
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa kutoka wizara ya Afya anayeshughulikia masuala ya Habari na Ukimwi, Benard Fimbo alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kutoa elimu kwa vijana juu ya kujiepusha na ngono ambazo zinaweza kuwasababishia kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa waandaaji wa tamasha hilo Deo Mwanansabi alisema kuwa mbali ya Banana kutoa burudani kwenye tamasha hilo pia kutakuwa na wanamuziki wengine wa hapa nchini.
Aliwataja wanamuziki hao kuwa ni Enika, bendi kongwe ya muziki wa dansi ya Mlimani Park na bendi ya Wahapahapa.
No comments:
Post a Comment