BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, October 30, 2010

TWENDE TUKAPIGE KURA MTANZANIA!!

Naitakia kheri ya uchaguzi wa haki na salama nchi yangu ya Tanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu. Nawasihi watu wote waliojiandikisha kupiga kura waitumie nafasi hii ambayo hutokea kila baada ya miaka mitano katika kuchagua Rais, Mbunge na Diwani.

Kapige kura tarehe 31/10/2010 siku ya Jumapili, ni haki yako ya msingi. ANKO MO BLOGSPOT inakutakia kila la kheri.

CUF YAKAMILISHA KAMPENI ZAO LEO MJINI PANGANI!

Jioni ya leo katika pita pita zangu nilikutana na chama cha wananchi (CUF) wakimalizia kampeni zao kwa amani hapa mjini Pangani. CUF wamemsimamisha Ally Omary Mohammed katika nafasi ya Ubunge.

Baadhi ya wanachama wa chama hiko, tawi la Chake Chake wakielekea kwenye mkutano jioni ya leo.

CCM WAMALIZA KAMPENI KWA AMINI LEO PANGANI!

Baadhi ya wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa makini wakimsikiliza Ismail Pamba mgombea ubunge wa chama hicho, eneo la stendi kuu ya magari ya Pangani jioni ya leo.

Kesho ndio watanzania wanapiga kura kwa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.

Friday, October 29, 2010

Q CHILLAH LIVE LEO NDANI YA TANGA BEACH RESTORT!



Msanii wa bongo flava nchini anayetokea Tanga, Q Chillah anatarajiwa kufanya show ya ukweli usiku wa leo kunako hoteli ya Tanga Beach Resort iliyoko maeneo ya Sahare. Q Chillah atafanya onyesho la aina yake kwani atafanya Live Band!! Tukutane huko badae wadau!

Q Chillah akiwa katika Pozz

Wednesday, October 27, 2010

"SEMA"- WIMBO MPYA WA RAZY FLAVA KUTOKA TANGA TOWN!!

Unataka kujua kuwa Tanga kuna vipaji vya muziki...?? Chukua muda wako na usikilize wimbo huu wa huyu kijana anaitwa Razy Flava!!! Wimbo unaitwa "Sema" umetengenezwa pale Mwambao Records producer akiwa Nass B. Alikuwa mshindi wa kwanza kwenye mchakato wa kutafuta vijana wenye vipaji vya kuimba. Pembeni kulia palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!!

MATONYA AIPAGAWISHA LONDON!!!

Msani wa Bongo Flava kutokea Tanga, Tanzania Seif Shaban a.k.a Matonya hivi karibuni aliwapagawisha wakazi wa jiji la London nchini Uingereza kwa kupiga bonge la Show sambamba na msanii mwengine kutoka Kenya Nonini.

Wasanii hao wanatarajiwa kupiga show zao za mwisho siku ya Ijumaa kunako mji wa Manchester na Luton siku ya Jumamosi.

Big Up Tonya Time!!!

Tuesday, October 26, 2010

SAM WA UKWELI, OFFSIDE TRICK NA DR LEADER JUKWAA MOJA TANGA!!



Msanii wa Bongo Flava Sam Wa Ukweli anayetamba na wimbo wake wa Sina , anatarajiwa kuungana na wasanii wengine nguli kutoka Zanzibar Offside Trick ambao wanafanya vizuri katika mambo ya miduara katika Show ya usiku mmoja jijini Tanga itakayofanyika katika Club mashuhuri ya La Grand La Casa Chica siku ya jumamosi ya tarehe 6/11/2010.



Show hiyo ambayo imeandaliwa na Screen Masters Entertainment, itakuw ana kiingilio cha 10000 kwa wanaume na 7000 kwa akina dada. Hata hivyo Dr Leader msanii kutokea Tanga nae ametajwa kuwepo katika show hiyo..Dr Leader kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Macho Kodo.

VIJANA WA TANGA TOWN!!

Musa aliyevaa fulana ya mistari, Dj Bob Nass aliyevaa shati jeupe pamoja na Martin Kahinga a.k.a Tiny Daddy....na mshkaji aliyevaa fulana ya njano mwanzo, japokuwa simfahamu.

Monday, October 25, 2010

BREAKING NEWS!!!!!!.....MWAMBAO FM YAHAMISHIWA KANGE!!




Kituo cha redio cha Mwambao Fm kinachorusha matangazo yake kutokea mkoani Tanga, Tanzania kwa masafa ya ya 106.0 kimehamishiwa Kange. Kituo hiko ambacho hapo awali kilikuwa jengo la Bandari House, kimehamishiwa eneo la Kange sambamba na kampuni ya maziwa ya Tanga Fresh. Pichani mtangazaji mahiri wa kituo hiko Ahmed Khatibu maarufu kama Wawoo akiwa katika kipindi wakati Blog hii ilipotembelea redio hiyo.

Ahmed Khatibu akiendesha kipindi cha Arabian Flava.

Wakati nafika jamaa ndio alitoka nje na kunipokea.

Hili ndilo jengo ambalo redio Mwambao Fm linarusha matangazo yake kutokea hapo.

Hapa wakati naelekea kwenye jengo la Mwambao Fm....jengo linaloonekana pichani la kampuni ya Tanga Fresh.

Kwa mbali jengo la Tanga Fresh.

Milinzi akitufungulia mlango kuingia ndani.

Lango kuu la kuingilia Tanga Fresh, ambamo linapatikana jengo jengine la redio Mwambao Fm ya jijini Tanga.

KARIBU TANGA BEACH RESORT!!

About the Hotel

Tanga Beach Resort is one of Tanga's and indeed Tanzania's superior tourist hotels offering 40 bedrooms and 6 suites. The hotel also offers 5,000 square feet of meetings and functions space. The hotel is located in Tanga's Sahare area overlooking the beautiful Indian Ocean.

The hotel is part of a chain of hotels including Silver Rado which is a sister hotel situated in the centre of Tanga City as well as Giraffe Hotel located in Dar es Salaam.

Activities

Apart from relaxing in our hotel, you can take a tour of nearby exotic locations. One of our favourite tours is the northeastern corner of Tanzania to visit a virgin forest of Amani Nature Reserve where you can spend a couple of nights and then travel eastward to visit the hot caves of Amboni in Tanga coastal region.

The caves are hot so you need to wear light clothes, after an hour or 2 hour exploring the caves, you can travel down to Pangani Coast, a historical site which serve as a reminder of the strong Arabic and later German, British colonial period in East Africa. You will enjoy and experience nature, history, culture and beach relaxation.

Welcome

Tanga Beach Resort is not only the best luxury hotel in Tanga, it is also the best luxurious hotel for tourists and business travellers in Tanga, Tanzania. It started operations in the year 2009. The Hotel is located adjacent to the Indian Ocean in Tanga city which has a dynamic and historic past.

CONTACT

Tanga Beach Resort

P.O. Box 2294, Tanga Tanzania

Tel: +255 27 2645424/5
Fax:+255 27 2645426
Mobile: +255 785 171717
+255 683 750000
+255 683 850000

http://www.tangabeachresort.com
info@tangabeachresort.com


Sunday, October 24, 2010

DR SLAA AITEKA TANGA!!

Dr Slaa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa jijini Tanga, muda mchache kabla hajakwenda Dar Es Salaam kwenye mdahalo.

Picha inaongea.........Umati ukimsikiliza Dr Slaa

Friday, October 22, 2010

BIG UP KWA WANAFUNZI WOTE WA USAGARA SECONDARY SCHOOL WALIOMALIZA 2009!!

PANGANI WAIKASIRIKIA CCM KUHUSU HIFADHI YA SAADAN


WANANCHI Wilayani hapa wameishutumu Serikali kwa kuhamishia Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani kutoka Mkwaja na kuyapeleka Bagamaoyo na kudai hizo ni njama za kudhoofisha uchumi wa Pangani.

Waliahidi kumchagua mgombea ambaye atakuwa na ushupavu wa kuyarejesha makao hayo makuu kuwa Pangani kama awali kwa kuwa ndiyo yenye eneo kubwa la hifadhi hiyo ambayo ni asilimia 75 kuliko upande wa Bagamaoyo.

Walitoa shutuma hizo hivi karibuni wakati wakiuliza maswali kwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Pangani kupitia CUF, Omar Ali Mohamed (Masomaso) katika mdahalo uliofanyika ukumbi wa Safari Annex mjini hapa.

Hoja hiyo ilianzishwa na mwanajopo katika mdahalo huo,Aweso Jabu ambaye alimhoji mgombea huyo kama anafahamu kuwa Serikali imehamisha makao makuu ya Hifadhi ya Saadani kutoka Mkwaja kuipeleka sehemu ya Bagamoyo.

Licha ya mwezeshaji wa mdahalo huo Lilian Kallaghe kuwataka washiriki wa mdahalo huo kutorudia maswali yaliyoulizwa, lakini karibu kila aliyekuwa akisimama aliweza kugusia kuhusu mbuga hiyo huku wakilalamika kuwa kuna ajenda ya siri ya kuhujumu uchumi wa Pangani.

Akijibu swali hilo, Mgombea huyo wa CUF ambaye ndiye pekee aliyejitokeza katika mdahalo huo, alieleza kukerwa na kitendo hicho na kusisitiza kuwa iwapo atachaguliwa atahakikisha Makao makuu ya Saadan yanarejeshwa Pangani.

Thursday, October 21, 2010

MUHEZA LEO ASUBUHI!!!

Njia ya kuelekea Amani Natural Reserve.

Karibu na stendi, eneo la kutokea magari yote ya kuelekea mikoani. Hapa kuna matunda mengi sana.

Mlango wa kutokea.....wachuuzi wa matunda na vipuri mbalimbali huuza kupitisa madirshani.

Mchuuzi wa urembo akipitisha bidhaa zake dirishani mwa moja ya magari ya kuelekea mikoani.

Magazeti pia hupatikana eneo hili la kutokea.

Hatua chache kutoka Muheza, mkonge hutawala. Tanga inasifika pia kwa zao la Mkonge.

HISTORIA YA MUZIKI WA TAARAB KUTOKA TANGA!

(Pichani Waziri Ally wa Kilimanjaro Band, wakati huo akiwa Lucky Star akipiga kinanda)

Katika miaka ya 50 wanawake tisa wa Tanga walijikusanya na kuanzisha wakaanzisha kikundi cha kuimba walichokiita Raha til Fuad maana yake Raha ya Moyo. Akina mama hawa chini ya bibie aliyeitwa Mama Akida au aka Mama Lodi, waliendesha kikundi chao wakiwa wanaimba nyimbo za Siti Binti Sadi na tungo zao ambazo waliimba katika melody ya nyimbo za kihindi zilizotamba wakati huo.

Kundi hili liliendelea na kuanza kuruhusu wanaume kujiunga hasa wakiwa wapiga vyombo. Hata mtoto wa Mama Akida, Akida Jumbe hatimaye alijiunga na kundi hili kama mpiga accordion kwenye mwaka 1962. Kundi hili ambalo baadae lilikuja kuitwa Young Noverty,liliendelea mpaka kukaweko na mgawanyiko uliozaa kundi la Shaabab Al Waatan. Hapa ndipo kukaanza mtindo wa kuweko kundi pinzani jambo ambalo kwa njia ya ajabu sana limekuwa linadumu kiasi cha miaka kumi kumi.

Miaka ya 1960s Young Noverty na Shabaab al Waatan, 1970s Lucky Star Musical Club na Black Star Musical Club, 1980 Golden Star Taarab na White Star Taarab, 1990, Babloom Modern Taarab na Freedom Modern Taarab. Taarab ya Tanga ndo haswa inastahili kuitwa modern Taarab, kwani wao hawkufuata taarab ile iliyoletwa Zanzibar enzi ya Sultan Seyyid Barghash, kundi la taarab hii lilikuwa dogo na vyombo vyake vilikuwa pamoja na Gitaa la besi, gitaa la solo, drums bongos ,akodion au kinanda.

Nyimbo zao zilikuwa fupi na si ndefu kama za Kizanzibari., nyimbo zilitegemea mipigo ya ngoma za asili za kumbwaya na chakacha na hata baadaye mitindo kama rumba,bossa nova ilitumika kama mapigo. Na Taarab ya Tanga ndio iliyoanzisha moto wa vikundi vya taarab Tanzania Bara.

Moshi kulikuwa na New Alwatan,AzimioTaarab, na Blue Star Taarab , Arusha-Blue Star Taarab,Dodoma-Dodoma Stars,Kondoa –Blue Stars,Mbeya-Magereza Kiwira, Mwanza-ujamaa Taarab, Bukoba –Bukoba Stars, na muendelezo huu uliingia mpaka Burundi kutokana na mwana muziki mmoja alie julikana kama Athmani Mkongo, alitoka Burundi na bendi yake kufika Tanga akawa mwanamuziki mahiri wa Taarab na hata kuipeleka kwao Burundi.

Tuesday, October 19, 2010

HASSAN SHARIFF AIBUKA MSHINDI WA VODACOM TANGA CYCLING

Mgeni rasmi Bwana Kisheru sambamba na Sophia Wakati akitoa zawadi kwa washindi. Katika mbio hizo za Baiskeli, Hassan Shariff aliibuka kidedea na kuzawadiwa kitita cha Tsh.150,000. Shariff aliupata ushindi huo kwa kuendesha baiskeli ya mwendo yenye umbali wa kilomita 140 yaliyoanzia mkwakwani mpaka hale na kurudi Tanga,kwa kutumia masaa 4.140.01 kwa kuwapita washiriki 26.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo Bwana Ndibalema Kisheru akisema neno kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga,Meja Jeneral Said Kalembo, aliishukuru kampuni hiyo ya simu za mikononi Vodacom kwa kudhamini michuano hiyo ya Baiskel mkoani hapa.

Mzee Hiza kiongozi wa waendesha baiskel akitoa maelekezo kwa wandesha baiskel za kawaida maarufu kama 'bodaboda' katika mashindano ya Nyerere Vodacom Tanga Cycling eneo la Mkwakwani mjini Tanga.


Kundi la baiskeli za taili tatu walemavu wakijiandaa kuondoka katika eneo la Mkwakwani

Kundi la baiskeli la matairi mawili, likijiandaa na mashindano hayo.

Kazi ilianza....kila mtu akitaka kuibuka mshindi.

Monday, October 18, 2010

SALAM KUTOKA DENMARK!!

Tanga ya Mjarumani, ni mji wa kizamani aliovutiwa mkoloni na hatimae kukaa hapa nchini. Wa mbali na mikoani, walikuja mashambani, sikwambii viwandani na pirika za bandarini. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Umaarufu Mwambao, kwenye bahari ya Hindi umeandikwa ubao, kuwa siku hazigandi, Elimu ndio ufunguo, idai japo hupendi, jamani muhimu ngao, ndio siri ya ushindi Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Inakupenza imani, na hiyo yako subira, umeanikwa juani, kwa kupenda hadhara Tanga umaskini, na hali wewe ni bora amka upo vitani, kabla hujawa ngawira. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Umekuwa Tanga bora, kwa kutaka yako kura, nawe usifanye papara ukaipata hasara bila uwape harara, natumbo lenye kuhara silaha yako ni kura, mpe kiongozi bora. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??

Kushindwa kulinda maji, chura na chake kijicho amkeni wana mji, fungueni yenu macho sasani wenu mtaji, mtapata mtakacho danganya kuitwa jiji, wacheza mwanjificho. Una nini Tanga kunani, akuonae ni nani...??


Shairi hili nimetumiwa na mdau wa Vijimambo Vya Tanga kutoka Copenhagen, Denmark.

VIGOGO WA CCM TANGA WABWAGA MANYANGA!!

Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tanga kimepata pigo baada ya viongozi wake mashuhuri kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kwa kile walichodai ni baadhi ta wanachama kukosa imani dhidi yao. Wanachama hao waliandika barua za kujiuzulu nafasi zao huku wengine wakihama kabisa chama na kujiunga na Chama cha Wananchi CUF na kusababisha mgawanyiko mkubwa katika chama hicho.

Katika barua yake ilioandikwa kwa Katibu wa UVCCM wilaya ya Tanga ambayo Blog hii inayo nakala yake Kigogo wa Chama hicho Kata ya Ngamiani Kati Bi.Fatihiya Nyalusi alitangaza rasmi kujiuzulu nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani Chama.

Nyalusi ambaye alikuwa ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Ngamiani Kati huku akiwa Katibu wa Uhamasishaji wa Kata hiyo kupitia Jumuiya ya Vijana (UVCCM). Mbali na Nyalusi wengine waliotangaza kujiengua katika Chama hicho ni aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Tanga Hassan Omari ambaye pia ni alikuwa kiongozi wa Tawi A katika Ngamiani kati tawi A.

Omari ambaye alitangaza kujitoa CCM na kujiunga na CUF wakati mgombea Urais wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipofanya mkutano wake katika uwanja wa Tangamano. Kujiengua kwa viongozi hao mashuhuri katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu kimetasfiriwa na wachambuzi wa siasa za Tanga kuwa huenda ukaongeza mpasuko uliopo kwa sasa na kuhatarisha ushindi wa CCM katika nafasi za Udiwani na Ubunge.

Katika barua yake ya Oktoba 4 mwaka huu ambayo Blog hii inayo nakala yake, Nyalusi alisema ameamua kujiuzulu kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kifamilia na vilevile viongozi wa Chama kukosa imani naye. “Kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kifamilia na vilevile uongozi wa Chama kukosa imani na mimi nitakuwa mwanachama wa CCM” ilisema sehemu ya barua hiyo.


Na Oscar Assenga,Tanga

PIGIKA CLOTHING COMPANY IMERUDI TENA!!

Baada ya kupotea kwa muda mrefu kutokana na mpambano wa kusaka mshiko, sasa PIGIKA Clothing Company imerudi ki vingine, ikiwamo products mbali mbali mpya na zinazokwenda na wakati.

Kutokana na kupendwa kwa ubunifu wa t shirt za PIGIKA, nje na ndani ya Tanzania tumeamua kuja tofauti kwa sasa hasa kwa kutengeneza ONLINE Shop, ambapo mtu yeyote aliyepo nje ya Tanzania, anaweza pata pamba za PIGIKA kwa urahisi na kwa kununua kupitia njia ya CREDIT CARD na kutumiwa mzigo popote alipo.

Vilevile tumekuja na chata mbalimbali na MPYA, rangi mbalimbali na Materials tofauti, kukupa mteja nafasi nzuri zaidi ya kuchagua nini wapendelea nini.

Tovuti yetu mpya, www.pigika.co.tz ina maelezo yote ya zaidi, na pia waweza wasiliana nasi kwa barua pepe, simu au ufike ofisi zetu.
Kwa Mawasiliano zaidi....

facebook
http://www.facebook.com/pages/Pigika-Clothing-Company/142772582435434?ref=ts

tovuti
http://www.pigika.co.tz/

barua pepe
info@pigika.co.tz




Friday, October 15, 2010

Q CHILLAH LIVE NDANI YA TANGA TAREHE 29!!



Msanii nguli wa muziki wa Bongo Flava nchini Q Chillah anatarajiwa kufanya show ya ukweli siku ya ijumaa ya tarehe 29 hapa jijini Tanga, show itafanyika kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort. Kaa tayari mkazi wa Tanga!!

TANGA IS BEAUTIFUL BEYOND IMAGINATION

Tanga Region has many areas of tourist attractions sites, which are yet to be fully developed.

Thursday, October 14, 2010

WANAOVUMA KUTOKA TANGA! SWAHIBA WAKO....ANTONIO NUGAS

Kijana machachari anapokamata microphone, hasa anapokuwa redioni ama kwenye television. Anaitwa Antonio Nugas a.k.a Swahiba, anatokea jijini Tanga lakini kwa sasa yupo CLOUDS MEDIA GROUP kupitia Clouds Tv kama mtangazaji wa kipindi cha Kambi Popote ambacho hurushwa kila siku ya Jumatano. Tanga imekuwa ikitoa vijana wenye vipaji kila kukicha.

Nugas akiwa ndani ya studio za Clouds Radio kabla hajahamia Clouds Tv.

Hapa ni Lushoto mkoani Tanga katika harakati zake za kuandaa kipindi chake cha Kambi Popote.

Antonio Nugas akiwa na wasanii wa muziki wa Bongo Flava....wa katikati ni Hemed, pamoja na Kassim.

Wednesday, October 13, 2010

TANGA FLAVA YAZIDI KUONGEZA IDADI YA WASIKILIZAJI!!

ANKO%20MO
Quantcast

Endelea kufurahia muziki kutoka Tanga (Tanga Flava) Bonyeza hapo chini palipoandikwa TANGA FLAVA na utaipata kwa urahisi zaidi.