
Parokia ya Mtakatifu Anthony wa Padua, Chumbageni ilianzishwa na Mapadre wa Shirika la Roho Mtakatifu. Ilikuwa ni moja ya sehemu za Vikarieti ya Kilimanjaro. Jinsi muda ulivyoenda, na bidii ya Wamisionari, wakristu waliongezeka. Hawa ni baadhi ya Mapadre waliofanya kazi katika Parokia hii kipindi hicho: Pd. Francis Kennedy, Pd. James Cannolly, na Pd. O’Kane.
Wamisionari walifungua vigango mbalimbali kandokando ya barabara kuu za Tanga-Mombasa, Tanga-Pangani na Tanga-Moshi. Vilevile waliwahudumia wafungwa ambao walikuwa wamehukumiwa kunyongwa katika Gereza kuu la Maweni Tanga. Mheshimiwa Pd. Madden wakati fulani alihudumia wafungwa ishirini na tatu. Miaka ya 1960, Pd. Gerald Smith aliendeleza vigango vingine, navyo ni Mtakatifu Karoli Lwanga-Majani Mapana, Mtakatifu Josef Kagwa-Amboni, Mtakatifu Mathias Mulumba-Usagara, Mtakatifu Petro Saruji na Mtakatifu Gerald Pongwe. Vigango vingine ni Chote, Kisimatui, Kange, Kakindu, Mkembe na Jaribu Tena.
Mwaka 1948 Tanga pamoja na bandari yake ilifanywa kuwa Mkoa maalumu kwa viwanda vya Mkonge. Tukio hili liliifanya Tanga kukua na kufahamika zaidi, hata hivyo watu waliongezeka zaidi kwa ajili ya kufanyakazi katika mashamba ya mkonge na viwandani. Mwaka wa 1952 mji wa Tanga peke yake ulikuwa na wakazi waafrika wapatao 4,635, waarabu 1,029, waeshia 5,779 na wazungu 558.

Pia alijenga Hostel ya wasichana katika parokia ya Mt. Anthony wa Padua, Chumbageni. Hostel hii daima imekuwa msaada mkubwa kwa wasichana wanaosoma elimu ya sekondari na vyuo Tanga mjni. Pia alijenga Go-down, kubwa Chumbageni ambalo linatumika hadi sasa.
Pd. Smith pia alikuwa ni Wakili wa Askofu wakati wa Mhashamu Askoufu Maurus Komba. Alipohamia parokia ya Mt. Petro Saruji Pongwe, Pd.. Martin Maganga akawa paroko mpya wa parokia ya Mt. Anton wa Padua, Chumbageni Tanga.
Pd. Gerard Smith alifariki mwaka 2001 na kuzikwa huko parokia Gare. Pd. Firmat Tarimo akawa paroko mpya katika parokia ya Mt. Petro Saruji Pongwe.
No comments:
Post a Comment