BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, May 30, 2011

IFAHAMU TANZANIA OPEN FILM FESTIVAL!



Tanzania open film festival is a commitment to film presentation as a way to examine, reflect, and celebrate diversity, while challenging existing stereotypes, and facilitating cultural dialogue.

A number of Bongo filmmakers are in attendance each year to talk to audiences about their work and the screenings are accompanied by a variety of complementary events such as discussions, master classes, seminars and music events.

Bongo Filmmakers and Movie stars travel with their films to present their work, engage in question and answer sessions, meaningful one-on-one discussions, panels, master classes, and workshops.


(Tanzania Open Film Festival Powered by Grand Malt..!)


Films are showcased in an open space called Tangamano. Filmmakers connect with audiences and open doors to new ideas, stories, and perspectives.


Tanzania Open Film Festival is also a meeting point for audiences with eager for enjoyment and specifically for sponsor marketing ground, to come together and celebrate, the ideal place for doing business, marketing product and making contacts.


Location: Our Offices are located at 62, Mwinyijuma Road, Kinondoni, Mwananyamala Dar es Salaam and FourWays, Tanga, P.O.Box 173 Dar es Salaam, Tanzania





Phone: 0719 221 333

Wednesday, May 25, 2011

THE BEAT FESTIVAL

THE BEAT FESTIVAL27.05.11 - 20.00 -00.00venue: Triniti - Msasani rd. 26, Oysterbay DSM

JHIKOMAN - Roots Reggae www.jhikoman.com
MZUNGU KICHAA - Reggae/World www.myspace.com/mzungukichaa
FID Q - conscious HIPHOP www.facebook.com/fidhop
BONGO BEAT - festival backing band


The Beat is a monthly festival (usually on the last friday of the month) showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is hosted by Mzungu Kichaa and features some of the best local and international talent passing through Tanzania.


Triniti (www.triniti.co.tz) provides a relaxed ambience to enjoy good music taking you far away from the cities hustle and bustle, and yet it is still very central. Entrance is only 5k at the door.
Please join this page and hit the like button.
www.facebook.com/TheBeatFestival
powered by CARAVAN RECORDS. www.myspace.com/caravanrec

Tuesday, May 24, 2011

ANKO MO USO KWA USO NA MBUNGE WA PANGANI!

Mimi (Anko Mo) niliyevaa fulana nyeupe nikiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa jimbo la Pangani Mh. Salehe Pamba tulipokutana hivi karibuni katika moja ya shughuli zake wilayani Pangani. Aliyevaa fulana ya manjano ni Mr Leopard, na wadau wengine.


Harakati zinaendelea!


Monday, May 23, 2011

WAREMBO MISS TANGA 2011 WAINGIA KAMBINI!

Warembo wa Miss Tanga 2011 wameingia kambi rasmi siku ya jana katika hoteli ya Raskazoni kwa ajili ya kujiweka sawa na shindano hilo linalotarajiwa kufanyika June 11 katika hoteli ya Mkonge jijini hapa. Kampuni inayoratibu mashindano hayo New Face Entertainment imesema kuwa, warembo hao watapiga kambi hapo kwa muda wa siku 20 ili kujipanga vema.

Warembo wa Miss Tanga punde waliposhuka kutoka kwenye gari lililowaleta kunako Raskazoni Hoteli.

Warembo wa Miss tanga 2011

Kampuni ya Sofia Production ilikuwepo kuhakikisha kumbukumbu inatunzwa. hapa kijana Juma akiwa kazini.

Anaitwa Mamy.....alikuwa akiwahoji watu mbali mbali waliofika Raskazoni Hoteli...

Anaitwa Maximilan Luhanga, ndie mratibu wa Miss Tanga 2011 kupitia kampuni yake ya New face Entertainment.

Hapa akifanya mahojiano na mmoja wa waandishi wa habari kutoka Tanga Televisheni.

Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Bingwa, anaitwa Oscar Assenga nae alikuwepo.

ASANTE HABARI LEO KWA KUNIONA!

Siku ya ijumaa ya tarehe 20/05/2011 nilipamba kurasa kupitia gazeti la Habari Leo linalotoka kila siku. Humo mwandishi aliandika mambo mengi sana kuhusu mimi. Maisha yangu pamoja na uwezo wangu katika utunzi wa hadithi ambao nimerithi kutoka kwa marehemu baba yangu Hammie Rajab. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru gazeti la Habari Leo pamoja na mwandishi Beda Msimbe kwa kazi nzuri mliyoifanya.



Thursday, May 19, 2011

KWA NINI MASHINDANO YA UREMBO TANGA YANAPOTEZA MVUTO..!!??

(Miss Tanga 2010 Anna Kiwambo, nafasi ya pili ni Jally Murei, wa tatu ni Zuleha Mrisho)

Hivi karibuni mashindo ya kumsaka mnyange wa Miss Tanzania 2011 yalizinduliwa rasmi katika hoteli ya kimataifa ya Kilimanjaro Kempnsiky. Haya ni moja kati ya mashindano maarufu sana hapa nchini ambayo huanzia katika ngazi za vitongoji, mikoa hadi kanda.

Chini ya uratibu wa kampuni ya Lino Agency na udhamini mnono wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, mashindano haya yamekuwa yakipata msisimko na kuzidi kuwa maarufu hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency Limited Bwana Hashim Lundenga, moja ya madhumuni ya mashindano hayo ni kuwakutanisha wasichana kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania , kujuana, kujenga urafiki na kujifunza mambo mbalimbali kutoka sehemu walizotoka. Zaidi pia kuitangaza nchi kimataifa.

Tangu mashindano haya yaliporejea mwaka 1994, kumekuwa na mafanikio mbalimbali, ikiwemo kukua kwa fani ya urembo, kuongezeka kwa ushiriki wa wasichana, kuongezeka kwa uelewa wa wananchi juu ya mashindano hayo pamoja na kutoa ajira kwa warembo mbalimbali.

Katika anga za kimataifa pia kumekuwa na mafanikio ya ushiriki wa kila mwaka katika mashindano ya mkumsaka mrembo wa dunia, kutangaza utalii na vivutio vya Tanzania , lakini pia mafanikio ya kushika nafasi nzuri katika mashindano ya dunia.

Mnyange Hoyce Temu, aliingia katika kumi bora mwaka 1999, huku Nancy Abraham Sumari akishinda taji la mrembo wa dunia kanda ya Afrika mwaka 2005, wakati alipoingia kwenye hatua ya fainali ya mashindano ya dunia na kushika nafasi ya tano katika mashindano ya mwaka huo. Hata hivyo historia hiyo haijavunjwa mpaka leo, ambapo mrembo wa mwaka 2010 Genevieve Emmanuel ndie anayeshikilia taji hilo kwa sasa na atamaliza muda wake hivi karibuni.


(Miss Tanga 2009 Glory Chuwa akiwa katika pozz pamoja na Rechal Mlaki namba mbili na Yasmini Zachari namba tatu.)


Wakati mashindao haya yakiendelea kupata umaarufu mkubwa hapa nchini kwa kuwa na msisimko na ushindani kuanzia katika ngazi za vitongoji, mkoani Tanga mambo yamekuwa yakibadilika ambapo mashindano hayo yanaanza kupoteza mvuto na hadhi yake.

Ili kupatikana mrembo wa Tanga atakayeuwakilisha mkoa kwenye mashindano ya Taifa au kanda mchakato huanzia kwenye vitongoji kama ilivyo kawaida katika sehemu zingine.

Vitongoji ambavyo vipo na tayari vimewahi kupeleka warembo kunako kambi ya Miss Tanga ni vya wilaya za Lushoto, Handeni, Pangani na Korogwe ambayo imeanza mwaka huu.

Kwa upande wa Tanga mjini vitongoji nguli ambavyo vimekuwa vikitoa warembo kupeleka kambi ya Miss Tanga ni Chumbageni, Ngamiani, Usagara, College pamoja na kitongoji cha Kati, yaani Tanga City Central.

Wakati ikionekana kwamba utamaduni wa watu wa Tanga unazorotesha mashindano hayo, kiasi cha kuyafanya kukosa msisimko katika miaka ya awali, kampuni ya Five Brothers Entertainment iliyokuwa ikiratibu mashindano ya vitongoji ilipewa jukumu la kuratibu mashindano ya urembo ya mkoa wa Tanga mwaka 2007 ambapo ilifanya mapinduzi mkubwa katika mashindano hayo mkoani hapa.

Kampuni hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wake bwana Nassoro Makau ilifanikiwa kurejesha heshima na msisimko katika mashindano hayo mkoani hapa, ambapo moja ya mafanikio ya haraka ni kuweza kutoa mrembo aliyeshika nafasi za juu katika mashindano ya taifa. Naye ni Victoria Martin, aliyekuwa Miss Tanga. alishika nafasi ya nne katika mashindano ya Miss Tanzania 2007.

Licha ya hivyo, pia Victoria alichaguliwa kuwa Balozi wa kinywaji cha Redds yaani Miss Redds, na baadaye kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya mrembo wa Afrika Mashariki mwaka 2009. Kwa sasa mwanadada huyu ni mwanamitindo.

Kabla ya Five Brothers mwaka 2007, kulikuwa na kampuni nyengine pia ziliwahi kuandaa mashindano ya Miss Tanga. Moja ya kampuni hizo ni Boy George Entertanment. Hii iliweza kutoa mwanga wa kutosha na kufanya watu wa Tanga wathamini mashindano haya.

Tangu alipofanya vizuri Victoria hadi sasa mkoa wa Tanga umekuwa ukihangaika kuifikia historia hiyo au kuivunja rekodi ya kutoa mnyange wa Tanzania miaka ya nyuma zaidi ya mwaka 2007. Lakini mkoa wa Tanga haukufurukuta sana . Lakini pia baada ya Victoria mkoa huu umeendelea kususua kwenye fani hiyo.


(Jally Murei ni Miss Tanga namba mbili aliyeuwakilisha mkoa mwaka 2010)

Pengine kumekuwa na tatizo ambalo ama linachangiwa na uratibu au kwa namna warembo wanavyochaguliwa. Kwa mfano mwaka 2009 na 2010 warembo waliochaguliwa na majaji walioitwa “mahiri”, hawakufanya vizuri kabisa kwenye mashindano ya kanda na hata taifa.

Miss Tanga 2010 Anna Kiwambo aliyechaguliwa na majaji
wenye ubora, hakuweza kufurukuta kwenye mashindano ya Kanda Kaskazini, na badala yake mshindi namba mbili kutoka Tanga Jally Murrei aliitoa Tanga kimasomaso kwa kushika nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo na kwenda kuiwakilisha Tanga kwenye mashindano ya Miss Tanzania ni moja ya mambo yanayozua utata juu ya namna ya uchaguaji warembo.

Bada ya malamiko na mambo mengine kutoka kwa wadau mwaka huu mashindano hayo ya Miss Tanga yanaratibiwa na kampuni ya New Face Entertainment ambayo awali ilikuwa ikiandaa mashindano ya kitongoji cha Miss College . Haijulikanani ni kwa nini kampuni ya Five Brothers Entertainment imeachia ngazi. Hakukuwa na taarifa rasmi iliyotolewa zaidi ya minong’ono ya hapa na pale.

Ushauri wangu ni kuwa hali hii inaleta ukakasi kidogo, kwani pamoja na mashindano hayo kuonekana kupwaya kwa kiasi kikubwa jijini hapa, lakini pia waandaji wamesahau kuwa wanapotumia jina la MISS TANGA ni Tanga ile ile yenye wilaya 8, tarafa 37, kata 136 na vijiji 557. Hivyo isionekane ni mashindano ya mtu binafsi ama vinginevyo.

Pengine maslahi ni jambo ambalo linawekwa mbele sana kwa waandaji wa mashindano haya, na pengine maslahi hayo hayo ndio yanafanya Tanga iwe inatoa warembo wasio na sifa kila mwaka. Sio kweli kwamba Tanga haiwezi kutoa Miss Tanzania , siamini hilo ! Kama iliweza pia kutwaa nafasi ya tatu mwaka 1996 kupitia mrembo Mona Koja, kwanini basi leo isiweze kupiga hatua zaidi?

Imani yangu ni kuwa sifa za mabinti wa Tanga bado zipo pale pale, ukarimu wao, lugha yao laini, ufundi wao katika mapishi na hata urembo pia. Tanga ina sifa nzuri sana midomoni mwa Watanzania wengi, lakini wengi wamekuwa wakijiuliza swali kama nililojiuliza mimi. Kwanini Tanga haijawaji kutoa Miss Tanzania .

Kwa mfano, katika mashindano ya kitongoji cha Tanga City Central yaliyofanyika hivi karibuni yaliyoandaliwa na kampuni ya Green Apple Entertainment ni ushahidi tosha kuwa mashindano haya ya urembo yamepoteza mvuto mkubwa hapa Tanga kwa idadi ndogo ya watu waliohudhuria siku hiyo. Ilikuwa aibu ya mwaka. Hapo kabla kitongoji hicho hakikuwa hivyo. Naweza kusema ni moja ya kitongoji kinachofanya vizuri sana kwani ndicho kilichomtoa Rachel Mlaki 2009.

Majaji wa Miss Tanga 2009 walimpa nafasi ya pili kwenye mchakato huo. Cha kufurahisha mwaka uliofuata akiwa chuoni dodoma alitwaa taji la Miss Udom na kufanikiwa kuingia kambi ya Miss Tanzania . Huwa najiuliza, ni vigezo vipi wanavyotumia waandaji wa Miss Tanga katika kuwapata majaji bora wanaojua maswala ya urembo.

Lakini pia, swala kubwa lililopo hapa ni dhamana ya kampuni husika iliyopewa ili kuhakikisha mashindano hayo ya urembo yanautangaza mkoa wa Tanga kama moja ya madhumuni yaliyotajwa na waandaji wakuu wa mashindano haya nchini. Isionekane tu yapo kwa ajili ya kuitangaza nchi, bali pia yatumike kujitangaza kitaifa kwa maana ya mkoa kwa mkoa. Kwani leo anapopatikana Miss Tanga na kwenda kuuwakilisha mkoa wake, akawa Miss Tanzania sifa hivi ni za watu wa Tanga wote na sio kampuni iliyoandaa pekee.

Ombi langu kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Meja Jenerali Msataafu Saidi Saidi Kalembo ni kuwa ayatazame kwa makini mashindano haya na waandaji wake pia. Isiwe anapewa mwaliko na kuhudhuria kama mgeni rasmi pasipo kujua utaratibu mzima wa uwandaaji wa mashindano yenyewe.

Labda majukumu ya kazi yatakuwa yanambana sana , lakini anaweza pia kutuma hata wajumbe ambao baadae watampelekea ripoti. Wayatazame haya kwa makini. Kwanza , uwezo wa kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanga. Pili, kama kampuni hiyo imesajiliwa. Na tatu, kama ina kamati madhubuti inayotazama uzalendo kwanza, pamoja maslahi, ni muhimu pia.

Kwa kufanya hivi nadhani labda Tanga inaweza kutoa mnyange wa Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2011. Napenda kutoa shukrani kwa kampuni ya Five Brothers Entertainment kwani walifanya kazi nzuri ya kurudisha heshima ya mashindano haya. Pia kila la heri kampuni ya New Face Entertainment. Mchanga wa pwani huo!

Makala hii imeandikwa na..

Mohammed Hammie Rajab (Anko Mo)


Wednesday, May 18, 2011

DULLY SYKES NDANI YA TANGA CITY IJUMAA HII!

Msanii wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wake wa 'Bongo Fleva' hivi sasa Dully Sykes atakuwepo jijini Tanga ijumaa hii ya tarehe 20/05/2011 kunako club ya kisasa ya Lacasa Chica kwa kiingilio cha 5000/= najua wajanja wote wa mjini tunakutana hapo.



SIKILIZA TANGA FM RADIO KWA NJIA YA INTERNET!


Habari zenu wadau wa VIJIMAMBO VYA TANGA! katika kuboresha na kuwaweka karibu zaidi na mkoa wa Tanga, blog hii imeamua kuanzisha redio inayoitwa TANGA FM RADIO itakayokuwa inakupa habari moto moto kutokea mkoani hapa halikadhalika burudani za kukata na shoka. Uwamuzi wa kuanzisha redio hii ni katika kuboresha blog ili mpate kuhabarika zaidi.

Anza sasa kusikilia TANGA FM RADIO kupitia internet yako popote pale ulipo (dunia nzima). Kuisikiliza, tazama hapo juu upande wa kulia kisha bonyeza kwenye kitufe cha njao! Nakaribisha maoni na ushauri, piga simu +255719000010 au nitumie e-mail kupitia ankomo25@yahoo.com KARIBUNI WOTE!

Monday, May 16, 2011

DJ'S WAKALI TANGA TOWN



Dj Roger Kiss aliyevaa fulana ya kijani na nyeupe pamoja na Dj Bob Nas, wote wanatokea Breeze Fm Radio ya hapa jijini Tanga. Ni dj's wanaofanya kazi yao kwa uhakika na utaalamu wa hali ya juu.

THE MAKING OF 'KIDOLE CHA MWISHO JUU'- ROMA


Video utaona hapa hapa soon....endelea kutembelea Blog.




Wednesday, May 11, 2011

WANNE STAR KUPAMBA MISS ARUSHA CITY CENTER

MSANII mahiri wa ngoma za asili Tanzania, Salum Wanne ‘Wanne Star’, anatarajiwa kutumbuiza katika mashindano ya kumtafuta mlimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2011 yanayotarajiwa kufanyika Mei 13 katika ukumbi wa Triple A, Arusha.


Mratibu wa shindano hilo, Bi. Sophia Urio, alisema kuwa msanii huyo ataungana na kikundi cha ngoma za asili cha Kontejazz cha jijini Arusha katika kutoa burudani ambayo haitawachosha wageni waalikwa.


Mpaka sasa wamehakamilisha wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha.


"Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni siku yenyewe ambayo walimbwende watakayochunana", alisema Bi. Sophia Urio.


Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.


Aliongeza kuwa katika shindano hilo natarajiwa kuanza majira ya saa 2 usiku kiingilio chake kitakuwa ni shilingi 7,000/- kwa viti vya kawaida na shilindi 10,000/- kwa viti maalumu.


Alisema, wadhamini wamezidi kuongezeka na kuwataja kuwa ni pamoja na Vodacom, Startimes, Mbogo Experdistio, Litte Roses, Kilimanjaro Express Bus, Intelligence Security Ltd, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour, Klabu Santiago pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.


Monday, May 9, 2011

MITAA YA TANGA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA!!

























MVUA ZA MASIKA KIZAA ZAA TANGA!

Kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha jijini Tanga, tayari kumekuwa na matukio tofauti tofauti ya hatari zinazosababishwa na mvua hizo. Camera ya Anko Mo Blogspot ilinasa tukio hili la kukatika kwa nyaya za umeme kunako eneo la Mabanda Ya Papa.



Gari la Tanesco likiwa limesimama katika eneo la tukio, wakiwa tayari kwa kurekebisha nyaya za umeme zilizokatika.


Wafanyakazi wa Tanesco wakijaribu kutatua tatizo hilo huku wananchi wakitazama wakati kazi hiyo ikiendelea


Hali hiyo ya pia iliweza kusababisha foleni za hapa na pale mpaka Tanesco walipomaliza kazi yao.








Wednesday, May 4, 2011

KWA MARA YA KWANZA MKOANI TANGA! MISS KOROGWE HIYOOOO

Waandaji wa kitongoji cha Miss Korogwe 2011 wakiwa katika pozi! Kupitia kampuni yao ya Shalola Suply ndio inaileta Miss Korogwe kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano ya urembo mkoani Tanga. Mchakato wa kumsaka mnyange wa Miss Tanga 2011 umepamba moto huku kila kitongoji kikionyesha nia ya kutwaa taji hilo kubwa. Tayari kitongoji cha Tanga City Central kimeshatoa warembo wake pamoja na kitongoji cha Miss Handeni. Miss College ni tarehe 13 ya mwezi huu siku ya ijumaa na Miss Lushoto ni tarehe 21 ya mwezi huu siku ya jumamosi.

Msanii maarufu wa komedi nchini Masele akiwa katika picha ya pamoja na warembo wa kitongoji kipya cha Miss Korogwe walipokutwa na kamera ya anko mo Blogspot.

Miongoni mwa warembo hao wa Miss Korogwe, watatu ndio watapata nafasi ya kuingia kambi ya Miss Tanga 2011 ambapo kilele chake ni June 11 siku ya jumamosi pale Mkonge Hotel, imeandaliwa na New Face Entertainment.

Monday, May 2, 2011

KIGODA KUWAPIGA JEKI WALIMBWENDE WA MISS HANDENI!


MBUNGE wa jimbo la Handeni,Abdallah Kigoda ameahidi kutoa ushirikiano kwa warembo baada ya kuibuka washindi katika kitongoji cha Handeni kwenda kambi ya miss Tanga. Dr.Kigoda alitoa ahadi hiyo juzi wakati wa sherehe za mapokezi ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu CCM.

Alisema kuwa atatoa msaada kwa warembo hao ili kuwawezesha kufanya vizuri katika hatua ya kuwania kinyang'anyiro cha kumpata mrimbwende atakaye wakilisha Tanga kwa urembo.

Mjumbe huyo aliahidi kutoa fedha mara baada ya warembo hao walioshika namba ya kwanza hadi ya tatu kuimba na kukiomba chama cha Mapinduzi kuwapa sapoti katika kambi ya Miss Tanga

Alisema kuwa anatambua uwepo wa warembo hao na kwamba kushiriki mashindano hayo si tu ni moja ya ajira kwao bali pia wanaitangaza wilaya,mkoa na Taifa kwa Ujumla,

"Ni wajibu wangu na jamii kutoa msaada wa kila hali kwa warembo hawa ili waweze kufanya vizuri na kufikia malengo yao ya urembo"alisema Dr.Kigoda.

Pia alitumia nafasi hiyo kwa kuitaka jamii kuondoa mawazo potofu kuwa urembo ni uhuni badala yake waone ni moja ya michezo hapa nchini na kwamba ni ajira.

Alibainisha kuwa urembo ni ujumbe tosha wa kuitangaza wilaya na utalii wetu kupitia mashindano hayo hivyo ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunatoa ushirikiano wa kutosha kwa warembo hao.

Nae mgeni rasmi diwani wa kata ya Chanika,Mhe.Mwinshashi Uledi aliwataka warembo hao kuhakikisha wanafanya vizuri na kuzingatia nidhamu katika hatua hiyo ya miss Tanga.

Alisema hatua ambayo wameimaliza ni ndogo kwani wakifanya vibaya katika kambi ya miss Tanga ni sawa na kuitia doa wilaya ya Handeni na kwamba ameahidi kutoa ushirikiano kwa warembo hao pale watakapo kwama.

Warembo hao ni Mwajabu Juma (20) ambaye amepata redio aina ya sabufa yenye thamani ya laki mbili,Habiba Rashid (19) amezawadiwa godoro kwa kushika nafasi ya pili huku Amina Bakari (19)akipata dina seti mshindi wa tatu

Kambi hiyo inatarajiwa kuanza May 22 mwaka huu ,kwa ajili ya mashindano ya kuwatafura warembo watakaowakilisha mkoa wa Tanga katika mashindano ya Miss Tanzania yatakayofanyika hapo baadae.


Na Sophia Wakati, Handeni


KUNDI LA DANSI LA ICE CREAM KUIWAKILISHA TANGA KWENYE FIESTA 2011!

Kundi la Ice Cream likiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuibuka vinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta ndani ya ukumbi wa Club Lacasa Chica hapa jijini Tanga.

Mratibu wa mchakato wa Serengeti dansi la Fiesta 2011 Sebastian Maganga akiwahoji kundi la Ice Cream mara tu baada ya kutangazwa washindi. Kundi hilo litapata nafasi ya kushiriki kilele cha juu kabisa cha msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta jijini Dar es salaam hapo baadae.

Baadhi ya watazamaji waliojitokeza kushuhudia nani ataibuka kidedea wa dansi na Serengeti la Fiesta 2011

Majaji wakijadiliana jambo. B Dozen, Issa Kwisa pamoja na Msami kutoka THT. Kwa picha zaidi BONYEZA HAPA


Sunday, May 1, 2011

MISS COLLEGE TANGA NI TAREHE 13

Mashindano ya kumsaka mnyange wa Miss Tanga 2011 jijini Tanga yamezidi kupamba moto kila kona. Baada ya Miss Tanga City Central kuwapata wawakilishi wao kunako kambi ya Miss Tanga na sasa kitafuatia kitongoji cha Miss College ambacho mbwembwe zake zitaonekana siku ya Ijumaa ya tarehe 13. Itafanyika wapi na wasanii gani watakuwepo!!? Endelea kutembelea Blog na utajua hayo muda sio mrefu.....