Kamati ya maandalizi ya Kumtafuta Miss Pangani 2010 imekutana leo katika ukumbi wa hoteli ya Koleprento uliopo Jijini tanga kwa ajili ya kujadili juu ya Mashindano hayo.
Muandaaji wa MissPangani , Mohammed Hammie kupitia kampuni ya Anko Mo Blogspot inayofanya shughulisha na maswala ya habari kwa njia ya Internet jijini Tanga- aliliambia gazeti hili kuwa maandalizi ya mashindano hayo yataendelea kufanyika mara kwa mara ili kufanikisha zoezi hilo ambalo litashirikisha warembo nane.
Kitongoji cha Miss Pangani ni kipya katika mchakato wa kusaka warembo mkoani hapa, ambapo kimeahidi kuleta mabadiliko katika sanaa ya urembo nchini Tanzania.
Vitongoji vyengine vilivyopewa dhamana ya kutoa warembo kwa ajili ya kumsaka Miss Tanga na hatimae Miss Tanzania ni pamoja kitongoji cha Ngamiani,Usagara,Chumbageni,College,Tanga city centre,Korogwe, na Lushoto
Hata hivyo Bw Mohammed amesema kuwa, kwa kuwa wilaya ya Pangani ni sehemu ya utalii mkoani Tanga. Hivyo kampuni yake imeona kuna haja kuchukua nafasi hiyo kutanga utalii wilayani humo kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi wake kutambua thamani ya eneo lao.
Mashindano ya urembo yameonekana kukuwa kwa kasi mkoani Tanga lakini takribani miaka miwili kumekuwa na ukosefu wa kushika nafasi za juu kunako mashindano ya taifa ya miss Tanzania.
Hivi karibuni mrembo Glory Chuwa kutokea mkoani hapa amejikuta akishika nafasi za chini katika mtanange huo uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mbele ya kamati kuu ya Miss Pangani, Bw Mohammed ameongeza kuwa katika shindano hilo washiriki watakaofanya vizuri kuanzia nafasi ya kwanza hadi ya Tatu watapata tiketi ya kuungana na Washiriki wengine katika Kinyanganyiro cha Kumsaka Miss Tanga ambaye atapata nafasi ya kwenda kuuwakilisha mkoa katika mashindano ya taifa ambapo kilele chake kimemalizika hivi juzi na Miriam Gerlad kutokea Mwanza kuibuka kidedea.
Aidha katika shindano hilo ambalo litawashirikisha washiriki (8)mshindi wa wa kwanza atajinyakulia kitita cha Tsh 400,000 -Mshindi wa pili 250,000, na Mshindi wa tatu 150,000. Mshindi wa 4 na 5 watajinyakulia tsh 100,000 na Washindi wengine wa 6 na 8 tsh 50,000 kila mmoja.
Na Oscar Assenga, Tanga.