BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, December 23, 2011

TAKUKURU FUATILIENI FEDHA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI HALMASHAURI-GALLAWA


MKUU wa mkoa wa Tanga, luteni (mstaafu) Chiku Gallawa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi ya kufuatilia fedha zinazopelekwa na serikali katika halmashauri nchini ili ziweze kutumika vizuri kwenye miradi mikubwa ysa maendeleo iliyokusudiwa.

Akifunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa takukuru kwenye hoteli ya Tanga beach Resort kwa maofisa wa taaisis hiyo kutoka mikoa yote ya tanzania bara, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa takukuru wamebeba dhamana kubwa ya kustawisha maendeleo kwa kufautilia watendaji kwenye halmasauri ambao wanatumia vibaya fedha zinazoolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo.

Amesema serikali hasa ya awamu ya nne, imekuwa ikitoa fedha nyingi katika halmashauri kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maeneleo hasa ya elimu, afya, barabara na kujenga majengo mbalimbali lakini fedha hizo wakati mwingine zimekuwa zikitumika visivyo na hivyo kuleta malalamiko kutoka kwa wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa pamoja na kuipongeza taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuokoa fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni 97.5, lakini ameitaka takukuru kuhakikisha inaongeza kasi ya mapambano ya rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.

Kuhusu wananchi mkuu huyo wa mkoa amewataka kutoa ushirikiano kwa taaisis hiyo na waache kulalamikia masuala ya ufisadi wakati kama watatoa ushirikiano masula hayo yanaweza kudhibitiwa kwa watu kuogopa fedha za umma hatua ambayo mwelekeo wa taasisi hiyo inakoelekea na kwamba waongeze jitihada kutumia nyenzo walizokuwa nazo katika mapambano hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala la mapambano ya rushwa ikiwemo kuwafundisha watumishi wake kwenda sambamba na mabadiliko ya teklonojia katika masuala ya rushwa.


Sunday, November 20, 2011

MKUU WA MKOA WA TANGA ATEMBELEA MGODI WA KUZALISHA UMEME WA HALE, AKUTANA NA CHANGAMOTO

MKUU WA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA NEW PANGANI FALLS POWER STATION INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA AKIMSOMEA TAARIFA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GALLAWA ALIPOTEMBELEA KAIKA MGODI WA KUZALISHA UMEME ULIOPO HALE WILAYANI KOROGWE.

INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA (ALIYENYOOSHA MKONO JUU) AKIMWELEZA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI CHIKU GALLAWA (KUSHOTO) NAMNA UZALISHAJI UNAVYOFANYIKA KWENYE MGODI HUO WA KUZALISHA UMEME HALE.

INJINIA MUSIMU MAKUNGA MSIMAMIZI WA MGODI WA KUZALISHA UMEME WA PANGANI FALLS AKITOA MAELEKEZO WA JINSI WANAVYOWEZA KUENDESHA MITAMBO HIYO YA KUZALISHA UMEME KATIKA MAJUKUMU YAO YA KILA SIKU.

HAPA MKUU WA MKOA LUTENI CHIKU GALLAWA AKIWA NA MSAFARA WAKE WAKIANGALIA KINA CHA MAJI KATIKA BWAWA LILILOZUIWA KWA AJILI YA KUPELEKA MAJI KATIKA MGODI HUO


KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA BARABARA YA TANGA/HOROHORO, BANDARI YA TANGA

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDOMBINU INJINIA OMARI CHAMBO, AKITOA UFAFANUZI KWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WALIOKUWA KWENYE MKUTANO KWENYE JENGO LA BANDARI HOUSE TANGA

WATENDAJI WA BANDARI YA TANGA WAKIFUATILIA KWA MAKINI MICHANGO YA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDOMBINU INJINIA OMARI CHAMBO (KATIKATI) AKIELEZEA JAMBO KWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WALIOTEMBELEA BANDARI YA TANGA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI

MJUMBE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU BW. HERBERT MNTANGI AMBAYE NI MBUNGE WA MUHEZA (BONDE) AKIWAELEKEZA WAJUMBE WENZAKE JINSI KISIWA KILICHOPO JIRANI NA BANDARI YA TANGA KINAVYOWEZA KUZIDISHA KUJAA KWA MCHANGA KATIKA BANDARI YA TANGA

Wednesday, October 26, 2011

WHITE BEACH PARTY NDANI YA RASKAZONE TANGA!!!!


Sio ya kukosa

SEKONDARI YA SHEMSANGA YAUNGUA TENA MOTO, SAFARI HII CHANZO CHAKE NI HITILAFU YA UMEME

Shule Ya Shemsanga Inayomilikiwa Na Jumuiya Ya Wazazi Wa Ccm Iliyopo Wilayani Korogwe Imeungua Moto Na Kusababisha Hasara Inayokadiriwa Kufikia Kiasi Cha Shilingi Milioni 10

Mkuu Wa Shule Ya Shemsangaga Bw. Paschal Deogradius Akiangalia Huku Haamini Moja Ya Chumba Ambacho Kilikuwa Ni Bweni La Kulala La Wanafunzi Hao.

Moja Ya Bweni Ambalo Limeteketea Kabisa Katika Shule Hiyo.


Thursday, October 13, 2011

JULIO NA MAZOEZI KABAMBE YA COASTAL UNION, LENGO NI KUINASUA MKIANI

Kocha Jamhuri Kihwelo 'Jullio' Akiweka Koni Ikiwa Ni Siku Yake Ya Kwanza Kuinoa Timu Yake Mpya Ya Coastal Union Kwenye Uwanja Wa Gymkhana Ambako Timu Hiyo Inachukua Mazoezi.

Wachezaji Wa Timu Ya Coastal Union Wakiw Ana Kocha Wao Jamhuri Kihwelo 'Julio' Wakifanya Mazoezi Kwenye Uwanja Wa Gymkhana Jijini Tanga Ambako Timu Hiyo Inafanya Mazoezi.


WAFUKIWA NA KIFUSI WAKITAFUTA RUPIA WALIKUWA WAKICHIMBA CHOO NDANI, MMOJA AFA PAPO HAPO

Mama Zaina Ramadhani Ambaye Nyumba Yake Kwa Nyuma Aliwaita Watu Watatu Wamchimbie Choo Kwa Ndani (Nyumba Ya Makuti Inayoonekana Nyuma Ya Picha) Watu Hao Walipoanza Kuchimba Wakaeleza Kwamba Wameona Dalili Ya Kuwepo Kwa Rupia Za Kijerumani Hivyo Wakaendelea Kuchimba

Hadi Shimo Likafika Kwenye Nyumba Hii Ya Bati, Ambako Mtu Mmoja Anayeitwa Saleh Wazir Alifukiwa Na Kifusi Humo Ndani Na Kufa Wakati Mmoja Anayeitwa Simon Alifunikwa Lakini Bahati Yake Miguu Yake Ilifunikwa Akawahi Kutolewa Huku Mwenzao Mmja Anayeitwa Otborn Aliwahi Kukimbia Na Kuwaacha Wenzake.

Nyumba Ambayo Shimo Limetokeza Kwa Ndani Na Kuua Mtu Mmoja Huko Mnyuzi

KOROGWE WAZINDUA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA

Kaimu Mkuu Wa Wilaya Ya Korogwe Methew Nasei Akisaliana Na Wananchi Mara Alipowasili Kwenye Viwanja Vya Magoma Shuleni Kulikofanyika Maadhimisho Ya Uzinduzi Wa Sherehe Za Miaka 50 Ya Uhuru Wa Tanganyika Ambapo Kiwilaya Zilifanyika Magoma Na Kuhudhuriwa Na Watu Wengi

Amanda Wa Jwtz Akiwa Na Kikosi Chake Cha Mgambo Ambacho Kimeanza Mafunzo Katika Kijiji Hicho Cha Magoma Mara Nyini Wana-Mgambo Ni Jeshi La Akiba Ambapo Katika Sherehe Hizo Za Uzinduzi Walinogesha Sherehe Hizo Kwa Gwaride Lao Zuri.

Katibu Tawala Wa Wilaya Ya Korogwe (Kushoto) Akiwa Na Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Korogwe Mr. Masembejo Wakiangalia Ratiba Ya Sherehe Za Uzinduzi Wa Sherehe Za Miaka 50 Ya Uhuru Magoma.

Saturday, September 24, 2011

HONGERENI CATHBERT KAJUNA NA DADA ESTER ULAYA KWA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA

Cathbert Kajuna na dada Ester Ulaya hatimaye wamefunga pingu za maisha. Maharusi wote ni marafiki wa karibu wa Anko Mo Blogspot. Mungu awape neema na baraka katika maisha yenu ya ndoa.



Hapa wakionyesha vyeti vyao vya ndoa.

Kajuna najua hapa presha ilikuwa inapanda na kushuka. Hongera sana kaka.



Monday, September 19, 2011

SHILLINGI VIT CLASS USAFIRI PANGANI- TANGA MPAKA DAR

SHILLINGI VIP CLASS ni mabasi mapya kabisa ambayo yanafanya safari zake PANGANI-TANGA mpaka DAR kila siku kuanzia saa moja kamili asubuhi. Halafu DAR- TANGA mpaka PANGANI.



Unafika mpaka Pangani na kuina fukwe nzuri za kuvutia.


Wednesday, September 7, 2011

KISIMA CHA MAJI CHAZINDULIWA LUSHOTO

Na Oscar Assenga,Lushoto.
MRADI wa Kisima cha maji katika kituo cha Afya Kangangai uliofadhiliwa na kikundi cha urafiki wa ujerumani na Tanzania (Deustsch Tanzanischer freundeskreis DTF)umezinduliwa juzi wilayani Lushoto.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Daktari Mfawidhi wa kituo hicho,Bakari Mavura alisema mradi huo ulianza mwaka 2008 kutokana na kuwepo kwa tatizo la maji katika kata ya Mwangoi tarafa ya Mlalo ambapo waliamua kukaa chini na kuanza kubuni mradi huo wakishirikiana na kamati ya afya ya kituo hicho.Mavura alisema baada ya kubuni mradi huo waliweza kuishirikisha jamii na kuweza kupata marafiki wa kikundi cha wajerumani na walipotoa mawazo na uweza kuyafanyia kazi.


Katika mradi huo shilingi milioni 16.2 zimetumika kati ya hizo shilingi milioni kumi laki mbili zimepatikana kutoka kwa kikundi cha urafiki na halmashauri ya wilaya ya Lushoto imechangia shilingi milioni sita.


Mavura alielaza maji hayo yatakuwa ni kwajili ya kituo hicho pamoja na watumishi wanaofanya kazi ambapo zaidi ya watumishi 10 pamoja na wananchi 22,000 watanufaika mradi huo pamoja na wagonjwa ambao watakwenda kupata matibabu kwenye kituo hicho cha afya cha Kangagai. "Wananchi wanapaswa kukitunza vizuri kisima hicho ili kuweza kuondokana na tatizo la maji "alisema Mavura.


Aidha aliongeza kuwa wanatarajiwa kuishirikisha jamii katika utunzji wa kisima ili kiweze kuwa endelevu.Alieleza kuwa licha ya kukamilika kwa kisima hicho wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa shillingi Millioni moja na laki nane kwa ajili ya kumalizia ufungaji wa mfumo wa maji safi na maji taka kwenye majengo ya kituo chicho.Mwisho.

ZUBEDA SEIF MKALI WA KUIGIZA VODACOM MISS TANZANIA

Mrembo Zubeda Seif kutoka Tanga aliyejinyakulia kitita cha Dola 1000 akimnanga muingizaji nguli Jacquline Wolpa wakati wa kutafuta mrembo wa Vodacom Miss Tanzania aliye na kipaji cha uigizaji lililozaminiwa na Kampuni ya Papazi.

Monday, September 5, 2011

HOTELI MPYA YAZINDULIWA TANGA

MMILIKI wa hoteli mpya inayojulikana kwa jina la NYUMBANI Hotel & Restaurant Bw. Aloyce Kimaro aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, amewataka wafanyabiashara na wananchi wa Jiji la Tanga, kumuunga mkono katika uwekezaji wake mpya wa sekta ya hoteli ili kusaidia kuongezeka kwa pato la uchumi la mkoa wa Tanga.

Akitoa neno la shukurani kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopo mkabala ya jengo la posta katikati ya Jiji la Tanga, mbunge huyo wa zamani alisema alipata wazo la kufungua hoeli hiyo mkoani Tanga, kushirikiana na wana-jamii kuongeza pato la mkoa hasa kutokanana uwepo wa bandari na shughuli nyingine za kiuchumi.

Alisema kutokana na uwepo wa bandari na kukua kwa shughuli nyingi za kibiashara alionelea kufungua hoteli hiyo hivyo amewataka wananchi na wafanyabiashara kushirikiana naye kumsapoti katika kuhakikisha hoteli hiyo inatoa huduma za kisasa na za kimaaifa.

Bw. Kimaro ambaye anaendesha hoteli hiyo akiwa na wakurugenzi wengine Bw. John Kessy na Mansfeld, wanatarajia kufungua hoteli zenye jina hilo katika mikoa yote nchini ili kuhakikisha wanawekeza katika sekta hiyo wakiwa kama Watazania na kusaidia kukua kwa uchumi wa Tanzania. Hoteli hiyo ya Tanga inafuatia kuwepo kwa hoteli nyingne zenye jina hilo la nyumbani katika miji ya Mwanza na Moshi.

Akizindua hoteli hiyo Waziri wa Uchukuzi, Injinia Omar Nundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Tanga, alisema katika kutembea kwake Ulaya hoteli hiyo inaingana kabisa na ambazo amezishuhudia na kwamba hoteli ya Nyumabni ni moja ya hoteli yenye hadhi kubwa mkoani Tanga na ambayo itafungua ukurasa mpya kwa wawekezaji wengine.

"Mbunge wenu mnajua nimemaliza huko Ulaya, lakini hoteli hii nilipoingai kwenye vyumba nimekuta vitu ambavyo nikiwa huko Ulaya kwenye mahoteli makubwa nimekutana na mambo makubwa mabyo yamo humu ndani, hii ni changamoto kwa wawekezaji wengine kuona umuhimu wa kuwekeza mahoteli makubwa kama haya katika Jiji letu," alisema Injinia Nundu.



Na Mashaka Mhando, Tanga

Saturday, September 3, 2011

WAZIRI MKUU AWASILI MKOANI TANGA

Waziri Mkuu, Mizwngo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Kanisa la Anglicana nchini, askofu Mokiwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga septemba 3, 2011 akielekea Korogwe ambako Septemba 4, 2011 atakuwa mgeni rasmi kwenye ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Mteule Maimba Modlwa wa Dayosisi ya Tanga (Picha na ofisi ya waziri mkuu)




Tuesday, August 30, 2011

ANKO MO BLOGSPOT INAKUTAKIA EID MUBARAK NJEMA

Anko Mo Blogspot inawatakia waislam wote Eid Mubark njema. Ni muda mrefu hatukuwa pamoja japokuwa mlikuwa mkipata habari za hapa na pale, yote hiyo ilitokana na Mwezi Mtukufu wa ramadhan. Libeneke linaendelea.

Saturday, August 27, 2011

Friday, August 26, 2011

KING MAJUTO KUTOKA TANGA!

MSANII mkongwe wa vichekesho Nchini Amri Athumani 'King Majuto'amesema kuwa tangu ameanza kuigiza hajawahi kufikiria kuacha na wala hana mpango huo ingawa umri wake ni mkubwa.Msanii huyo ambae pamoja na umri wake mkubwa ana uwezo wa kuigiza nafasi zote ukitaka awe kijana nakua na ukitaka awe mzee anakua.


Alisema anawashangaa wanaofikiria kwamba ataacha leo au kesho kuigiza wamesahau kuwa hiyo ni kazi yake."Nawashangaa wanadhani nitaacha kuigiza leo au kesho eti umri wangu mkubwa mbona kwenye mashindano mbali mbali nawafunika"alisema Majuto.

Alifafanua kuwa pamoja na kuwafunika kwenye mashindano mbali mbali amekuwa halipwi fedha anazoahidiwa akishinda hivyo hataki tena kuitwa kwenye hayo mashindano uchwara.

"Nilishinda kwenyevshindano lililoandaliwa na Global Publishers lakini mpaka leo sijapewa zawadi yangu, wanaandaa mashindano bila kujiandaa matokeo yake kila nikishinda hawanipi changu hivyo sitaki tena na wakiniita siendi na ninawakumbusha mimi hii ndio kazi yangu kama alivyo Polisi .daktari ,mwalimu sasa kwani nini wanaidharau"alihoji Majuto.


Majuto alisema pamoja na misukosuko yote hiyo kupitia sanaa ya vichekesho amefanikiwa kujenga nyumba ya kuishi na anamiliki magari mawili.


Wednesday, August 24, 2011

MPIGIE KURA ZUBEDA SEIF

Mpigie Kura Miss Tanga, Zubeda Seif ili aweze kuibuka kidedea katika mashindano ya Miss Tanzania 2011. Kupiga kura andika neno 'mrembo' kisha acha nafasi unaandika namba 11 halafu unatuma kwenda namba 15550. Anza kumpigia kura sasa, onyesha uzalendo. Tanga inaweza!

Saturday, August 20, 2011

SIMBA NDANI YA MKWAKWANI LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA

Klabu Ya Simba Ya Jijini Dar Es Salaam, Itautumia Uwanja Wa Mkwakwani Kuchezea Michezo Yake Ya Ligi Kuu Ya Vodacom Inayotarajia Kuanza Augosti 20 Mwaka Huu, Kufuatia Uwanja Wa Taifa Ambao Ulipanga Kutumia Michezo Yake Kufungwa Na Serikali Baada Ya Kuharibika Kwa Michezo Ya Ligi Ya Kagame.


Kwa Mujibu Wa Habari Kutoka Kwa Mwenyekiti Wa Matawi Ya Simba Mkoani Tanga Mbwana Msumari Ni Kwamba Simba Itautumia Uwanja Wa Mkwakwani Kwa Vile Wanachama Wa Klabu Hiyo Wa Mjini Tanga Wameomba Hivyo Klabu Hiyo Kukubali.


Msumari Ambaye Pia Ni Meneja Wa Uwanja Wa Mkwakwani Alisema Kuwa Amewasiliana Na Mwenyekiti Wa Klabu Hiyo Ismail Aden Rage Kwa Njia Ya Simu Asubuhi Akiwa Dodoma Amemwakikishia Kwamba Klabu Hiyo Itatumia Uwanja Wake.


"Amenihakikishia Kabisa Kwamba Watatumia Uwanja Wa Mkwakwani Badala Ya Arusha Ambako Walisema Walipokuwa Kwenye Tamasha La Simba Day Hawakupata Mapato Ya Kutosha Hivyo Kuona Ni Vema Wakahama Uwanja Huo Na Kuutumia Uwanja Wetu," Alisema Msumari Na Kuongeza Kwamba Katika Tamasha Hilo Simba Walipata Milioni 25 Tu.


Kama Itakuwa Hivyo, Mashabiki Wa Tanga Wataweza Kupata Uhondo Mkubwa Hasa Timu Hiyo Ikija Kupambana Na Mtani Wake Yanga Ambaye Juzi Wamempa Kipacho Cha Mabao 2-0, Tusubiri Tuone Na Blogu Yako Hii Italifuatilia Kwa Karibu Suala Hili Ili Liweze Kukujuza.

Friday, August 19, 2011

JENGO LA WATU WENYE VVU NA UKIMWI LAZINDULIWA BOMBO TANGA

Mganga Mkuu Wa Mkoa Wa Tanga Dkt Ally Uledi Akisoma Risala Katika Ufunguzi Wa Jengo La Kliniki Ya Matunzo Na Matibabu Ya Watu Wenye Vvu Na Ukimwi Katika Hospitali Ya Bombo Mkoani Tanga.



Baadhi Ya Watu Mbalimbali Waliofika Kwenye Uzinduzi Huo Wa Kliniki Hiyo Ya Wagonjwa Wa Vvu Na Ukimwi Wakiwemo Waandishi Wa Habari Ambapo Kushoto Ni Lulu George Wa Nipashe Na Anyefuata Ni Fatma Matulanga Wa Tbc.

Mwakilishi Wa Shirika La Kimaraekani Cdc Dkt Stefan Wiktor Akitoa Salamu Kutoka Kwa Watu Wa Marekani Ambao Wamefadhili Mradi Huo Wa Ujenzi Wa Jengo Hilo Katika Hospitali Hiyo Aliteinama Ni Waziri Wa Fya Dkt Hadji Mponda Na Pembeni Yake Ni Katibu Tawala Wa Mkoa Wa Tanga Bw. Benedictor Ole Kuyan.


Meya Wa Jiji La Tanga Bw. Omari Guledi Akihitimisha Uzinduzi Huo Kwa Kueleza Kwamba Ili Kuondoa Mrundikano Wa Wagonjwa Kaika Hospitali Hiyo Ya Bombo, Halmashauri Ya Jiji La Tanga Wapo Mbioni Kujenga Hospitali Ya Wilaya Eneo La Masiwani.



Picha zote na Mashaka Mhando

Tuesday, August 16, 2011

COASTAL UNION KUKUTANA JUMAPILI



KLABU ya soka ya Coastal Union ya Tanga Agosti 13 inatarajia kufanya mkutano mkuu kwa ajili ya kukusanya na kuzungumza na wanachama kupanga mikakati itakayoifanya timu hiyo kung’ara kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hemed Aurora alisema pamoja na mambo mengine madhumuni ya mkutano huo ni kuzungumza na wanachama ili kupanga mikakati ya kuhakikisha timu yao hiyo inafanya vizuri kwenye Ligi Kuu.


(Gari ya Coastal Union)


Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2011/2012 inatarajiwa kuanza Agosti 20 katika viwanja mbalimbali nchini ambapo Coastal Union watashuka dimbani kucheza na Mtibwa Sugar

Saturday, August 13, 2011

CRDB YAWASAIDIA WAKULIMA WA KILIMO CHA MPUNGA KOROGWE

Afisa wa benki ya crdb la mkoani tanga akiangalia moja ya mashamba ya mpunga wilayani korogwe ambayo benki hiyo imekuwa ikisaidia kilimo cha umwagiliaji kuwainua wakulima.



Mfereji wa maji yanayokwenda kwenye mashamba ya mpunga ambao umekarabatiwa kwa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa mpunga wilayani korogwe kulikofanywa na benki hiyo ya crdb


COASTAL UNION YAITUMIA SALAM MTIBWA

KLABU ya Coastal Union imesema kuwa inatarajiwa kufanya vizuri katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu kati yao na Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani katika mchezo unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Mkwakwani agosti 20 mwaka huu.


Akizungumza na blog hii ,Mwenyekiti wa Klabu hiyo,Hemed Aurora amesema maandalizi ya mchezo huo hivi sasa yanaendelea vizuri ambapo timu hiyo inafanya mazoezi yake katika uwanja wa chuo cha Shinzu Mombasa chini ya kocha wao,Hafidhi Badru.

Aidha aliongeza kuwa uongozi wa Klabu hiyo unamshukuru mkuu wa mkoa wa Tanga,Said Kalembo ,mkuu wa wilaya ya Tanga pamoja na wabunge wa mkoa wa Tanga kwa kuwa msatri wa mbele kujitolea kuweza kuisaidia timu hiyo na kuhaidi kutowaangisha katika michezo mbalimbali ya ligi kuu msimu huu.

Aurora aliwataka wakazi wa mkoa wa Tanga pamoja na wadau wengine waliopo hapa nchini kujitokeza ili kuweza kuisadia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu na kuweza kurudisha heshima ya mkoa wa Tanga ambayo ilikuwa imepotea muda mrefu na hivi sasa imerudi tena.