BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Saturday, October 24, 2009

FIESTA ONE LOVE LEO JIJINI TANGA- MVUA NIAJEEE BANA!!!!


Sikukuu ya wasanii Tanzania maarufu kama Fiesta safari hii ikiwa ni ONE LOVE- inashuka leo jijini Tanga huku kila kona ya mji ukiwa na hamu ya kutaka kupata raha hizo.
Katika hali isiyo ya kawaida, jiji la Tanga asubuhi ya leo hadi kufikia saa nane mchana kumekuwa na mvua kubwa jambo lilloonekana kuwakatisha tamaa wapenda burudani.
Hata hivyo shangwe zinasubiriwa kwa hamu, kwani waswahili husema Maji Ukishayavulia Nguo Ni Sharti Uyaoge!!!
Anko Mo Blogspot itajivinjari kunako uwanja wa Mkwakwani kushuhudia show hiyo na kukuletea picha za ukweli kwenye kurasa hii.

No comments:

Post a Comment