BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, January 20, 2011

HISTORIA YA TANGA HAPO ZAMANI!!

Mji wa Tanga ni mji mkuu wa Mkoa wa Tanga uliyoko ufukoni mwa Bahari ya Hindi. Tanga ina bandari kubwa kabisa katika sehumu ya kaskazini mwa Tanzania. Njia ya reli kwenda Mji wa Moshi inaanza hapa.

Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni: Iliyo nyooka; Bonde lenye rutuba; Barabara upande wa mto na Shamba juu ya mlima, neno hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei ambalo ni wenyeji wa mkoa huo linamaana ya shamba, wao hulitamka N'tanga

Tanga insaemekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya 14 BK. Mji wa Tanga haikupata umuhimu kama mji wa jirani ya Mombasa. Tarihi ya Pate inasema ya kwamba kabla ya kuja kwa Wareno Pate iliwahi kutawala Lindi kwa muda fulani.

Katika karne ya 19 BK Tanga ilikuwa chini ya utawala wa Omani na Zanzibar. Misafara ya biashara imeanzishwa hapa kwenda bara. Kutokana na bandari yake nzuri ya kiasili Tanga ilikua sana wakati wa ukoloni wa Wajerumani waliojenga bandari wa kisasa pamoja reli kwanda Moshi. Reli iliwezesha kilimo kwa ajili ya soko la dunia Tanga ikawa bandari kuu kwa jili ya katani na kahawa.

Baada ya Uingereza kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani reli ya Tanga-Moshi iliunganishwa na ile ya kati hivyo ikawa na njia kwenda Daressalaam pia. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Tanga iliona mapigano makali tar. 3 - 5 Novemba 1914. Jaribio la Uingereza kuvamia Tanga kwa kikosi cha maaskari 8000 Waingereza na Wahindi kutoka meli kwenye Bahari Hindi ilishindwa vibaya na Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck.

Mwaka 1922 "Tanganyika Territory African Civil Services Association" (TAA) iliundwa Tanga ambayo ilikuwa shirika ya kwanza ya Kiafrika yenye shabaha za kisiasa.

No comments:

Post a Comment