BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, November 30, 2010

MJI WA TOLEDO, MAREKANI NDIO MJI DADA WA TANGA, TANZANIA!!

Toledo is the fourth most populous city in the U.S. state of Ohio and is the county seat of Lucas County. The municipality is located in northwest Ohio on the western end of Lake Erie, and borders the State of Michigan.

Tanga is both the name of the most northerly seaport city of Tanzania, and the surrounding Tanga Region. It is the Regional Headquarters of the region. The city of Tanga sits on the Indian Ocean, near the border with Kenya. Major exports from the port of Tanga include sisal, coffee, tea, and cotton.

Situated near the historic center of Toledo, Eurostars Toledo offers beautiful views of the city. It has an outdoor swimming pool, a chic restaurant, and spacious rooms with free Wi-Fi.

Tanga Beach Resort is not only the best luxury hotel in Tanga, it is also the best luxurious hotel for tourists and business travelers in Tanga, Tanzania. It started operations in the year 2009. The Hotel is located adjacent to the Indian Ocean in Tanga city which has a dynamic and historic past.

GAZETI LA THE CITIZEN LAITAJA 'VIJIMAMBO VYA TANGA' KUWA NI HOT BLOG

Kwanza napenda kumshukuru Mungu muweza wa yote kwa kuweza kutuamsha tena siku ya leo na kuendelea na majukumu yetu ya kila siku, ni yeye kwa mapenzi yake ndio amependa sote tuione siku ya leo....Pia nawashukuru wale wote ambao kila siku wanachukua muda wao kwa kupitia hii Blog, ni yenu na mimi nipo hapa kuwatumikia. Nachukua muda huu pia kuwashukuru gazeti la The Citizen kwa kuitaja Blog hii kuwa ni moja ya Blog zinazofanya vizuri nchini Tanzania.

Nafarijika kuona kazi ninayofanya inawagusa watu wengi. Tuendelee kufurahia Blog hii....inawezekana huu ndio mwanzo mzuri wa kupata Tuzo endapo litatokea shirika la kuandaa mashindano ya Blog zinazofanyakazi na kukubalika na wengi.

Monday, November 29, 2010

BELLE 9 ALIVYOWASHA MOTO JIJINI TANGA!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Belle 9 akiwarusha wakazi wa jiji la Tanga siku ya ijumaa wakati msanii huyo alipofanya show yake kunako La Club Lacasa Chica.......hata hivyo show hiyo pia ilipewa baraka na msanii mwengine ambaye hakuwa kwenye ratiba hiyo kiasi cha kufanya watu kupiga shangwe za kutosha punde alipoitwa juu ya steji kusalimia- namzungumzia Tunda Man wa Tip Top Connection. Ilikuwa poa sana pia alipopanda Man Sasha kutoka Tanga Town.

Kutunza ilikuwa inaruhusiwa...Belle 9 aliweza kukonga nyoyo za mashabiki wake ipasavyo,

Belle 9 akipiga show mbele ya mashabiki.

Dj D Whte ndio alikuwa akiongoza show ya Belle 9

Amir kutoka Breeze Fm Radio ndio aliokuwa msema chochote.......hapa wakati anafungua show.

Belle 9 akiwa na Dj wa Breeze Fm ya jijini Tanga Dj Bob Nass wakati alipofika kwenye redio hiyo kwa ajili ya kufanya interview.

Belle 9 ndani ya Breeze Fm Radio akifanya mahojiano

TANGAZO LA SIKUKUU YA UHURU WA TANZANIA NCHINI DENMARK!!

TANGA LEO MCHANA!!

Eneo la barabara ya nane njia ya kuelekea Chuda

Stendi ya daladala...kuelekea stendi kuu ya mabasi ya mikoani. Mbele ni daladala ya Mikanjuni-Raskazoni.

Njia ya kuelekea Chuda....panapopatikana Hoteli ya Mtendele pamoja na Nyinda

Kituo cha kuweka mafuta- kipo karibu na stendi kuu ya mabasi ya mikoani.

Thursday, November 25, 2010

BELLE 9 NDANI YA CLUB LACASA CHICA IJUMAA HII!!

Msanii mahiri wa kizazi kipya nchini Belle 9 anatarajiwa kufanya onyesho siku ya kesho kunako La Club LaCasa Chica jijini Tanga katika harakati za kuelekea sikukuu ya Uhuru. Akizungumza na Blog hii mmoja wa waandaji wa onyesho hilo Dj RogerKiss amesema kuwa, wameamua kumleta msanii huyo ili kukonga nyoyo za mashabiki wanaopenda kujivinjari katika Club hiyo ya kisasa



Belle 9 hadi sasa anatamba na nyimbo zake kama 'Sumu Ya Penzi', 'Masogange', pamoja na 'We Ni wangu'

TANGA OYYEEE!! MH. NUNDU AUKWAA UWAZIRI!

Mbunge wa Tanga mjini Mh. Omari Nundu hatimae ameitoa Tanga kimasomaso baada ya kuchaguliwa kuwa Waziri na Rais Jakaya Kikwete hapo jana wakati akitangaza baraza la Mawaziri.

Nundu ametajwa kuwa waziri katika wizara ya Uchukuzi, sanjari na naibu wake Mh. Athumani Mfutakamba.

Omari Nundu ni Mbunge wa jimbo la Tanga mjini, na aliibuka kidedea kwa jumla ya kura 40,225 na hivyo kuwabwaga wagombea wa vyama vya upinzani waliokuwa wakiwania jimbo hilo.

Kila la Kheri Mheshimiwa Nundu.


Wednesday, November 24, 2010

MWALIKO WA SIKUKUU YA UHURU KUTOKA NORWAY!!

WATANZANI WAISHIO BERGEN NORWAY TUNAFUNGUA UMOJA WETU WA WATANZANIA HAPA BERGEN NA PAMOJA NA KUSHEHEREKEA SIKU YA UHURU WA TANZANIA KWA PAMAMOJA NA WATANZANIA WENZETU POPOTE WALIPO DUNIANI SIKU YA TAREHE 10.12.2010.

KATIKA SHUGHULI YETU HII MGENI RASMI ATAKUA NI MWAKILISHI WA BALOZI WA TANZANIA KUTOKA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI SWEEDEN. TUNAWAKARISHA WATANZANIA WOTE WAISHIO BERGEN NORWAY NA NJE YA NCHI YA NORWAY KUJA KUJUMUIKA NASI KATIKA GHAFLA HII. NAWE UKIWA MMOJA WAPO KARIBU SAANA.

NAPIA TUNA PAGE YETU YA CHAMA KWENYE FACEBOOK INATAMBULIKA KWA JINA LA (WATANZANIA BERGEN) WATU WOTE WANAKARIBISHWA KUWA NA URAFIKI NASI, NA PIA TUNAKARIBISHA MAONI KWA KUPITIA ANUANU PEPE YA CHAMA NAYO NI ( WATANZANIA.BERGEN@GMAIL.COM)

UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.


KARIBUNI SAANA.

MIRIAM CHEMMOSS- NI KWELI ASILI YAKE TANGA

Endapo kuchanganya utaifa,damu na tamaduni mbalimbali ni mojawapo ya chachu za mafanikio fulani hapa duniani, basi ushahidi wa dhana hiyo unaweza kuupata kwa kuangalia maisha ya mrembo Miriam Chemmoss(pichani).

Miriam ni muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model) ambaye mpaka hivi leo ana haki ya kusimama na kujivunia rekodi yake katika ulimwengu changamani wa sanaa na maonyesho. Mwenyewe anasema safari yake ndio kwanza inaanza kwani bado ana ndoto na malengo chungu mbovu ya kutimiza. Hivi leo kazi zake nyingi anazifanyia kutokea jijini New York nchini Marekani anapoishi.

Kama ilivyo kwa wasanii wengi, safari ya Miriam katika ulimwengu wa sanaa inaanzia tangu akiwa mwanafunzi mdogo. Lakini ni pale alipohamia jijini New York mwaka 2004 na kujiunga na kundi maarufu lililojulikana kama The Marvallettes Revue lililokuwa chini ya Pam Darden, ndipo nyota yake ilipoanza kung’ara ipasavyo. Baadaye alijiunga na kundi lingine maarufu la Soukouss Stars kama mwimbaji pekee wa kike na mnenguaji kabla ya kuamua kuimba peke yake(solo artist) mwaka 2006.

Kwa upande wa uigizaji, Miriam ameshaigiza katika show mbalimbali maarufu ikiwemo ile ya “District” katika kituo maarufu cha televisheni cha CBS. Pia ameshiriki katika “Bedford Diaries” ya Warner Bros. Sauti yake imetumika katika matangazo mbalimbali ya biashara kama vile Western Union(USA-African Market) nk.

Kwa upande wa mavazi Miriam amewahi kuwa model wa jeans za Levi’s,Getty Images/Brazilian Salsa Club(Print),Bebe Noir Clothing Line,New York nk.Mwaka 2007 mtandao wa Jamati.com ulimtaja Miriam katika orodha yao ya Top 10 Sexiest African Women akiwa ni miongoni mwa wasichana wawili kutoka eneo la Afrika Mashariki.

Miriam asili yake kwa upande wa Mama anatokea kijiji cha Tingeni-Muheza, Tanga na pia marehemu bibi mzaa mama ni Mbondei kabisa. Ni faraja iliyoje Tanga kutoa msanii mkubwa kama huyu duniani. Kutaka kumjua vizuri Miriam tembelea website yake BONYEZA HAPA au kwa Facebook yake BONYEZA HAPA

Tuesday, November 23, 2010

Monday, November 22, 2010

'DESEMBA 26' NI HADITHI YA KUSISIMUA

Unapenda hadithi za kusisimua zinazofanya ujisikie furaha pindi unaposoma...!!?? Leo gazeti la HABARI LEO limetoa hadithi yangu ya DESEMBA 26, ni hadithi nzuri ya kusisimua ambayo kwa hakika hutasita kuacha kuisoma pindi utakapoanza na sentinsi ya kwanza. Tafuta gazeti hili la leo na hata kesho....uendelee kunifuatilia katika simulizi hii.

'NDANI YA ONE WEEK'- WA SUMA LEE KUTOKA TANGA!

Friday, November 19, 2010

KIKUKU- NI KWELI ASILI YAKE TANGA..?

Leo nimepata E-mail kutoka China.....kuna mdau kutokea huko ambaye anatokea Tanga anataka kujua kuwa ni kweli "KIKUKU" kilianza kuvaliwa na wanawake wa Tanga...?


Thursday, November 18, 2010

Tuesday, November 16, 2010

HAPPY EID EL HAJJ KWA WAISLAMU WOTE!!

Anko Mo Blogspot (VIJIMAMBO VYA TANGA) inawatakiwa Waislamu wote heri ya sikukuu ya Eid El Hajj. Inshaalah!

SALAM ZA EID EL HAJJ KUTOKA KWA FAMILIA YA CHUMA!

Issa Chuma na Mohammed Chuma wanawatakia waislam wote sikuuu ya Eid El Hajj njema tuisherehekee kwa amani

Z ANTO ATAKUWA TANGA EID HII!!

Nimedokezwa kuwa msanii Z Anto aliyewahi kutamba na wimbo wake wa 'Binti Kiziwi' anatarajia kufanya show jijini Tanga katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj. Kwa sasa msanii huyo anatamba na wimbo wake wa 'Kisiwa cha Malavidavi'

KUTANA NA MARAFIKI WENGI KUTOKA TANGA

Je wewe unatokea TANGA au hata sehemu nyengine ya nchi..!!? Upo Tanzania ama nje ya nchi, na unahitaji kukutana na marafiki kutoka TANGA ili upate kujua zaidi ni kitu gani kinaendelea katika mkoa huu!!? Nafasi hii hapa sasa. Ungana na MARAFIKI WA TANGA ili kuweza kubadilishana nao mawazo.

Kujiunga na MARAFIKI WA TANGA BONYEZA HAPA

Monday, November 15, 2010

ROMA FUNIKO BOVU SHOW YA EBONY FM IRINGA!!


Roma anasema "ASANTENI SANA MASHABIKI WA IRINGA...kwa mapokezi yenu mazuri...show ilikuwa kidole cha mwisho juu kuanzia ngoma ya kwanza hadi ya mwisho...daaaaah mpo live sana iringa...naahidi nitarudi tena huko......"

Mashabiki wakiwa makini kufuatilia show (Picha zote kwa hisani ya Dj Choka)

UZURI WA BUSTANI ZA JIJI LA TANGA!






Friday, November 12, 2010

WIMBO MPYA WA DR LEADER- "MBUZI KAGOMA KWENDA'

Msanii wa Bongo Flava kutoka Tanga, Tanzania Dr Leader aliyewahi kutamba na nyimbo zake kama "Msambaa", "Macho Kodo" na nyengine nyingi, ameachia ngoma mpya yenye mahadhi ya mduara inayoitwa "Mbuzi Kagoma Kwenda". Fanya kama unachukua muda wako na kuiskiliza hapo juu kulia palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!!

KAMA HUJAWAHI KUFIKA MUHEZA- BASI ITAZAME HAPA!!



Fika muheza kwa kutazma video hii.


Thursday, November 11, 2010

LUSHOTO HIYO MZEEEE!!!

Benki ya NMB Lushoto.

Gereza la Lushoto

Boda boda kila sehemu Lushoto. Pikipiki zikiwa zimepaki.

Stendi kuu ya mabasi lushoto.

Akina mama ambao ni wachuuzi wa matunda na mbogamboga.

"TUKICHOKA HUWA TUNAPUMZIKA NA SISI!!"

Maafande wa kike wakiwa chini ya mti wamepumzika. Camera ya Anko Mo Blogspot ilikutana na maafande hawa eneo la Bago njia ya kuelekea Pangani.

Wednesday, November 10, 2010

HAPPY BIRTHDAY ASMAH MAKAU!!!

Happy Birthday dada yangu Asmah Makau, umezaliwa tena upya siku ya leo. Mungu akuzidishie amani na uzima katika maisha yako pamoja na famili yako. Inshaalah!! Asmah ni mkurugenzi mtendaji wa Five Brothers Entertainment, kampuni yenye mamlaka ya kuandaa Miss Tanga kila mwaka.

HALE LEO ASUBUHI!!!!

Kitu cha TASHRIFF brand new kikiwa eneo la Hale, kuelekea Dar Es Salaam leo asubuhi. Kama ulipata kusikia Tanga kumekucha basi hukudanganyika ndugu yangu.....mabasi ya abiria kwenda mikoani yapo supa ile mbayaa!!

Kona ya kuelekea Hale Power Station

Wakazi wa eneo la Hale wakivuka barabara katika shughuli zao za kila siku.

Soko huria Hale