BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, October 2, 2009

MISS TANZANIA 2009- WASHIRIKI KUCHUANA VIKALI USIKU WA LEO!!

Mshiriki kutoka Tanga, Glory Chuwa akiwa amepozi wa kwanza mwenye namba ya ushiriki MOJA. Washiriki 30 leo watashuka jukwaani kumsaka mnyange wa Miss Tanzania 2009

Washiriki wengine wa Miss Tanzania 2009- kutoka namba 6 hadi 10


Kutoka namba 11 hadi 15


Kutoka namba 16 hadi 20


Washiriki kutoka namba 21 hadi 25


Hawa ni washiriki kutoka namba 26 hadi 30


Mbali ya mshindi kuvikwa taji lililonakshiwa kwa vito vya madini ya tanzanite, pia ataondoka na gari aina ya Suzuki Grand, lenye thamani ya sh mil. 53.2 na fedha taslimu shilingi mil. 9.

Mrembo atakayevikwa taji usiku wa leo, atakuwa ni wa 17 tangu kuruhusiwa tena kwa shindano hilo mwaka 1994, baada ya kupigwa marufuku mwaka 1968.
Kwa upande wa shindano la leo, atakayekamata nafasi ya pili, atajitwalia shilingi mil. 6.4; mshindi wa tatu sh mil. nne; huku mrembo wa 11 hadi 29, akilamba shilingi 700,000.

Aidha, warembo watawania mataji mengine madogo kama Mrembo Mwenye Mvuto ‘Redd’s Photogenic’ atakayetangazwa leo na kujitwalia sh mil. moja zitakazotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Warembo watakaopanda jukwaani leo, ni Glory Chuwa (Tanga), Sylia Shally (Ilala), Miriam Gerarld (Mwanza), Jackline Nitwa (Dodoma), Shanny Anthony (Temeke),Wagala Shungu (Vyuo Vikuu), Inony Bigirwa (Kinondoni), Julieth William (Ilala), Sabina Budodi (Mara), Stellah Chidodo (Kanda ya Kati) na Ester Gao (Vyuo Vikuu).

Wengine ni Doris Deonatus (Vyuo Vikuu), Sandra Malebeka ( Kinondoni), Sia Ndaskoi (Temeke), Stella Solomoni (15-Temeke), Mary Lucas (Nyanda za Juu Kusini), Suzan Emmanuel (Arusha), Alocyia Innocent (Kinondoni), Gladdies Shao ( Ilala) na Precious Donald wa Pwani.

Wamo pia Maria Daniel Arusha (Arusha), Gloria Mayowa (Lindi), Lulu Ibrahim (Kinondoni), Beatrice Lukindo (Vyuo Vikuu), Evelyn Gamasa ( Ilala), Glory William (Ilala), Catherine Letara (Nyanda za Juu Kusini),Torry Oscar (Morogoro) na Mary Joseph kutoka Mara.

Mgeni rasmi katika fainali za leo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ladislaus Komba.
Shindano hilo litasindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Koffie Olomide, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Mshindi wa leo, ataingia kwenye orodha ndefu ya waliowahi kulitwaa tangu mwaka 1994, ambako kwa mwaka huo, mshindi alikuwa ni Aina Maeda, ambaye alivikwa taji katika Hoteli ya White Sands.
Waliofuatiwa kwa miaka, ni Emily Adolph, Shose Senare, Saida Kessy, Basila Mwanukuzi, Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe, Happiness Magesse, Angela Damas, Sylvia Bahame, Faraja Kotta, Nancy Sumari, Wema Sepetu, Richa Adhia na Nasreem.


No comments:

Post a Comment