BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, March 25, 2009

Tuesday, March 24, 2009

NAKAAYA NDANI YA LUV NA M1 WA Dead Prezz
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari ambaye siku za karibuni wametemana na mchumba wake wa siku nyingi, hatimaye amezama ndani ya penzi zito la msanii wa kundi la Dead Prezz kutoka Marekani M1. M1 ambaye ameshirikishwa kwenye...Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari ambaye siku za karibuni wametemana na mchumba wake wa siku nyingi, hatimaye amezama ndani ya penzi zito la msanii wa kundi la Dead Prezz kutoka Marekani.M1 ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo wa Mr Politician ulioimbwa na mnyange huyo.Katika mahojiano na kituo kimoja cha Radio kipindi yupo nchini M1, akiulizwa swali la kizushi M1 aliwahi kukiri kuwa Nakaaya ni mwanamke mrembo ambaye mwanaume yeyote akiambiwa awe nae hata sita kukubali na kama hatakubali basi atakuwa na matatizo.Baada ya majibu hayo ya M1 yalizuka maneno ya kuwa baada ya Nakaaya kuachana na mchumba wake wa siku nyingi alikuwa na mahusiano na Mwanamuziki huyo habari ambazo zilikuwa za chini ya kapeti mpaka leo hii ambapo Nakaaya kwa mdomo wake mwenyewe amekubali kuwa ni kweli ana uhusiano na msela huyo wa nchini kwa Obama.Akipasha zaidi Nakaaya anasema kuwa tayari wameshaingia kwenye hatua za kuelekea kwenye agizo la Mungu yani kufunga pingu za maisha kwani jamaa tayari kashamvalisha pete ya uchumba hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment