BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, August 4, 2011

AUAWA KWA KUUA WATOTO WAWILI KWA SHOKA

MKAZI wa kijiji cha Misima, Rashidi Maglasi (35), ameuawa na wananchi akituhumiwa kuwaua watoto wawili kwa kuwakata kwa shoka vichwani na kuwajeruhi wazazi wao.


Tukio hilo lilitokea hivi karibuni baada ya Maglasi kuwaua Ridhiwan Bakari (6) aliyekuwa na baba yake Bakari Mokiwa (53) ambao walikuwa wakitokea hospitali kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo. Katika tukio hilo, muuaji huyo alimjeruhi baba wa mtoto huyo.


Habari zaidi zinasema kwamba baada ya tukio hilo, muuaji huyo alikimbia umbali mrefu kidogo ndipo alipokutana na Mwajiha Mwalimu akiwa na mtoto wake Gumbo Mukwagu (4) ambapo aliendeleza mashambulizi hayo na kumuua mtoto na kisha kumjeruhi mama yake.


Baada ya tukio hilo, Mwalimu alipiga kelele za kuomba msaada ndipo wananchi walipotokea na kuanza kumshambulia muuaji huyo hadi kufa. Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Masawe, alisema huenda muuaji alikua na matatizo ya akili, jambo ambalo bado halijapatiwa uthibitisho.


Hata hivyo wazazi wa watoto hao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Handeni wakiendelea na matibabu na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Auawa kwa kuua watoto wawili kwa shoka.

Na Bertha Mwambela, Handeni, Tanga

No comments:

Post a Comment