BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, September 24, 2011

HONGERENI CATHBERT KAJUNA NA DADA ESTER ULAYA KWA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA

Cathbert Kajuna na dada Ester Ulaya hatimaye wamefunga pingu za maisha. Maharusi wote ni marafiki wa karibu wa Anko Mo Blogspot. Mungu awape neema na baraka katika maisha yenu ya ndoa.



Hapa wakionyesha vyeti vyao vya ndoa.

Kajuna najua hapa presha ilikuwa inapanda na kushuka. Hongera sana kaka.



Monday, September 19, 2011

SHILLINGI VIT CLASS USAFIRI PANGANI- TANGA MPAKA DAR

SHILLINGI VIP CLASS ni mabasi mapya kabisa ambayo yanafanya safari zake PANGANI-TANGA mpaka DAR kila siku kuanzia saa moja kamili asubuhi. Halafu DAR- TANGA mpaka PANGANI.



Unafika mpaka Pangani na kuina fukwe nzuri za kuvutia.


Wednesday, September 7, 2011

KISIMA CHA MAJI CHAZINDULIWA LUSHOTO

Na Oscar Assenga,Lushoto.
MRADI wa Kisima cha maji katika kituo cha Afya Kangangai uliofadhiliwa na kikundi cha urafiki wa ujerumani na Tanzania (Deustsch Tanzanischer freundeskreis DTF)umezinduliwa juzi wilayani Lushoto.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Daktari Mfawidhi wa kituo hicho,Bakari Mavura alisema mradi huo ulianza mwaka 2008 kutokana na kuwepo kwa tatizo la maji katika kata ya Mwangoi tarafa ya Mlalo ambapo waliamua kukaa chini na kuanza kubuni mradi huo wakishirikiana na kamati ya afya ya kituo hicho.Mavura alisema baada ya kubuni mradi huo waliweza kuishirikisha jamii na kuweza kupata marafiki wa kikundi cha wajerumani na walipotoa mawazo na uweza kuyafanyia kazi.


Katika mradi huo shilingi milioni 16.2 zimetumika kati ya hizo shilingi milioni kumi laki mbili zimepatikana kutoka kwa kikundi cha urafiki na halmashauri ya wilaya ya Lushoto imechangia shilingi milioni sita.


Mavura alielaza maji hayo yatakuwa ni kwajili ya kituo hicho pamoja na watumishi wanaofanya kazi ambapo zaidi ya watumishi 10 pamoja na wananchi 22,000 watanufaika mradi huo pamoja na wagonjwa ambao watakwenda kupata matibabu kwenye kituo hicho cha afya cha Kangagai. "Wananchi wanapaswa kukitunza vizuri kisima hicho ili kuweza kuondokana na tatizo la maji "alisema Mavura.


Aidha aliongeza kuwa wanatarajiwa kuishirikisha jamii katika utunzji wa kisima ili kiweze kuwa endelevu.Alieleza kuwa licha ya kukamilika kwa kisima hicho wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa shillingi Millioni moja na laki nane kwa ajili ya kumalizia ufungaji wa mfumo wa maji safi na maji taka kwenye majengo ya kituo chicho.Mwisho.

ZUBEDA SEIF MKALI WA KUIGIZA VODACOM MISS TANZANIA

Mrembo Zubeda Seif kutoka Tanga aliyejinyakulia kitita cha Dola 1000 akimnanga muingizaji nguli Jacquline Wolpa wakati wa kutafuta mrembo wa Vodacom Miss Tanzania aliye na kipaji cha uigizaji lililozaminiwa na Kampuni ya Papazi.

Monday, September 5, 2011

HOTELI MPYA YAZINDULIWA TANGA

MMILIKI wa hoteli mpya inayojulikana kwa jina la NYUMBANI Hotel & Restaurant Bw. Aloyce Kimaro aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, amewataka wafanyabiashara na wananchi wa Jiji la Tanga, kumuunga mkono katika uwekezaji wake mpya wa sekta ya hoteli ili kusaidia kuongezeka kwa pato la uchumi la mkoa wa Tanga.

Akitoa neno la shukurani kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopo mkabala ya jengo la posta katikati ya Jiji la Tanga, mbunge huyo wa zamani alisema alipata wazo la kufungua hoeli hiyo mkoani Tanga, kushirikiana na wana-jamii kuongeza pato la mkoa hasa kutokanana uwepo wa bandari na shughuli nyingine za kiuchumi.

Alisema kutokana na uwepo wa bandari na kukua kwa shughuli nyingi za kibiashara alionelea kufungua hoteli hiyo hivyo amewataka wananchi na wafanyabiashara kushirikiana naye kumsapoti katika kuhakikisha hoteli hiyo inatoa huduma za kisasa na za kimaaifa.

Bw. Kimaro ambaye anaendesha hoteli hiyo akiwa na wakurugenzi wengine Bw. John Kessy na Mansfeld, wanatarajia kufungua hoteli zenye jina hilo katika mikoa yote nchini ili kuhakikisha wanawekeza katika sekta hiyo wakiwa kama Watazania na kusaidia kukua kwa uchumi wa Tanzania. Hoteli hiyo ya Tanga inafuatia kuwepo kwa hoteli nyingne zenye jina hilo la nyumbani katika miji ya Mwanza na Moshi.

Akizindua hoteli hiyo Waziri wa Uchukuzi, Injinia Omar Nundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Tanga, alisema katika kutembea kwake Ulaya hoteli hiyo inaingana kabisa na ambazo amezishuhudia na kwamba hoteli ya Nyumabni ni moja ya hoteli yenye hadhi kubwa mkoani Tanga na ambayo itafungua ukurasa mpya kwa wawekezaji wengine.

"Mbunge wenu mnajua nimemaliza huko Ulaya, lakini hoteli hii nilipoingai kwenye vyumba nimekuta vitu ambavyo nikiwa huko Ulaya kwenye mahoteli makubwa nimekutana na mambo makubwa mabyo yamo humu ndani, hii ni changamoto kwa wawekezaji wengine kuona umuhimu wa kuwekeza mahoteli makubwa kama haya katika Jiji letu," alisema Injinia Nundu.



Na Mashaka Mhando, Tanga

Saturday, September 3, 2011

WAZIRI MKUU AWASILI MKOANI TANGA

Waziri Mkuu, Mizwngo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Kanisa la Anglicana nchini, askofu Mokiwa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga septemba 3, 2011 akielekea Korogwe ambako Septemba 4, 2011 atakuwa mgeni rasmi kwenye ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Mteule Maimba Modlwa wa Dayosisi ya Tanga (Picha na ofisi ya waziri mkuu)