BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, October 6, 2009

HII NDIO PANGANI (PAN TOWN)- KARIBUNI SANA WAGENI

Jiwe hili la kumbukumbu pia- liliwekwa na wajerumani July 23 mwaka 1916. Lipo Pangani karibu na kivuko


Hili jiwe liliwekwa hapa miaka kumi baada ya Tanzania kupata uhuru wake kutoka kwa mkolini


Hii Lodge inapatikana Pangani- ipo barabara inayoelekea Halmashauri

Kituo cha utalii wilayani Pangani, Tanga kama kinavyoonekana katika picha


Moja kati ya majengo ambayo yanafanya mji wa Pangani kuwa kivutio kikubwa cha watalii duniani

Jengo jengine ambalo lipo katikati ya mji wa Pangani- watalii wengi huja kutazama majengo haya ya kihistoria

Hapa ni karibu na barabara ya Jamhuri, baadhi ya boti zikiwa zimepaki ufukweni

Anko Mo akiongea na simu wakati akiwa wilayani Pangani kikazi- Pangani ni mji mtulivu, huku ukipambwa na upepo mwanana wa bahari

Boti za kuvulia samaki zikiwa zimepaki ufukweni- sikuwa najua kama Pangani ipo karibu sana na Zanzibar!!! Watu huenda na kurudi

Boti na makumbi ya nazi baharini- Pangani husifika kwa kutoa nazi pia. Kuna mashamba ya minazi sana

Hapa panaitwa STOP OVER, moja ya bar maarufu wilayani Pangani ambayo watalii wengi hufika kwa ajili ya kula na kunywa!! Hapa ndipo nilipokuwa natoa menyu ya Pizza wadau

Pangani kwa majengo ya kihistoria usipimie- tazama jengo jengine hapa

Hapa panaitwa PANGADECO- klabu ya kujirusha siku za wikiend. Ipo baharini kabisaaaaa

Sio zote!!! Hii ni moja tu ya Beach zinazopatikana Pangani

Ukitaka kuamini Pangani inasifika kwa nazi tazama hiki kifuu- kipo baharini

Hii ndio anga ya Pangani wadau- KARIBUNI PANGANI







1 comment:

  1. Safi sana Anko Mo. Asante kwa kutuletea vijimambo vya mkoa wetu.
    Daima mbele nyuma mwiko, kaza uzi.

    Fresh Jumbe
    Tokyo.

    ReplyDelete