BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, March 27, 2009

Mh. Mohammed Abdulazizi- Mkuu wa mkoa Tanga.

MKUU wa Mkoa wa Tanga,Mheshimiwa Mohamed Abdulaziz akizungumzia maandalizi ya zoezi la upigaji kura za maoni kuwaibini watu wanaojihusisha na Mauaji ya Albino,Vikongwe na wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi pamoja na uuzaji na ununuzi wa dawa za kulevya katika kipindi cha Amka na Mwambao Machi.27.2009.
Zoezi la upigaji kura huo limefanyika Mkoani Tanga Machi 28 mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu,Mheshimiwa Mizengo Pinda aliyelizindua Machi 5 mwaka huu.
Anayefanya mahojiano naye ni Msimamizi wa Kipindi cha Amka na Mwambao kinachotangazwa na Radio Mwambao FM 106.0 cha jijini Tanga,Bw.Benedict Kaguo
.


Kipindi cha Amka na Mwambao hujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kero za wananchi,Mada mbalimbali ambazo msikilizaji hupata fursa ya kupiga simu ama kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kuuliza ama kuchangia mada hiyo.
Kipindi kinarushwa kila siku za isipokuwa Jumapili kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi na kinadhaminiwa na Mtandao wa Simu za Mkononi wa Tigo.

Unapokuwa Mkoani Tanga sikiliza kipindi hiki kupitia 106.0 Mwambao Fm Sauti ya Tanga uweze kuhabarika na kuburudika zaidi.


Katika Kipindi hicho watu mbalimbaliwameshahojiwa akiwemo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Simon Sirro,Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,Bw.Deodatus Kinawiro,Afisa Uhusiano na Umma wa Mamlaka ya Majisafi na Maji Taka jijini Tanga,Tanga Uwasa,Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo,Dokta Joseph Nzige,


Pia Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto jiji la Tanga,Ayubu Mhando,Mratibu wa Elimu ya Sekondari Wilayani Mkinga,Omari Kombo,Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya Mkinga,Zahoro Idrisa,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Salim Bawazir,Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Tanga,Hamisi Jafari,Katibu wa Uhamasishaji wa Mchezo wa Ndondi Mkoa wa Tanga,Allan Kamote.




No comments:

Post a Comment