BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, September 5, 2011

HOTELI MPYA YAZINDULIWA TANGA

MMILIKI wa hoteli mpya inayojulikana kwa jina la NYUMBANI Hotel & Restaurant Bw. Aloyce Kimaro aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, amewataka wafanyabiashara na wananchi wa Jiji la Tanga, kumuunga mkono katika uwekezaji wake mpya wa sekta ya hoteli ili kusaidia kuongezeka kwa pato la uchumi la mkoa wa Tanga.

Akitoa neno la shukurani kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopo mkabala ya jengo la posta katikati ya Jiji la Tanga, mbunge huyo wa zamani alisema alipata wazo la kufungua hoeli hiyo mkoani Tanga, kushirikiana na wana-jamii kuongeza pato la mkoa hasa kutokanana uwepo wa bandari na shughuli nyingine za kiuchumi.

Alisema kutokana na uwepo wa bandari na kukua kwa shughuli nyingi za kibiashara alionelea kufungua hoteli hiyo hivyo amewataka wananchi na wafanyabiashara kushirikiana naye kumsapoti katika kuhakikisha hoteli hiyo inatoa huduma za kisasa na za kimaaifa.

Bw. Kimaro ambaye anaendesha hoteli hiyo akiwa na wakurugenzi wengine Bw. John Kessy na Mansfeld, wanatarajia kufungua hoteli zenye jina hilo katika mikoa yote nchini ili kuhakikisha wanawekeza katika sekta hiyo wakiwa kama Watazania na kusaidia kukua kwa uchumi wa Tanzania. Hoteli hiyo ya Tanga inafuatia kuwepo kwa hoteli nyingne zenye jina hilo la nyumbani katika miji ya Mwanza na Moshi.

Akizindua hoteli hiyo Waziri wa Uchukuzi, Injinia Omar Nundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Tanga, alisema katika kutembea kwake Ulaya hoteli hiyo inaingana kabisa na ambazo amezishuhudia na kwamba hoteli ya Nyumabni ni moja ya hoteli yenye hadhi kubwa mkoani Tanga na ambayo itafungua ukurasa mpya kwa wawekezaji wengine.

"Mbunge wenu mnajua nimemaliza huko Ulaya, lakini hoteli hii nilipoingai kwenye vyumba nimekuta vitu ambavyo nikiwa huko Ulaya kwenye mahoteli makubwa nimekutana na mambo makubwa mabyo yamo humu ndani, hii ni changamoto kwa wawekezaji wengine kuona umuhimu wa kuwekeza mahoteli makubwa kama haya katika Jiji letu," alisema Injinia Nundu.



Na Mashaka Mhando, Tanga

No comments:

Post a Comment