BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, January 24, 2011

KLABU MPYA YAFUNGULIWA TANGA- INAITWA PWEZA!!

Kama atatokea mtu kuniuliza kuna tofauti gani kati ya Tanga ya leo na Tanga ya miaka ishirini iliyopita basi dhahiri nitamjibu kuwa tofauti kubwa ni ongezeko la klabu katika kuwafanya watu wake wawe na sehemu ya kupata starehe baada ya kazi za wiki nzima. Nasema hivyo kwa sababu hivi karibuni kumefunguliwa klabu nyengine mpya inayotwa PWEZA.

Nilipata bahati ya kuhudhuria siku ya ufunguzi. Nilichokutana nacho na wewe ningependa ukakione. Klabu moja safi yenye manndhari mazuri. Air Condition kupoza joto. Bei safi ya vinywaji huku ukipata muziki mzuri kutoka kwa maDj wanaojua kufanya kazi yao vyema. Ipo eneo la Chuda Relini. Zamani ilijulikana kama La Club Tanzanite.


Hapa ni kwa ndani. Taa zake zilikuwa zikiwaka na kung'arisha kila kona. Zaidi ya PWEZA pia Tanga kuna klabu nyengine kama Lacasa Chica, Ibiza Carnival pomoja na Lavida Loca.

No comments:

Post a Comment