BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, August 6, 2009

UFAHAMU MKOA WA TANGA, TANZANIA.


UFAHAMU MKOA WA TANGA

Mkoa wa Tanga unapatikana Kaskazini Mashariki mwa nchi ukiwa unapakana kabisa na Bahari ya Hindi. Mkoa huu ambao wenyeji wake ni watu wa makabila ya Wasambaa, Wabondei na Wadigo.

Shughuli kubwa za kiuchumi za wenyeji wa mkoa huu ni za kilimo na uvuvi ambapo shughuli za kilimo hujumuisha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, mkonge ukiongoza kama zao la biashara mkoani hapa.

Mkoa wa Tanga unayo idadi ya watu anaofikia 1,642,015 ambao hulijaza eneo la kilometa za mraba 26,808 ambazo ni sawa na maili za mraba zipatazo 10,351.
Mkoa huu unayo majimbo ya uchaguzi yanayofikia (8) ambayo yanajumuisha Kilindi, Tanga Mjini, Handeni, Lushoto, Bumbuli, Muheza, Korogwe Magharibi, Korogwe Mashariki.


MALIASILI

Misitu:
Katika Mkoa wa Tanga zipo hekta 6,000 za mashamba ya miti ya kupanda kwa ajili ya uvunaji – Shume (Lushoto) na Longuza (Wilayani Muheza).

Misitu ya Hifadhi:
Jumla ya hekta 160,795 ni misitu ya hifadhi ya vyanzo vya maji na bioanuwai iliyotengwa sehemu mbalimbali za Mkoa

Wanyamapori:
Mkoa una kilometa za mraba 5,920 kwa ajili ya mapori ya wanyama; ikiwa kati ya eneo hilo, kilometa za mraba 3,120 ni “Game Controlled Areas”.Mkoa pia unachangia katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,062. Aidha, lililokuwa pori la akiba la Umba sasa limekuwa Mbuga ya Taifa ya Wanyama (National park) baada ya kuunganishwa na Pori la Akiba la Mkomazi katika Mkoa wa Kilimanjaro




No comments:

Post a Comment