BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, May 8, 2009

NAS, KELIS WATEMANA KIAINA!!

Habari zilizokuwa zikielezwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu harakati za kutengana kwa wanandoa Nas na Kelis takribani kwa mwezi mzima uliopita leo zimethibishwa na msemaji wa Kelis
"Nina thibisha kuwa Kelis ameshasign hati za kuachana na Nas" alieleza wakili Laura Wasser ambaye pia amewahi kuwa wakili wa Britney Spears, Angelina Jolie na Steve Wonder.
Wakili huyu alijaza hati hizo kwa niaba ya Kelis akieleza kuwa ni kwa sababu zisizorekebishika wasanii hao wameamua kila mmoja kula hamsini zake.
Hata hivyo Kelis kwa sasa anaujauzito wa takribani miezi 7 akitarajia mtoto wakiume. Baadhi ya wapenzi na mashabiki wa nyota hao wamesikitika huku wakibaki kusema huenda Nas hana bahati na warembo.

No comments:

Post a Comment