BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, March 25, 2009

MOJA KATI YA MA'DJ WAKALI JIJINI TANGA- DJ BOB NASS



Nikiwa jijini Tanga nilikwenda disko usiku katika club moja maarufu jijini hapa inayoitwa Lacasa Chica. Kulipigwa nyimbo changanyiko na zakuvutia sana, muda wote huo nilikuwa kwenye kiti nikipata kinnywaji. Ila ulipoigwa wimbo wa Lady uliopigwa na vijana wa Modjo wanaotokea kule nchini Ufaransa nikashindwa kuvumilia.


Hakika ulikuwa wimbo mzuri sana ulionivutia na kugusa hisia zangu. Hivyo ilinibidi niinuke toka kitni na kwenda kuselebuka, baada ya muziki huo kuisha ndipo nikaamua kwenda juu aliko Dj anayepiga muziki ili nimpongeze kwa kazi nzuri.


Nilistaajabu baada ya kumuona kijana mdogo kiumri hadi kiumbo nikidhani labda kamshikia Dj husika. Sikusita kumuuliza maswali machache, na ndipo nilipogundua kuwa ni yeye ndiye aliyekuwa akiporomosha muziki kwa kipindi chote kile nilichokuwa pale.

Nilishtuka sana!!
Kikubwa kilichonishtua ni kutokana na umahiri wake wa kufanyanya "Scrutching" pamoja na kupangilia midundo ya muziki aliokuwa akipiga. Hakika sikuwa mimi pekee niliyevutiwa na utundu aliokuwa anaufanya, nilishakuwa na mazoea ya kusikiliza muziki bila kufanyiwa "Mixing"- au hata kama ikiwa hivyo basi ni kwenye Redio ambazo zina watu ambao wamesomea kwa kina maswala hayo.


Nikapata hamasa ya kufanya nae mahojiano si unajua kazi zetu za uandishi ni kama askari akiwa vitani kila unapoenda unakuwa na zana tayari kwa lolote, mahali popote bila kujali mazingira ili mradi hali iwe ina ruhusu.

Akiniambia nimpe kama nusu saa aweze kumaliza kazi kisha tuongee nami kwa vile nilikuwa natamaa ya kujua kwanini kijana kama yeye baada ya kuwa anajisomea kwa muda huo wa usiku yuko mahali kama pale anaburudisha watu.
Kwa zile nusu saa alizonipa, zilikuwa pia changamoto kwangu kuweza kumsikiliza kwa kina ili ninapoanza nae mahojiano nipate kitu ambacho nimekikusudia kukipata toka kwake.


Nilijivuta pembeni karibu na kinywaji changu nilichokuwa nimekiwacha mezani, kisha nikawa nasubiri.
Alipomaliza ndipo sasa Tukaanza mahojiana kwa kunafahamisha yeye ni nani na anatokea wapi. Jina lake la kuzaliwa ni Nasir Bakari Thabit, ana umri wa miaka 20 na kabila lake ni Mngoni. Pamoja na kutokea Iringa lakini pia kijana huyu ni mwenyeji wa mji wa Tanga kwani amezaliwa hapa na kusomea hapa pia.
Anasema alianza masuala ya muziki toka akiwa shule ya msingi darasa la nne, wakati huo alikuwa anapenda sana kusikiliza muziki wa rap haswa wa msanii mongwe kwenye ramani ya Bongo Flava hapa nchini Tanzania Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr2.


Zaidi ya hapo pia alikuwa akimhusudu sana hayati 2pac Shakur na alikuwa akiyaandika mashairi ya nyimbo za wasanii hao pembeni kitu kilichofanya ajue kuimba kwa kufuatisha mashairi na akaanza kujifunza utunzi akiwa na umri mdogo.
Alipofika darasa la tano alikuwa anaufahamu wa muziki huku akiwa na mjomba wake anayeitwa Musa Thabit ambaye alikuwa anakwenda nae disko toto wakati wa likizo. Wakifika disko yeye na mjomba wake wanakaa kwa Dj kisha mjomba wake anamuomba Dj amfundishe Nasir jinsi ya kupiga muziki na vitu vidogo vidogo vinavyohusiana na u'Dj.

Kutokana na mwanzo huo aliweza kujijenga vyema na kuweza kupiga disko kwenye madisko toto mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika wakati huo kama vile Saruji club pamoja na Maweni club hasa wakati wa sikukuu na likizo ndefu.
Alipoingia sekondari mwaka 2004 tayari alishajua mambo mengi kuhusu maswala ya muziki na u'Dj kwa ujumla kwani alikuwa anakwenda Internet Caf'e kujifunza zaidi na kujua watu wa nchi za magharibi wanafanya nini kwani kwa hapa Tanzania hakuna shule ya u'Dj na kupitia Internet alidhanin kungeweza kumsaidi.


Aliweza pia kufanya Downloading kwa softwares za u'Dj ili kufahamu vizuri na pia wakati wote huo akiwa shule, rafiki zake walimtia hamasa na hari ya kujifunza zaidi muziki na u'Dj ambapo hadi anamaliza kidato cha nne tayari alikuwa ni mzoefu juu maswala hayo.
Mnamo mwaka 2008 alifanikiwa kuingia katika kituo cha radio hapa jijini Tanga kinachoitwa Mwambao fm. Hapo Nasir alijifunza si tu u'Dj bali hata uandishi wa habari na utangazaji.
Akiwa Mwambao Fm tayari amekutana na watu wengi waliokuwa na ufahamu zaidi yake na kwamba mpaka sasa anapiga kwenye kumbi mbalimbali mmoja wapo ndio ambao alikutana na mwandishi wa makala hii.


Nasir au Bobnas anasema katika kuhangaika kwake kulikuwa kuna watu waliokuwa wakimpa moyo na kumuongezea hari kwa kila hatua anayoifikia. Akiwashukuru watu hao, Bob Nas aliwataja wazazi wake pamoja na familia yake kwa ujumla, mjomba wake, marafikizake na pia Mkurugenzi wa radio Mwambao Bw Ahmed Simba kwa kukiona kipaji chake mapema na kukiinua halikadhalika Dj maarufu kwa mkoa wa Tanga Raphael Chambo au Dj Rach kuty na Dj Donchlee ambao bado wanaendelea kumpa mafunzo zaidi.
Hata hivyo Nasir ndoto zake ni kuwa mmoja wa maDj maarufu kama vile John Dilinga au Dj JD ambaye kwa upande wake anamkubali kwa kazi zake, ambazo kwa upande wake zimekuwa zikimpa changamoto sana.


Pia kuhusu swala la kuwa producer, Bob Nas maarufu kama Mkali wa milazo- mchai wa Mixing amesema kuwa kwa sasa ameanza kujifunza kuhusiana na utengenezaji wa nyimbo.

Pamoja na kutaka kutema cheche kwenye maswala ya utengenezaji muziki, Nasir pia ameshawahi kushirikishwa kwenye wimbo wa msanii maarufu kwenye muziki wa Bongo Flava anayeitwa Pete ambaye pia ameshawahi kutamba na kibao chake cha Mazoea alichomshirikisha Rado.
Wimbo ambao Nasir ameshirikishwa na msanii huyo unaitwa Nenda ambao pia ndani yake kuna Dj Roger Kiss ambaye nae ni mmoja kati waonafanya vizuri Redio mwambao pamoja na Tin Dady, kazi ilifanyika King Falcom Production chini ya Producer Sam Chad.
Huyo ni Nasir Thabit, wengi humfahamu kama Dj Bobnas. Kwa sasa ni mmoja kati ya wafanyakazi wa redio Mwambao Fm, ambayo ipo hapa jijini Tanga.

Safari yake yakulekea kwenye u'Dj bora na u'Producer ni ndefu sana, ila amenipa changamoto kuwa kama wazazi tunapaswa tuangalie watoto wetu wanataka nini na tujaribu kuwapa moyo na tushirikiane nao kwa pamoja katika kutimiza ndoto zao kwani kama sio mjomba wake kukiona kipaji chake toka hapo awali basi nafikiri sasa hivi angekuwa darasani akipata elimu. Sipingi asisome, ila kipaji ndio kitu pekee kilichomfanya awepo mahala alipo sasa.

No comments:

Post a Comment