BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, June 30, 2011

UFUNGUZI WA TAMASHA LA FILAMU TANZANIA (TANGA, TANGAMANO) LAFANA








Hizi ni baadhi ya picha za tukio la ufunguzi wa Tamasha la Filamu Tanzania linalofanyikka hapa mkoani Tanga kunako uwanja wa Tangamano huku likipewa udhamini mnono na kinywaji cha Grand Malt. Kaa tayari kwa picha nyengine zaidi.



Wednesday, June 29, 2011

NINAOMBA KURA ZENU ZA DHATI


Habari wadau wa vijimanbo vya tanga, natumai wote ni wazima wa afya tele, kama hivyo ndivo basi sote tumshukuru Mungu muweza wa yote. Nakuja mbele yenu siku ya leo kwa kusudi moja tu ambalo kwa hakika tutashirikiana kwa pamoja na naamini tutafanikiwa. Ni muda mrefu tangu tuwe pamoja tukipashana habari za Tanga na hata zile zinazojiri kutokea nyje yaTanga, ndugu zangu watanzania wenzangu na wale wote wanaotokea Tanga.

Kuna hii kitu inaitwa TANZANIAN BLOG AWARDS 2011, natumai mmeisikia. Lengo la kuandika waraka huu kwenu ni kuwaomba kura zenu ili Blog yenu ya vijimambo vya tanga iweze kuibuka kidedea katika mchakato huo ambapo imechaguliwa kwenye category kadhaa ambazo ni Best Informative - Entertainments, Best Entertainments, Best News, pamoja na Best Music.

Mambo yote haya ukiyatazama kwa kina yapo kwenye Blog hii na nimatumaini yangu mnayafurahia sana. Jinsi ya kupiga kura BONYEZA HAPA kisha tazama upande wa kulia utaona vipenge kadhaa pamoja na nilivyokutajia kisha piga kura yako palipoandikwa http://ankomo.blogspot.com ukishabonyeza kwenye kile kiduara unabonyeza palipoandikwa VOTE, na hapo utakuwa umeipigia kura Blog yako.

NASHUKURU SANA NA NIMATUMANI YANGU NITAPATA KURA ZENU. NAOMBENI SANA!!


Monday, June 27, 2011

Friday, June 24, 2011

GRAND MALT TANZANIA OPEN FILM FESTIVAL NI JUNI 27 JIJINI TANGA

Kulia ni Mkurugenzi wa Sofia Production Musa Kissoky akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo kuhusu Tamasha la wazi la filamu nchini Tanzania litakalojulikana kama (Grand Malt Tanzania Open Film Festival) lililopangwa kuanza tarehe 27 Juni hadi Julai 3 Mwaka huu mjini Tanga. Katikati ni Meneja Masoko TBL Fimbo Butallah na Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam.

Wednesday, June 22, 2011

SIKILIZA 'MATHEMATICS' WIMBO MPYA WA ROMA!

Sikiliza wimbo mpya wa msanii nguli wa hip hop kutokea Tanga, Tanzania anafahamika kama R.O.M.A.....wimbo unaitwa MATHEMATICS umetengenezwa pale Tongwe Records. Roma tayari anatamba na nyimbo zake nyengine kama Tanzania, Mr. President, Pastor pamoja na Mechi za Ugenini. Kusikiliza wimbo wa MATHEMATICS tazama kulia pembeni palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Wimbo namba moja.

Tuesday, June 21, 2011

MISS TANGA 2011 NI ZUBEDA SEIF

Miss Tanga 2011 Zubeda Seif akipokea zawadi ya Flat Screen kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Dr Ibrahim Msengi aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo. Miss Tanga 2011 iliandaliwa na kampuni ya New Face Entertainment.



Miss Tanga 2011 kati kati Zubeda Seif mshindi wa pili kushoto Mwajabu Juma na mshindi wa tatu kulia Siphael Nashon

Miss Tanga 2011 Zubeda Seif akipita na vazi la ubunifu. (Kumradhi wadau kwa kuchelewa kuwaletea picha hizi)



KITABU CHA 'YALIYONIKUTA TANGA' KINAKUJA KAA TAYARI!!



……Kwa mujibu wa yule dereva teksi, tulikuwa tayari tumekwishafika katika eneo alilolitaja kuwa ni Four Ways, moja kati ya eneo maarufu linalokutanisha barabara nne mahali pamoja. Nilitulia tuli mule garini.

Pamoja na kwamba kulikuwa ni usiku lakini niliweza kuona baadhi ya majengo yaliyokuwa pembezoni mwa barabara kutokana na taa za gari zilizokuwa zikimulika wakati tunaikaribia kona ya kuingia upande wa kushoto, kitendo ambacho kingefanya tuiache ile barabara tuliyokuwa tunakuja nayo.

Jengo moja lenye ghorofa tatu lililojengwa vyema likiwa na ukurutu wa rangi ya manjano, lilikuwa upande wa barabara ya pili kulia kwetu. Kulikuwa kimya, taa zikiwa zimewashwa kila upande wa jengo, huku wadudu aina ya kumbikumbi wakiwa wanaruka ruka juu ya zile taa. Hapakuwa na mtu pale nje.
Mbele tena kwa upande wa ile barabara, kulikuwa na jengo jengine lenye ghorofa nne likiwa limepakwa rangi nyeupe. Chini ya jengo hili palikuwepo na fremu tano za maduka, sikufahamu yalikuwa maduka ya nini lakini palionekana penye biashara nzuri, yote yalikuwa yamefungwa wakati ule.

Watu watatu waliokuwepo nje ya lile jengo, niliwahurumia sana kutokana na ubaridi mkali ulioambatana na upepo uliokuwa unavuma. Wawili kati yao walikuwa wamejibanza kwenye moja ya viambaza vilivyoko pale. Walijifunika makoti huku wamelalia maboksi.

Mwengine ambaye niliweza kumuona vizuri alikuwa amekaa kwenye kiti, amevalia gwanda za rangi ya buluu huku ameshikilia rungu kwa mkono wake wa kulia. Ni mwanamke!!! Tena bila shaka alikuwa ni mlinzi.................................


KAA TAYARI, KINAKUJA HIVI KARIBUNI!!

Tuesday, June 14, 2011

KAA TAYARI- ANAKUJA TENA....!!! ITS ROMAAAAAA



INATIA MOYO- ASANTE FRESH JUMBE KUTOKA TOKYO!

Jana nilipata ujumbe kutoka kwa Mwanamuziki Fresh Jumbe ambaye anafanya shughuli zake za muziki kule nchini Japan mjini Tokyo, Fresh Jumbe asili yake ni Tanga. Ujumbe wenyewe ni huu hapa chini...

"Mkuu, Saluti. Kazi unayofanya ya kutangaza mkoa wetu, unastahili nishani. Tupo pamoja."

Fresh Jumbe- Tokyo.

Monday, June 13, 2011

MSIKILIZE ROMA NA UJIO WAKE MPYA!

Ujio mpya wa msanii ROMA kutoka Tanga, Tanzania BONYEZA HAPA Umsikilize, ana kitu cha muhimu kwa ajili yako.



Thursday, June 9, 2011

KWA WANANCHI WA JIMBO LA BUMBULI- WASILIANA NA MBUNGE WAKO NDUGU JANUARY MAKAMBA

Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya SMS Kati ya Wananchi wa Bumbuli na Mbunge wao, Ndugu January Makamba, yamezinduliwa tarehe 29 Januari 2011 kwenye Semina Elekezi aliyoitisha Mbunge huyo wa viongozi na watendaji wa vijiji na Kata wapatao 250 wa Jimbo la Bumbuli.

Mfumo huo utaanza kutumika tarehe 10 Februari 2011, baada ya kipindi cha elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo kuu kukamilika. Kwa kifupi, wananchi wanapaswa kutuma kero, maoni na ushauri kwa Mbunge ambaye kila siku, yeye na wasaidizi wake, watakuwa wanasoma meseji hizi na kuwajibu au kuwatafutia majibu.


Kama kuna taarifa za haraka ambazo inabidi Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri, au Mkuu wa Polisi wa Wilaya au Bwana Afya inabidi azijue, basi Mbunge atasaidia kuzifikisha kwa haraka zaidi.


Huduma hii haiondoi haja ya Mbunge kuendelea kutembelea Jimbo na kuonana na watu wake. Ni kwamba, simu au SMS, kama njia rahisi ya mawasiliano, hakuna haja ya kuacha kuitumia wakati wananchi wenyewe wanaitumia sana.


Inawezekana ikaonekana ni gharama kubwa kwa Mbunge lakini hata haiko hivyo, ni suala ya mazungumzo kati ya Mbunge na mitandao ya simu ili gharama iwe at cost na Mbunge bado anaweza kugharamia hili kwa nusu ya posho yake (wapo Wabunge ambao wamejitolea nusu mshahara kwa jambo moja au jingine - kwa Mbunge wa Bumbuli hili ni muhimu).

Wednesday, June 8, 2011

FROM DAR TO TANGA- WOTE MNAKARIBISHWA!

NANI KUINGIA KATIKA ORODHA HII YA MISS TANGA HAPO JUMAMOSI..?

NANI KUWA MISS TANGA 2011....????

Anna Kiwambo Miss Tanga 2010

Glory Chuwa Miss Tanga 2009

Nadya Ahmed Miss Tanga 2008

Victoria Martin Miss Tanga 2007

Tuesday, June 7, 2011

BEKA KUTOKA THT NAE KUISINDIKIZA MISS TANGA 2011 JUMAMOSI

Msanii kutoka THT anayefahamika kama Beka nae atakuwepo siku ya jumamosi ya tarehe 11/06/2011 pale Mkonge Hoteli ambapo itafanyika Miss Tanga 2011. Mambo mazuri yanazidi kunoga Miss Tanga....usIkose!


Miss Tanga 2011 'YES WE CAN'


WAZIRI MKUU AKITETA JAMBO NA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOANI TANGA MJINI DODOMA

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Walemavu) Mh. Al.Shaymaa Kwegyir mara baada ya kutoka kwenye kipindi cha maswali na majibu kwenye mkutano wa nne wa Bunge la Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012. (Picha kwa hisani ya Michuzijr)

BARABARA ZINAJENGWA SASA TANGA

Katika pita pita zangu nilikutana na ujenzi wa barabara jijini Tanga. Safiii!!



Monday, June 6, 2011

LINAH KUISINDIKIZA MISS TANGA 2011 JUMAMOSI



Msanii kutoka THT Linah Sanga anatarajiwa kupamba shindano la kumsaka mnyange wa Miss Tanga 2011 linalotarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 11/06/2011 kunako Mkonge Hoteli. Endelea kutembelea Blog utajua ni msanii gani mwengine atakayepiga show siku hiyo. Miss Tanga 2011 "YES WE CAN"



'SIO YA KUKOSA'

Thursday, June 2, 2011

HAWA NDIO WATAKAOIWAKILISHA TANGA KWENYE SERENGETI FIESTA FILAMU!

Kutoka kushoto LEAH MASAMBAJI, (ZAMARADI MKETEMA), ATU JAMES, FARIDA ABDALLAH pamoja na LUKEI PENTZEL.. hao ni baadhi ya waliopatikana katika mkoa wa TANGA kupitia Serengeti Fiesta Filamu ambapo ilikuwa ni mchakato wa kutafuta vipaji vipya kabisa kwenye swala zima la filamu.

Wakiwa katika picha ya pamoja- (Picha kwa hisani ya blog ya Zamaradi Mketema)

GRAND MALT TANZANIA OPEN FILM FESTIVAL INAKUJA TANGA

GARI INAUZWA



Petro Engine, outomatic gear, and 2L engine.

The price is 20M but we can talk.


Exported from Japan- haijatumika.

kwa mawasiliano piga namba 0653144551 au 0754210106

Wednesday, June 1, 2011

'SISI TUTAIJENGA TANGA' GROUP MPYA KUTOKA TANGA!

Je wewe ni mdau madhubuti, mpenda maendeleo kutokea Tanga. Wanaharakati wanaopigania Tanga wanakuletea GROUP nyengine kwenye mtandao wa facebook inayojulikana kwa jina la 'SISI TUTAIJENGA TANGA' humo kuna mijadala mbali mbali ya kuijenga Tanga pamoja na watu wake. Nini kifanyike, na nani aambiwe! Unganga na watanga wenzako katika kuipigania Tanga. Kujiunga BONYEZA HAPA au kujiunga na GROUP ya MARAFIKI WA TANGA pia BONYEZA HAPA hakikisha umeifungua facebook yako wakati wa kujiunga.