Benedict Kaguo kushoto na Oscar Assenga Mwandishi wa New Habari Co-operation wachapishaji wa gazeti la Bingwa nje ya ofisi ya kampuni hiyo mtaa wa Ring jijini Tanga.