BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, June 2, 2009

MISS TANGA TALENT 2009- WAREMBO KUMI WAPATA NAFASI


Logo ya Five Brthers Entertainment- ambao ndio wandaaji wa kubwa wa shindano la kumsaka Miss Tanga 2009 ambalo linatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 6/6/2009 kwenye uwanja wa Mkwakwani kwa kiingilio cha 5000/= viti vya kawaida na 15000/= viti maalumu yaani VIP hii ikiwa ni mpamoja na chakula cha jioni.
Mkurugenzi wa Five Brothers akiwa na majaji wengine Mr. Ebo ambaye ni msanii na pia ni Producer kutoka Motila Records ya jini Tanga pamoja na mzee Mtambo katika mchakato wa kuwatafuta warembo kumi kati ya ishirini ambao watatakiwa kushindania taji la Miss Talent Jumamosi
.


Baadhi ya warembo wakiwa makini kufuatilia burudani tofauti zilizokuwa zikiendelea kwenye ukumbi wa Club La Casa Chica katika mchakato wa Miss Tanga Talent 2009

Antonio Nugas kutoka Clouds Fm, alikuwepo. Mtu mzima akiwa kwenye ngazi za kuelekea juu- kunako Club La Casa Chica!! Pembeni sijui ndio shemeji au vipi kaka...Aah poa tu mwana!!!

Miss Tanga 2008 ambaye anamaliza muda wake Nadya Ahmed, akiwaeka pozi- kwenye korido za la Casa Chica. Mkononi akiwa ameshikilia bilauli ya wine


Usifanye masihara- watu wa Tanga wanaijua starehe bwanaa!! Baadhi ya wadau wakila raha na Miss Tanga Telent iliyokuwa imeandaliwa na Five Brothers Entertainment.

Unakumbuka wimbo wa msanii wa bongo flava Bwana Misosi- unaitwa MABINTI WA KITANGA!! basi alikuwa anamaanisha hivi.


Makamua kutoka Wakali Kwanza alipiga Show!!!

Q-Jay nae alipagawisha kwa sana!!

Nahisi kama ungekuwepo mdau wangu!

Kiukweli washkaji wa Wakali Kwanza walibamba!! Ilikuwa shangwe sana baada ya kuimba wimbo wao wa NATAMANI

Mkurugenzi wa Five Brothers Nasa Makao akiwa na warembo kumi waliongia moja kwa moja kwenye Miss Tanga Talent- warembo hao watachuana vikali siku ya Jumamosi ya terehe 6/6/2009 kunako ukumbi wa Mkwakwani. Ila washiriki wa Miss tanga 2009 wapo ishirini. Talent hiyo ilisimamiwa na Mc shupavu kutoka hapa Tanga, Ras Bizo ambaye aliwa shangwe za kutosha mashabiki.

No comments:

Post a Comment