BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, June 2, 2009

TAMASHA LA FILAMU TANZANIA 2009 LAZINDULIWA TANGA


Mstahiki meya wa jiji la Tanga Salim Kisauji akiteta jambo na baadhi ya wadau wengine wa filamu mkoani hapa. Pembeni ni Aisha Kisoki au mama Sofia Production, ambao ndio wandaaji wakuu wa tamasha hilo la filamu Tanzania lililozinduliwa siku ya jana ya terehe 1/6/2009 kwenye viwanja vya Tangamano. Kisauji alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo

Kikundi cha Tumaini Arts kikitoa burudani ya ngoma aina ya Baikoko- moja ya midundo ambayo inapendwa sana na wakazi ya Tanga. Hapo dada Mwajuma akicheza ile staili ya "VIBRATION"




Kikundi chengine cha Channel O kutoka hapa hapa jijini Tanga, kikipagawisha na Baikoko ya nguvu.

Wakazi wa Tanga wakipata burudani ya kipekee siku ya jana wakati tamasha hilo lilipofunguliwa rasmi.

Hapa mwanzo mwisho- mashabiki na wadau wa filamu jijini Tanga wakifuatilia Tamasha.

Baadhi ya mitaa ya jijini Tanga

Walimbwende wa Miss tanga 2009 pia walipewa mwaliko


Miss tanga 2008, Nadya Ahmed aliwakilisha vya kutosha kwenye tamasha la filamu


Mkurugenzi wa Sofia Production, Musa Kisoki ambaye kampuni yake ndio imedhamini tamasha la filamu Tanzania kwa mwaka huu- akifungua ramsi tamasha hilo.


Kudadeki!! Wakurugenzi wamekutana- mkurugenzi wa Five Brothers Entertainment Nasa Makao akiteta jambo na mkurugenzi wa Sofia Production Musa Kisoki

Crew ya Sofia Production ikiwa makini kwenye mitambo. Tamasha hilo la filamu mkoani Tanga limezinduliwa siku ya jana, na kilele chake ni siku ya Jumanne ya tarehe 9/6/2009 wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment