BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, January 11, 2011

MFAHAMU FRESH JUMBE MKUU KUTOKA TANGA!!

Fresh Jumbe Mkuu Waziri Kungugu Kitandamilima alizaliwa tar. 19 Oktoba, 1968 katika hospitali ya Ngamiani iliyopo katikati ya jiji la Tanga, Tanzania. Anatoka kwenye familia ya watoto nane, wanne wa kiume na wanne wa kike.

Wazazi wake wote wawili wametokea wilaya ya Pangani mkoani Tanga. Mama yake anatokea katika kijiji cha Bweni kinachoangalia mto Pangani na baba kwenye tarafa ya Mkwaja kijiji cha Buyuni kitopeni kilichopo mpakani kabisa kati ya wilaya ya Pangani na Bagamoyo.

Akiwa Tanga sehemu anayoiita nyumbani ni Makorora “Mti Mkavu” karibu kabisa na shule ya msingi Makorora ambayo ndipo alipoanzia elimu yake ya msingi kabla ya kuelekea Bakwata Sekondari kwa ajili ya elimu ya sekondari.

Fresh Jumbe ni mmojawapo wa wanamuziki wanaofanya muziki wa dansi akiwa nchi za nje. Na inaaminika kuwa analiwakilisha taifa lake katika nyanja za muziki huo vilivyo. Rasmi anafanyia shughuli zake za muziki nchini Japan. Lakini awali alikuwa na baadhi ya bendi za muziki huo kama vile Sikinde, Msondo, Bicco Stars, Safari Sound na nyingine nyingi tu. Kwa hakika Fresh Jumbe ni mojawapo ya majina ambayo washika dau katika medani za muziki hawawezi kuyasahau.

Tangu akiwa mdogo Fresh Jumbe alikuwa na ndoto ya kuwa mwimbaji. Kipindi fulani wakati akiwa bado katika shule ya msingi kule Tanga, aliwahi kuapa kuwa maisha yake ya ukubwani, kama yatakuwa ni ya kimasikini au ni yakitajiri au vyovyote vile, basi yatakuwa yametokana na miziki.

Aliapa kuwa uimbaji ndio utakaoongoza maisha yake. Kwahiyo ndoto yake hiyo nilianza kuifuatilia mapema tu akiwa bado mdogo kabisa na matokeo yake ni kuwa, mpaka leo maisha yake ni muziki na muziki ndiyo maisha yake.

Jumbe alivutiwa sana na marehemu Marijani Rajabu kutokana na utungaji wake, uimbaji wake na ufanyaji wake wa kazi akiwa jukwaani alimfanya atake kuwa kama yeye.

Mwingine ni kaka yake binamu "Marika Mwakichui" ambaye alikuwa mwimbaji wa bendi ya Tanga International ya Tanga. Yeye pia alikuwa mwimbaji mzuri na ndiye aliyempandishaAlign Center kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza ili aimbe baada ya kugundua uwezo wake wa kuimba akiwa bado yuko darasa la sita.Alimpa moyo sana na kumwambia kuwa yeye anaweza kabisa kuimba kuliko hata baadhi ya waimbaji wakubwa wa wakati ule. Hivyo shukrani za dhati zikamwendea ndugu huyo kwa msukumo na msaada aliompa na kumfanya ajiamini na aingie kikamili kwenye muziki mpaka kufikia alipofikia leo hii.

Mnamo mwaka wa 1988 akiwa katika bendi ya Safari Sound "Ndekule", Taasisi ya Kuhifadhi Mazingira ya Tanzania kupitia chama cha muziki wa dansi Tanzania "CHAMUDATA" iliteua baadhi ya watungaji iliyoamini kuwa ni watungaji wazuri, ili watunge nyimbo mbili za uhifadhi wa mazingira ili zikawakilishe nchi ya Tanzania kwenye Tamasha la kuhifadhi mazingira la Afrika katika siku ya mazingira duniani. Kwa wakati huo kwa upande wa Afrika, tamasha lilifanyika mjini Nairobi, Kenya.

Jumbe alikuwa mmoja kati ya walioteliwa kutunga nyimbo hizo. Walioitwa katika katika utunzi huo alikuwa Cosmass Chidumule, marehemu Hemedi Maneti, Jah Kimbute, marehemu Eddy Sheggy, marehemu Jerry Nashon "Dudumizi" na wengine kadhaa.

Walipewa maelekezo ya kila mtu kutunga nyimbo moja ya mazingira. Pia walielezwa ni masuala gani muhimu yanayotakiwa kuzungumzwa kwenye hizo nyimbo. Wakapewa wiki mbili za kutunga nyimbo. Pia waliambiwa kuwa, haya ni mashindano na washindi wawili watakaopatikana, yaani watakaotunga nyimbo mbili za kwanza zitakazokubalika zaidi na Taasisi ya Mazingira ya Tanzania, watapata zawadi ya pesa na pia wao ndiyo watakuwa wawakilishi wa nchi kwenye hilo tamasha la mazingira huko mjini Nairobi. Kwa bahati nzuri, nyimbo yake ikawa namba moja na ya Cosmass Chidumule ikawa ya pili.

Zawadi zikatolewa kwa washindi na pia wakapelekwa Nairobi kuiwakilisha nchi kwenye tamasha hilo. Hilo ndilo lilikuwa chimbuko la wimbo wa "Tuhifadhi Mazingira" na ndiyo wimbo pekee uliyomleta juu katika masiha ya muziki.No comments:

Post a Comment