BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, August 2, 2011

FAIDA YA FUTARI YA TENDE NA MAJI


Assalam alaykoum,

Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) ametufundisha namna ya kufturu na vyenye faida katika miongoni mwa futari.
Kufuturu ni kitu cha kwanza kinachofungua kinywa cha mfungaji mara baada ya kumaliza muda wa kufunga katika siku husika. Kifungua kinywa hiki cha mwanzo ndio huitwa futari.
Nabii wa karne hii ya sayansi na teknolojia ametuhusia sana Waislaam tunapokuwa tumefunga, ni vyema kufturu kwa tende au maji.


Mafundisho haya ya Mtume Muhammas (S.A.W) yamekuwa kinyume kabisa na namna waislaam wengi wanavyofungua saumu zao.
Watu wengi wanapofungua saum zao hukimbilia kula vyakula vya nafaka kama vile uji, juice, tambi, katlesi n.k. Pamoja na kufuturu vitu hivo vizito katika tumbo, huwa mfuturuji wa vyakula vingi mwisho hushindwa kuhema uzuri.Kuhusiana na kula Mtume Muhammad ametuhusia sana tumbo tuligawe sehemu tatu kuu nazo ni:-MajiChakulaHewa.
Utaratibu huu wakulipa nafasi tumbo kwa chakula, maji na hewa unasaidia sana katika mfumo wa usagaji wa chakula.Tende na maji ni vitu vilivyotajwa sana kwa matumisi ya mfungaji wa saum na mzazi pia.


"Basi akachukua mimba yake akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali kisha uchungu ukampelekea katika shina la mtende, akawa anazaa huku anasema laiti ningelikufa kabla ya haya na ningelikuwa niliyesahaulika kabisa, mara ikafika sauti chini kutoka chini yake ikamuambia usihuzunike Maryaam hakika Mola wako amejaalia kijito cha maji chini yako. Na litikise shina la mtende kwako litaangusha tende nzuri zilizoiva basi ule, unywe na liulie jicho lako furahi na pumua moyo wako." (QUR-AAN 19:22-26)
Kutokana na mafundisho hayo ya Quraan inaonesha tumbo la mtu aliyezaa linahitaji tende au maji kama ilivyo mtu mwenye kufunga.


Jambo la kujiuliza hekima ipi Mtume ameitumia katika kutufundisha kula tende na maji na sio kula vyakula vizito.Vyakula vya nafaka kama vile mbaazi,viazi,maandazi n.k ni vyakula vizito husababisha maumivu katika tumbo.
Hali hii hutokana na ukweli kuwa katika ukuta wa tumbo la chakula na hata katika utumbo mwembamba kuna maji mazito mfano wake kama ute wa yai la kuku, maji hayo yanasaidia aina mbali mbali za acid zisifike katika ngozi ya tumbo na kufanya michubuko ambayo yanaweza kuleta ugonjwa wa vidonda vya tumbo.Kuta za tumbo zinapokutana na acid husababisha eneo hilo kutepeta na kulifanya liwe laini.


FAIDA YA TENDE NA MAJI: katika tende na maji kuna madini mengi yanayoambatana na sukari na hewa ya oxygen. Vitu vinapofika katika eneo hili vinasaidia kupunguza nguvu ya gas, gas ambayo ikizidi hatima yake huleta matatizo na magonjwa.
Kwahio Inshallah ftari yetu ya mwanzo iwe ni tende kwa maji kisha utafuatilisha machopochopo mengine ambayo machoopochopo hayo yasiwe yakushibisha kiasi ambacho mtu ukashindwa hata kuswali taraweh.


No comments:

Post a Comment