BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, May 28, 2009

MR. PAUL AZIDI KUNG'AA NCHINI AUSTRALIA!!


Ikiwa ni muda sasa tangu atimkie nchini Australia ambako ameweka makazi kwa sasa,msanii wa miondoko ya RnB & Zouk....Paul Mbena a.k.a Mr Paul amerudi kwenye mapambano ya muziki kama alivyoahidi siku kadhaa zilizopita.

Paul ambaye yuko ktk jiji la Melbourne,tayari ameshakamilisha nyimbo mbili alizozitaja kuwa 'Nakutamani' na 'Malaika wa Moyo wangu' zilizo kwenye mahadhi ya Afro Funk, na kudai kuwa track hizo ndizo zitakuwepo kwenye mradi uitwao 'Multicultural Art Victoria Visible CD', mradi ambao unajumuisha wanamuziki wa mataifa na mitindo mbalimbali yeye akiwa kama Project Officer.

Hongera kaka!

Tuesday, May 26, 2009

BLACK RHINO AZIDI KUFUNIKA CHANNEL O

Napenda kukuhabarisha kwamba, msanii Black Rhino- mdogo wake na msanii Prof Jay. Bado anaendelea kukamata chati za juu kunako Kituo cha Televisheni cha Channel O cha Afrika Kusini kupitia video ya ngoma yake, Black Chata

Monday, May 25, 2009

MALTA GUINNESS STREET DANCE 2009 YATUA TANGA!!


Haya tena wakazi wa jiji la Tanga na vitongoji vyake- hatimae yale mashindano ya kuwasaka vijana wenye vipaji vya kucheza mitaani imetia timu jijini hapa.

Usahili unatarajiwa kufanyika terehe 6/6/2009 katika ukumbi wa Tanga Hotel maeneo ya Chumbageni. Ukifika tu mahala hapo utakutana na muwakilishi wa Malta Guinnes na atakupa fomu ya ushiriki.



Lakini pia washiriki wote wanaotaka kushiriki mashindano haya ya Ku'shake...watatakiwa kufika kwenye ukumbi wa Tanga Hotel tarehe 4/6/2009 kuanzia muda wa saa nane mchana kabla ya mashindani, hii ikiwa ni kwa ajili ya semina fupi itakayotolewa kuhusiana na mashindano hayo.

Kiingilio ni Malta Guinnes mbili tu, kama wewe ni mdau wa maswala ya kucheza muziki- njoo uwape tafu vijana wenzako wa mkoani Tanga ili waweze kupata nguvu ya kutuwakilisha vyema huko waendapo.

Zaidi ni kwamba msanii wa kizai kipya ( Bongo Flava) matonya atakuwepo katika kuwasherehesha watu watakaofika hapo siku hiyo- Naamini Tanga tunaweza wadau wangu!!

Kwa maelezo zaidi gonga hapa- http://www.mgstreetdanceafrica.com/

Friday, May 22, 2009

VIDEO YA CPWAA YATINGA CHANNEL O, MTV BASE

Ikiwa ni siku chache baada ya video ya wimbo 'Black Chata' ya msanii Black Rhyno kushika nafasi ya kwanza kabisa kwenye top ten za luninga ya Chanel O,video ya wimbo Problem kutoka kwa msanii Cpwaa kwa mara ya kwanza imeanza kurushwa na kituo cha MTV Base kwenye kipindi cha Spankin New.
Ikiwa hiyo haitoshi...ktk kuonesha kuanza kukubalika kwa video za kibongo ktk anga kimataifa.....Jumamosi hii ya juzi video hiyo hiyo ilizinduliwa pia kwenye kipindi cha Channel O Cripsy Fresh.
Pia Katika kuendeleza na kuupeleka muziki wetu level za mbele “ Advanced Bongoflava” ningependa kushare na wadau wote product yangu mpya ambayo iko tayari.



MOBILE PHONE WEBSITE,ili uweze kupata habari mbalimbali za msanii CPWAA, miziki yake, uweze kudownload video, wallpapers na michezo ya simu bure! Basi tembelea tovuti yake ya simu za mkononmi na utapata huduma zote hizo.

Kwa sasa msanii C.p a.k.a CPWAA anatamba na kibao chake kipya cha PROBLEM bofya hapo ujionee video
http://www.youtube.com/watch?v=OXhqQY4QxvE .

Ukitaka kudownload wimbo huo kwenye simu yako tembelea tovuti yake ya simu . Jinsi ya kuingia kwenye tovuti hiyo: Tuma neno CPP kwenda 15551 na utapokea link itakayokupeleka kwenye tovuti hiyo. ( Hakikisha simu yako imeunganishwa na GPRS,WAP au INTERNET). Kama simu yako haina internet unaweza kupata kwa kutumiwa nyimbo hizo baada ya kujiunga na CPWAA SMS FAN CLUB kwa kutuma neno CPWAA kwenda 15551.

Ukishajiunga utakuwa unapokea nyepesi nyepesi za Cpwaa, Interview zake na show zake mahala zinapofanyika ( BUREE!), pia utapata discount ya 20% kwenye kila bidhaa za Cpwaa zitakazouzwa kuanzia saba saba. Also:

Wakae tayari kwa super dupa website http://www.cpwaa.co.tz/ to be launched Soooon!!!

Wednesday, May 20, 2009

WEMA SEPETU AJIRUDI KWA KANUMBA


Hivi juzi kwenye kipindi cha Bongo Movies kinachorushwa na kituo kimoja cha televisheni cha Chennel Ten, palikuwepo na mahojiano ya kati ya wasanii wasili ambao ni vinara kwenye Tasnia ya Filamu nchini Tanzania- Wema Sepetu na Steven Kanumba kuhusiana na Saga lao la kufikishana mahakamani.
Katika mahojiano hayho ambayo kwa namna moja ama nyengine yalikuwa ya kufurahisha kama sio kuburudisha, baada ya wasanii hao kuonekana kukwama kwama kwenye maelezo yao juu ya mustakabali mzima kwenye sanaa ya filamu.

Wema alinikuliwa akikiri kuwa, kweli hakuwa anajitambua wakati akifanya tukio la kuvunja kioo cha gari la Kanumba hivyo anaomba msamaha kwa tukio hilo. Pia mlimwende huyo wa Tanzania kwa mwaka 2006 alisema kuwa, kwa sasa ugomvi wao na Kanumba umekwisha na yupo tayari kuendelea kufanya nae kazi.

Cha kushangaza, kanumba likanusha kauli za Wema baada ya kusema hadi sasa mambo kati yao si shwari- na kuhsu kuendelea kufanya kazi za filamu msanii huyo amesema kuwa ni mapema sana kuzungumzia hilo au ni mapema sana kwa sasa kushiriki movie moja na Wema kutokana kwamba bado hakijaeleweka kati yao.

Hivi kuna nini kati yao hawa watu..? Lakini zaidi ya hapo msanii mwengine ambaye pia ni kinara kwenye Tasnia ya Filamu Tanzania maarufu kama JB alisema kuwa, wamekuwa wakipigana kufa na kupona kuhakikisha wasanii hao wanaelewana na ushirikiano wao katika filamu uendelee kama kawaida.



Saturday, May 16, 2009

NI RACHEL MLAKI MISS TANGA CITY CENTER 2009.


Mshiriki namba nne, Rachel Mlaki akiwa kwenye tabasamu pana baada ya kuvikwa taji la Miss Tanga City Center 2009

Rachel Malki akiwa mshindi wa pili wa Miss Tanga City Center 2009 Ester Flavian, na mshindi wa tatu Martha Moses


Hongera Rachel Mlaki

Mamiss wote walikuwa bomba, ila palikuwa hapatoshi hadi akapatikana mmoja


Hii ndio ilikuwa tano bora ya Miss Tanga City Center 2009. Washindi wote hawa wamepata nafasi ya kushiriki Miss Tanga 2009, ambayo itafanyika June 6 kwenye uwanja wa Mkwakwani


Mkurugenzi wa Five Brothers Entertainment, Nasa Makao akiwa jukwaani tayari kumtangza mnyange wa Miss Tanga City Center.
Moja kati ya Penel of Judges, Asma Makao na Nasa Makao- wakifuatilia kwa makini mtanange wa Miss Tanga City Center ili kuweza kutoka kitu kamili
Hawa ndio washiriki wote wa Miss Central Tanga City Center 2009

Msanii Roma, mzee wa Tanzania alipiga bonge la show

Roma akilishambulia jukwaa ipasavyo

Msanii Hemed a.k.a PHD kutoka Tusker Project Fame aliwakilisha vya kutosha

Hemed akiwa mzigoni

From now where!! Msanii Cassim aliyewahi kutanba na wimbo wake wa AWENA na e alitia timu. Kikubwa ni kwamba aliwasabahi tu wakazi wa jiji la Tanga.

Cassim akiwa na mmoja wa MC aliyesherehesha vizuri Miss Central- anaitwa Antonio Nuga

Antonio Nuga, Hemed pamoja na Cassim. Nyuma ya pazia

Bra-A kutoka Redio Mwambao Fm, mmoja wa washereheshaji wa Miss Central akiwa na mnyange wa kitongoji hicho 2009 Rachel Mlaki


Panel of Dj's kutoka Redio Mwambao Fm- aliyevaa fulana nyekundu ni Dj Rogger Kiss, akifuatiwa na DjBob Nass pamoja na Dj Don Chill. Kwa pamoja wakiwa makini katika kufanya Mixing.

Wana Mwambao Fm walikuwepo katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, baada ya kuwa mdhamini mkuu wa mashindanio hayo. Wa lwanza ni Mkali Lupa, Moshen, anty Moza, Leila totii pamoja na Blandina Lukindo.

Mkurugenzi wa Redio Mwambao Fm Tanga, Ahmed Simba akifuatilia kwa makini mashindano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Swimming Club maeneo ya Raskazoni.


Fatuma Makoko na Zena, kwa pamoja ndio wanaunda ZEFA Promotion, ambayo ndio imeandaa Miss Tanga City Center 2009- mashindano hayo pia yalidhaminiwa na Mwambao Fm sauti ya Tanga. Ambako Rachel Malaki ameibuka na mshindi, lakini pia washindi wengine wanne wamepata fursa ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka Miss tanga 2009 inayotarajiwa kufanyika June 6 kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa chini ya FIVE BROTHERS ENTERTAINMENT

AY APATA SHAVU LA KUWA BALOZI WA MALTA GUNNIES

Msanii wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Ambwene Yesayah maarufu kama Y.A. Amepata shavu la kuwa balozi wa Malta Gunnies Afrika Mashariki. Msanii huyo sasa anaungana na mabalozi wengine waliochaguliwa kutokea nchini Uganda na Kenya.



Wednesday, May 13, 2009

MFAHAMU DJ RACH KUTY WA LA CASA CHICA

Anaitwa Rafael Chambo, maarufu kama Dj Rach Kuty. Ndie Dj wa Club La Casa Chica na Redio Mwambao Fm ya jijini Tanga. Ukitaka kumpata lwenye redio na kusikiliza ladha zake, fungulia 106.0 kila siku ya jumamosi kwenye Jazz Time. Vile vile utampata kwenye kipindi cha Nyumba Ya Mwafrika kila siku kuanzia saa kumi jioni hadi saa kumi na mbili kamili jioni.

Friday, May 8, 2009

NAS, KELIS WATEMANA KIAINA!!

Habari zilizokuwa zikielezwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu harakati za kutengana kwa wanandoa Nas na Kelis takribani kwa mwezi mzima uliopita leo zimethibishwa na msemaji wa Kelis
"Nina thibisha kuwa Kelis ameshasign hati za kuachana na Nas" alieleza wakili Laura Wasser ambaye pia amewahi kuwa wakili wa Britney Spears, Angelina Jolie na Steve Wonder.
Wakili huyu alijaza hati hizo kwa niaba ya Kelis akieleza kuwa ni kwa sababu zisizorekebishika wasanii hao wameamua kila mmoja kula hamsini zake.
Hata hivyo Kelis kwa sasa anaujauzito wa takribani miezi 7 akitarajia mtoto wakiume. Baadhi ya wapenzi na mashabiki wa nyota hao wamesikitika huku wakibaki kusema huenda Nas hana bahati na warembo.

Thursday, May 7, 2009

AY NDANI YA MITAA YA ADDIS ABABA

Msanii kutokoa nchini Tanzania, Ambwene Yesayah akiwa na Mr Fix huko nchini Ethiopia mjini Addis Ababa ambako msanii huyo alikwenda kufanya show kwenye Tamasha la Selam lililofanyika nchini humo hivi juzi.

AY na Mr Fix waki'Show Love wa wadau wa muziki nchini Ethiopia pamoja na wadau wa Blog hii.


ALI KIBA AZIDI KU'SHINE NCHINI ITALY!!


Msanii wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Ali Kiba akiwa amepoz na wadau wa muziki huo huko nchini Italia muda mfupi kabla hajapanda jukwaa kuwapa burudani watu hao.

Hapa akiwa ametulia na mashabiki wake, moja ya wadau ambao wamesababisho ujio wake nchini Itilia

Ali Kiba akijaribu kuwaelewesha jambo baadhi ya waandaji wa show yake ambayo kwa hakika ilifana kwa kiasi kikubwa.

Wapenzi wa mwanamuziki Ali Kiba wakijidai, wakati msanii huyo akiwa jukwaaani akifanya show.

Monday, May 4, 2009

HATIMAE MJOMBA HADHARANI!!!

Hatimae ile albamu iliyokuwa ikusubiriwa kwa hamu, ya msanii mwenye maneno makali na yenye kuvuta hisia za watu wengi Mrisho Mpoto imetoka. kamata nakala yako chap chap ili uweze kujifunza kile usichokijua kupitia msanaa ya muziki.