BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, March 24, 2009

KARIBUNI TANGA WADAU.

Moja kati ya watu ambao nawaheshimu sana katika maisha yangu, ni baba yangu mzazi Hammie Rajab ambaye kwa kweli amekuwa akinionyesha njia nzuri ya kuishi maisha bora hapo baadae. Kupitia vitabu ambavyo ameandika kama 'SANDA YA JAMBAZI', ' KAMLETE AKIBISHA MLIPUE', 'MLIMA KOLELO' pamoja na novo ambayo inasomwa nchini Kenya hivi sasa 'REST IN PEACE DEAR MOTHER' ni miongozi mwa vitabu vilivyonipa msukumo mkubwa wa kuingia kwenye ramani ya uwandishi ili hali kuendeleza heshima yake kwenye fani hii.

Nawakaribisha ndugu, jamaa, marafiki pamoja na kila mwenye kuvutiwa na blog hii, tubadilishane mawazo ili tuweze kumshinda mdudu UJINGA katika nchini yetu.

Kwa sasa nafanya kazi Redio Mwambao Fm Sauti Ya Tanga, nipo hapa kama mtangazaji, mwandishi wa habari na kusimamia productio za redio.

Nimeshaandika hadithi pia, ila kwa sasa zaidi ya kuwa mmoja wa watu wanofanya vizuri mkoani Tanga kupita Redio- lakini pia naandika makala kwenye gazeti la Tanga Yetu ambalo lipo hapa Tanga.

Karibuni Wote, ila huu ni mwanzo tu. Kila kitu kitakaa sawa mambo yakiwa mazuri zaidi.

No comments:

Post a Comment