BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, February 21, 2011

MWIZI APONEA CHUPU CHUPU KUFA TANGA!

Kijana mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, ameponea chupuchupu kufa baada ya wananchi wenye hasira kali kumshushia kipigo. Kijana huyo ambaye alikuwa ameiba simu ya mkononi aina ya Nokia, alikumbwa na dhahama hiyo siku ya jana majira ya saa kumi katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani hapa jijini Tanga.

Katika purukushani hizo, baadhi ya wananchi walichukua jukumu la kumkimbizia kijana huyo katika kituo kidogo cha polisi kilichopo hapo stendi baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na huenda akapoteza maisha.

Katika picha wananchi wakimkimbiza mwizi ambaye alikuwa anapelekwa katika kituo cha polisi.

Baada ya kuhakikisha yupo mikononi mwa polisi. Mmoja baadaa mwengine alirudi na kuendelea na shughuli zake.
No comments:

Post a Comment