MKOA wa Mwanza umezidi kung'ara kupitia sanaa mchini baada ya mshiriki kutoka mkoani humo, Pascal Cassian kuibuka mshindi katika shindano la kusaka vipaji vya waimbaji chipukizi maarufu kama Bongo Star Search ambalo fainali zake zilifikia tamati jana usiku kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kabla ya ushindi huo, tayari Mwanza ilikuwa imetwaa mara mbili mfululizo taji la urembo maarufu kama 'Miss Tanzania 2009' baada mwanadada Miriam Gerald kuibuka mshind.
Kabla ya ushindi huo, tayari Mwanza ilikuwa imetwaa mara mbili mfululizo taji la urembo maarufu kama 'Miss Tanzania 2009' baada mwanadada Miriam Gerald kuibuka mshind.
Kutokana na ushindi huo, Cassian aliweza kutia kibindoni fedha taslimu sh25 milioni kutoka kwa waandaaji wa shindano Kampuni ya Benchmark Production .
Mbali na zawadi hiyo kutoka kwa waandaaji, mshindi huyo pia alikabidhiwa sh1,500,000 baada ya kuibuka mtunzi bora wa wimbo wa ukimwi sambamba na kitita kingine cha Sh500,000 kutoka duka la mavazi la Mariedo Botique ambalo pia lilidhamini shindano hilo.

Washindi wa mashindano hayo ni pamoja na Peter Msechu kutoka Kigoma, ambaye alishika nafasi ya pili- Kelvin Mbati nafasi ya tatu na Jackosn George kutokea Tanga. Mshiriki pekee wa kike Beatrice William alishika nafasi ya tano huku akipata zawadi ya mavazi kutoka Mariedo kama kifutio jasho.
Jackosn George- TANGA
Mkoa wa Tanga ulishindwa kung'ara kwenye mashindano ya Miss Tanzania yaliyofanyika mwaka huu, huku mshiriki wake Glory Chuwa akirudi nyumbani mikono mitupu. Jamani---- watanga mpooooo!!
No comments:
Post a Comment