Kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha jijini Tanga, tayari kumekuwa na matukio tofauti tofauti ya hatari zinazosababishwa na mvua hizo. Camera ya Anko Mo Blogspot ilinasa tukio hili la kukatika kwa nyaya za umeme kunako eneo la Mabanda Ya Papa.
Gari la Tanesco likiwa limesimama katika eneo la tukio, wakiwa tayari kwa kurekebisha nyaya za umeme zilizokatika.
Wafanyakazi wa Tanesco wakijaribu kutatua tatizo hilo huku wananchi wakitazama wakati kazi hiyo ikiendelea
Hali hiyo ya pia iliweza kusababisha foleni za hapa na pale mpaka Tanesco walipomaliza kazi yao.
No comments:
Post a Comment