BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, May 20, 2009

WEMA SEPETU AJIRUDI KWA KANUMBA


Hivi juzi kwenye kipindi cha Bongo Movies kinachorushwa na kituo kimoja cha televisheni cha Chennel Ten, palikuwepo na mahojiano ya kati ya wasanii wasili ambao ni vinara kwenye Tasnia ya Filamu nchini Tanzania- Wema Sepetu na Steven Kanumba kuhusiana na Saga lao la kufikishana mahakamani.
Katika mahojiano hayho ambayo kwa namna moja ama nyengine yalikuwa ya kufurahisha kama sio kuburudisha, baada ya wasanii hao kuonekana kukwama kwama kwenye maelezo yao juu ya mustakabali mzima kwenye sanaa ya filamu.

Wema alinikuliwa akikiri kuwa, kweli hakuwa anajitambua wakati akifanya tukio la kuvunja kioo cha gari la Kanumba hivyo anaomba msamaha kwa tukio hilo. Pia mlimwende huyo wa Tanzania kwa mwaka 2006 alisema kuwa, kwa sasa ugomvi wao na Kanumba umekwisha na yupo tayari kuendelea kufanya nae kazi.

Cha kushangaza, kanumba likanusha kauli za Wema baada ya kusema hadi sasa mambo kati yao si shwari- na kuhsu kuendelea kufanya kazi za filamu msanii huyo amesema kuwa ni mapema sana kuzungumzia hilo au ni mapema sana kwa sasa kushiriki movie moja na Wema kutokana kwamba bado hakijaeleweka kati yao.

Hivi kuna nini kati yao hawa watu..? Lakini zaidi ya hapo msanii mwengine ambaye pia ni kinara kwenye Tasnia ya Filamu Tanzania maarufu kama JB alisema kuwa, wamekuwa wakipigana kufa na kupona kuhakikisha wasanii hao wanaelewana na ushirikiano wao katika filamu uendelee kama kawaida.



No comments:

Post a Comment