BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, May 25, 2009

MALTA GUINNESS STREET DANCE 2009 YATUA TANGA!!


Haya tena wakazi wa jiji la Tanga na vitongoji vyake- hatimae yale mashindano ya kuwasaka vijana wenye vipaji vya kucheza mitaani imetia timu jijini hapa.

Usahili unatarajiwa kufanyika terehe 6/6/2009 katika ukumbi wa Tanga Hotel maeneo ya Chumbageni. Ukifika tu mahala hapo utakutana na muwakilishi wa Malta Guinnes na atakupa fomu ya ushiriki.



Lakini pia washiriki wote wanaotaka kushiriki mashindano haya ya Ku'shake...watatakiwa kufika kwenye ukumbi wa Tanga Hotel tarehe 4/6/2009 kuanzia muda wa saa nane mchana kabla ya mashindani, hii ikiwa ni kwa ajili ya semina fupi itakayotolewa kuhusiana na mashindano hayo.

Kiingilio ni Malta Guinnes mbili tu, kama wewe ni mdau wa maswala ya kucheza muziki- njoo uwape tafu vijana wenzako wa mkoani Tanga ili waweze kupata nguvu ya kutuwakilisha vyema huko waendapo.

Zaidi ni kwamba msanii wa kizai kipya ( Bongo Flava) matonya atakuwepo katika kuwasherehesha watu watakaofika hapo siku hiyo- Naamini Tanga tunaweza wadau wangu!!

Kwa maelezo zaidi gonga hapa- http://www.mgstreetdanceafrica.com/

No comments:

Post a Comment