BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, May 16, 2009

NI RACHEL MLAKI MISS TANGA CITY CENTER 2009.


Mshiriki namba nne, Rachel Mlaki akiwa kwenye tabasamu pana baada ya kuvikwa taji la Miss Tanga City Center 2009

Rachel Malki akiwa mshindi wa pili wa Miss Tanga City Center 2009 Ester Flavian, na mshindi wa tatu Martha Moses


Hongera Rachel Mlaki

Mamiss wote walikuwa bomba, ila palikuwa hapatoshi hadi akapatikana mmoja


Hii ndio ilikuwa tano bora ya Miss Tanga City Center 2009. Washindi wote hawa wamepata nafasi ya kushiriki Miss Tanga 2009, ambayo itafanyika June 6 kwenye uwanja wa Mkwakwani


Mkurugenzi wa Five Brothers Entertainment, Nasa Makao akiwa jukwaani tayari kumtangza mnyange wa Miss Tanga City Center.
Moja kati ya Penel of Judges, Asma Makao na Nasa Makao- wakifuatilia kwa makini mtanange wa Miss Tanga City Center ili kuweza kutoka kitu kamili
Hawa ndio washiriki wote wa Miss Central Tanga City Center 2009

Msanii Roma, mzee wa Tanzania alipiga bonge la show

Roma akilishambulia jukwaa ipasavyo

Msanii Hemed a.k.a PHD kutoka Tusker Project Fame aliwakilisha vya kutosha

Hemed akiwa mzigoni

From now where!! Msanii Cassim aliyewahi kutanba na wimbo wake wa AWENA na e alitia timu. Kikubwa ni kwamba aliwasabahi tu wakazi wa jiji la Tanga.

Cassim akiwa na mmoja wa MC aliyesherehesha vizuri Miss Central- anaitwa Antonio Nuga

Antonio Nuga, Hemed pamoja na Cassim. Nyuma ya pazia

Bra-A kutoka Redio Mwambao Fm, mmoja wa washereheshaji wa Miss Central akiwa na mnyange wa kitongoji hicho 2009 Rachel Mlaki


Panel of Dj's kutoka Redio Mwambao Fm- aliyevaa fulana nyekundu ni Dj Rogger Kiss, akifuatiwa na DjBob Nass pamoja na Dj Don Chill. Kwa pamoja wakiwa makini katika kufanya Mixing.

Wana Mwambao Fm walikuwepo katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, baada ya kuwa mdhamini mkuu wa mashindanio hayo. Wa lwanza ni Mkali Lupa, Moshen, anty Moza, Leila totii pamoja na Blandina Lukindo.

Mkurugenzi wa Redio Mwambao Fm Tanga, Ahmed Simba akifuatilia kwa makini mashindano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Swimming Club maeneo ya Raskazoni.


Fatuma Makoko na Zena, kwa pamoja ndio wanaunda ZEFA Promotion, ambayo ndio imeandaa Miss Tanga City Center 2009- mashindano hayo pia yalidhaminiwa na Mwambao Fm sauti ya Tanga. Ambako Rachel Malaki ameibuka na mshindi, lakini pia washindi wengine wanne wamepata fursa ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka Miss tanga 2009 inayotarajiwa kufanyika June 6 kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa chini ya FIVE BROTHERS ENTERTAINMENT

1 comment:

  1. Rachel Mlak awa mshindi wa kwanza kwny Miss Udom 2010,add the cv in da blog

    ReplyDelete