BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, May 31, 2010

MATANGAZO YA MISS PANGANI YAWA KIVUTIO!!!

Matangazo ya Miss Pangani 2010 yamekuwa kivutio kila kona ya mji huu wa kihistoria. Hii nilikutana nayo katika eneo la Ferry, karibu na ofisi za Halmashauri. Miss Pangani inatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 4 kwenye ukumbi wa Safari Lodge Annex. Sikiliza tangazo lake hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!

Hapa ni eneo la stendi ya magari yanayotokea Tanga. Kila kona ya jiji mazungumzo ni Miss Pangani...hii sio ya kukosa mdau!!

Tangazo hili nilikutana nalo kwenye ofisi za Pangani Coast Cultural Tourism Programme.

Hili nililikuta mtaani....Miss Pangani 2010 inaletwa kwenu kwa udhamini mkuwa wa Mwekasu Hostel, African Design, Sofia Production, Aljazira, Salome Hair Dressing Sallon, Amazon Hair Dressing Saloon, Pangani Coast Cultural Tourism Programme, Safari Lodge Annex, River View Inn, Breeze Fm Radio, pamoja na Voda Com Tanzania.

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE WILAYANI PANGANI MKOANI TANGA!

Akiwasili kwenye hoteli ya Sea Side iliyopo maeneo ya funguni wilayani Pangani.

Mama Zippora Pangani ambaye ni mkuu wa wilaya ya Pangani akimtambulisha Mama Salma Kikwete kwa wenyeji wake.

Mkuu wa mkoa wa Tanga meja jenerali mstaafu Saidi Saidi Kalembo aliyevaa suti, akiwa na mgeni wake punde tu alipowasili hotelini hapo kwa ajili kuzungumza na wananchi wa Pangani pamoja na umoja wa kinamama wilayani hapa UWT!

Akikabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa umoja wa kinamama wilayani Pangani.

Akitazama kazi mbalimbali zinazofanywa na akina mama wa Pangani.

Sanaa haikuwa nyuma.

Akiteremka kwenye kivuko kutokea kijiji cha Mwera alipokwenda kutoa msaada kwenye vituo cha afya

Kisha akawaaga wananchi wa Pangani. Karibu tena mama! Ujio wako ulikuwa mzuri na kweli wananchi walinufaika kwa msaada wako.

Sunday, May 30, 2010

WITNESS JUSTINE NDIO MISS NGAMIANI 2010!!

Mnyange wa Miss Ngamiani 2010 Witness Justine akiwa katika uso wa furaha punde tu baada ya kutangazwa mshindi wa kitongoji chicho. Mshindi wa pili alikuwa Asha Thabit huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Tabu Mrisho. Kitongoji cha Miss Ngamiani 2010 kiliandaliwa na kituo cha redio Breeze Fm kilichopo jijini Tanga.

Ilikuwa mashamsham baada ya Witness kutangazwa kuwa mshindi, mashabiki wake walishindwa kujizuia.

Mapaparazi nao hawakuwa nyuma.

Nilipenda hii- Baba na Mama Witeness walikuja kumpa pongezi mtoto wao.

Baba akionyesha 'dole' ishara kwamba mwanangu ndio kiboko yao!!

Oooohh baba! baaaba baba, babaaaaaa! Baba huyo, babaaaaa babaaaaa huyo babaaaa, baba huyo babaaaaaaaaaa!! Safi sana baba

Mkurugenzi wa 5 Brothers Entertainment Nasoro Makau akiwa juu ya stage, tayari kumtangaza mshidni wa Miss Ngamiani. 5 Brothers ndio inandaa Miss Tanga 2010, ambayo itafanyika tarehe 19/06/2010 kunako hoteli ya Tanga Beach Resort.

Alipotaja mshindi wa tano, wanne na watatu! Wakabakia hawa....ilikuwa presha inapanda na kushuka!!

Hapa ilikuwa presha juuuuuuuuuu!!!

Hii ndio ilikuwa Tano Bora ya Miss Ngamiani 2010.

Burudani kibao zilikuwepo...ngoma za asili hiyo!

Jamaa alipoiga bonge la show!

Mtangazaji wa redio Breeze Fm anaitwa Fabby- ndio alikuwa Mc wa shughuli nzima.

Kundi la TMC ambalo linazidi kupanda chati jijini Tanga likitoa burudani...jamani, hawa jamaa wanaimba ile mbaya! sikiliza wimbo wao wa 'Tuna Bang Zaidi Yao' hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!

Man Sasha wa kundi la TMC akiwa kazini.

Dogo pamoja na Dokta Leader wote wa TMC....

Yassir 'Yeyo' akiwa na Dj wa Breeze Fm Dj Bob Nass

Lunza, Amina ambaye alikuwa mwalimu wa warembo pamoja na Fabi- nyhuma ya stage wakiweka mambo sawa.

Hawa ndio walimu wa warembo....mwalimu Lunza pamoja na mwalimu Amina. Amina pia ndio mwalimu wa warembo wa Miss Pangani 2010 ambayo inaandaliwa na Anko Mo Blogspot. Miss Pangani itafanyika siku ya ijumaa ya terehe 4 kwenye ukumbi wa Safari Lodge Annex.

Amina katika pozzz!!!

Warembo wakiwa katika vazi la asili ambalo walifanyia show ya ufunguzi.

Mdau pamoja na Dj Bob Nass.

Palikuwa hapatoshi...watu wakifuatilia mchakato. Ilifanyika katika uwanja wa Mkwakwani VIP.

Raha Tupu!!!!

Monday, May 24, 2010

'NILIWAZE'- NGOMA YA UKWELI KUTOKA KWA KHALEED

'Niliwaze" ngoma ya ukweli kutoka kwa Khaleed, msanii kutokea Tanga City anayefanya vizuri kunako game ya muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania.

Khaleed amewahi kutamba na nyimbo kama 'Nimpendae' aliofanya na Matonya pamoja na 'Tanga Town' aliofanya na Mr Ebbo.

Sikiliza 'NILIWAZE' ya Khaleed hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!




TANGAMANO- UWANJA MAAFURU KWA MATUKIO JIJINI TANGA!

Wananchi wa jijini Tanga wakiwa katika uwanja wa Tangamano wakifuatilia tukio.

Akinamama wakijimwaga Tangamano.

Hii kali jamani!!

Tangamano pia ni maarufu kwa biashara (Soko Huria)

Haya sasa, waliosema Tanga kunani hawakukosea!

Thursday, May 20, 2010

TIP TOP INATAFUTA WAREMBO KWA AJILI YA VIDEO YAO MPYA!!

Kundi maarufu Tanzania kwenye anga za muziki wa bongo flava Tip Top Connection linatarajia kufanya video wa wimbo wao mpya unaitwa 'Bado Tunapanda' uliotengenezwa pale Mj Record chini ya producer Markochali.

Akizungumza na VIJIMAMBO VYA TANGA meneja wa kundi hilo Babu Tale amesema kuwa ili kukamilika kwa video hiyo anahitaji warembo watakaopamba katika baadhi ya matukio.

Tale ameongeza kuwa, video hiyo itafanyika siku ya jumapili pale Kunduchi Beach na warembo watapata nafasi ya ku'shine kunako video hiyo itakayotengenezwa na gwiji la kutengeneza video bora nchini Tanzania Adam Juma.

'Bado Tunapanda' umetiwa sauti na wasanii wote wakubwa wa kundi la Tip Top ikiwa ni pamoja na Keisher, Kassim, Tunda Man, na Madee.

Je wewe ni mrembo na unahisi unaweza kuuza sura kwenye video za wasanii wakubwa!!!?? piga namba hii 0652116576

Wednesday, May 19, 2010

ZULEA MRISHO NDIO MISS USAGARA 2010!

Mchakato wa kutafuta warembo wa miss vitongoji ambao wataingia moja kwa moja kunako mashindano ya Miss Tanga 2010 unazidi kupamba moto jijini Tanga, ambapo hivi juzi mwanadada Zuleo Mrisho alifanikiwa kuibuka mnyange wa kitongoji cha Miss Usagara.

Shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Two Sisters na kufanyika kwenye ukimbi wa Splendid- lilikuwa na ushindani mkubwa kiasi cha majaji kumchagua Amina Twaha kuwa mshindi wa pili na Sabrina Rajab kuwa mshindi wa tatu.

Washindi wote hao wamepata nafasi ya kuingia kwenye kambi ya Miss Tanga ambayo kilele chake ni mapema mwezi ujao pale Tanga Beach Resort maeneo ya Sahare.

Tuesday, May 18, 2010

NGOMA MPYA YA TIZZLE- KUTOKA TANGA MPAKA LONDON!!

(Tizzle na Damuz)

Msanii kutokea jijini Tanga anayejulikana kwa jina la Tizzle ambaye hivi sasa anaishi nchini Uingereza kuonako jiji la London, amechia ngoma yake mpya inayoitwa 'Nameless' aliyomshirikisha Damuz.

Akiongea na Blog hii moja kwa moja kutokea Uingereza, Tizzle amesema kuwa ngoma hiyo ameifanya pale studio za East London kwenye studio moja inaitwa Mzuka Entertainment Rec chini ya producer Josh.

Tizzle aliongeza kuwa, anaamini ngoma hiyo itamuweka pazuri kunako ramani ya Bongo Flava na duniani kwa ujumla kwa kuwa ina kiwango cha kimataifa. Sikiliza wimbo huo hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Song: NamelesS, Artist: Tizzle feat Damuz

Msanii huyo ambaye kabla ya kwenda Uingereza alikuwa anaishi pale Majani Mapana na baadae kuhamia Bara Bara ya 15, kwa sasa yupo anajipanga kutoka na ngoma nyingine ya 'Hisia Zangu' ambayo atawashirikisha washkaji zake damuz, josh pamoja na danny.

Mpango wa albamu unakuja na ataipa jina punde tu itakapokamilika.



MITAA YA TANGA CITY LEO ASUBUHI!!!