BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, February 17, 2011

WAKULIMA TANGA WAINGIZWA MFUMO VOCHA ZA RUZUKU

WAKULIMA 47,294 wa Wilaya za Korogwe, Muheza, Kilindi, Handeni na Lushoto mkoani hapa, wameingizwa katika mpango wa kupata mbolea unaoratibiwa kwa mfumo wa vocha za ruzuku.

Wakulima hao wa mahindi na mpunga watanufaika kwa kulima hekari 18,918 na kati ya hizo mpunga utalimwa kwenye hekari 874 na mahindi hekari 18,044.

Kwa mujibu wa Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Tanga, Lameck Tungu ili kukamilisha utaratibu huo kwa msimu wa kilimo wa 2010/2011, tayari uongozi wa mkoa umekabidhiwa vocha 141,878 zenye thamani ya Sh bilioni 2.6 na zimegawiwa katika wilaya husika.

“Kwa kuzingatia mgao huu, tayari mkoa umekwishakabidhi vocha wilayani na maandalizi ya awali ya matumizi yake yameanza ili pembejeo hizo zianze kutumika katika msimu wa masika wa 2010/2011, kwa maeneo yenye skimu za umwagiliaji,”alisema.

Alitaja aina za pembejeo zitakazogawanywa kupitia mfumo huo kuwa ni mbegu ya mahindi OPV, mbegu ya mpunga, mbolea ya kupandia (DAP) pamoja na mbolea ya kukuzia (UREA).

Katika msimu uliopita wa 2009/20101 wilaya tatu tu za Lushoto, Muheza na Korogwe zilizonufaika na vocha 5,400 za pembejeo zenye thamani ya Sh milioni 94.2.

Pembejeo hizo zilitumika katika mashamba ya wakulima 2,655 walioko katika skimu za umwagiliaji zilizopo Kitivo (Lushoto), Mombo (Korogwe) na Muheza.No comments:

Post a Comment