BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, August 2, 2011

KUTOKUFUNGA MWEZI WA RAMADHANI

Kufunga Ramadhani ni nguzo ya nne katika nguzo tano za Kiislamu na kutokufunga Ramadhani bila udhuru wowote ule wa kisheria ni moja ya madhambi makubwa sabini. Mwenyezi Mungu S.W.T. kautukuza sana mwezi wa Ramadhani kuliko miezi yote mingine kwani imeteremshwa Qurani katika mwezi huu mtukufu na pia kajaalia kuwepo katika mwezi huu usiku wa Lailatul-Qadri usiku wa heshima, usiku ulio bora kuliko miezu elfu.


Kufunga katika mwezi huu mtukufu ni faridha wajibu kwa aliyetimiza masharti yake, kama ilivyokuwa faridha wajibu kwa wale waliokuwa kabla yetu. Na yule atakaeacha kufunga siku moja tu bila sababu yoyote ile ya kisheria kama vile ugonjwa au safari, basi atakuwa amefanya madhambi makubwa. Na akifa katika hali hiyo basi atakuwa amefanya dhambi kubwa na adhabu yake ni kubwa nayo ni Moto wa Jahannam. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Baqarah aya ya 183 na ya 184, "?يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمْ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ * أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ¦?


Maana yake, "Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumchaMungu. Siku chache (kufunga huko), basi atakaekuwa mgonjwa miongoni mwenu au katika safari (akafungua) basi (atimize) hesabu katika siku nyingine."Na pia Hadithi iliyopokelewa na Ibn `Umar R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari na Muslim, Mtume S.A.W. kasema, ""بُنِيَ الإسْلامُ عَلَى خَمْسٍ : شَهَادَةِ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ وَصَوْمِ رَمَضَانَ وَحَجِّ الْبَيْتِ."Maana yake, "Umejengwa Uislamu kwa nguzo tano, (nguzo ya kwanza):


Hapana mungu mwenye kupasa kuabudiwa ila Allah, na hakika Muhammad S.A.W. ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na (nguzo ya pili): Kusimamisha Sala, na (nguzo ya tatu): Kutoa Zaka, na (nguzo ya nne): Kufunga (mwezi wa) Ramadhani na (nguzo ya tano): Kuhiji (nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa yule mwenye uwezo)."Sahaba Ibn Abbaas R.A.A. kasema, ""عُرَى الإِسْلامِ وقواعد الدين ثلاث : شَهَادَةِ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ ، والصَّلاةُ ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ."Maana yake, "Uislamu pamoja na kanuni za dini zimefungamana na mambo matatu: Shahada ya kuwa hapana apasae kuabudiwa (kwa haki) ila ALLAH na Sala na kufunga mwezi wa Ramadhani."

No comments:

Post a Comment