BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, July 16, 2010

TANGA YETU YA LEO!!!!!

Chuo cha kiislam cha Zahrau cha jijini Tanga, kipo eneo la madina njia ya kwenda Sahare.

Eneo la soko la Ngamiani.

Soko la Ngamiani...wananchi wa Tanga wakiwa kwenye mahitaji yao ya kila siku.

Karibu na stendi kuu ya mabasi.....sehemu ya kuingia.

Taifa Road.......moja kati ya njia kuu inayopitiwa na barabara za namba zote.

Reli za Tanga zinavyoonekana sasa.

Bodaboda wa baiskeli Tanga kibao......hapa ni kituo cha reli.

Makutano ya barabara kutokea Chumbageni polisi...

Hapa ni eneo maarufu sana...linajulikana kama Tawakal! Tende Shake utazipata hapa

TOVUTI YA MKOA WA TANGA HADI LINI...!????

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa umekuwa katika michango mbalimbali ya kukuza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) katika ngazi ya mkoa na halmashauri za wilaya kwa lengo la kujenga serikali mtandao (e-government). Kuimarika kwa matumizi haya ya (TEKNOHAMA) kutasaidia sana kurahisisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika shughuli mbalimbali za kila siku kati ya serikali (mkoa), halmashauri za wilaya na wadau wengine.

Moja ya vitu ilivyoshughulikia ni uanzishwaji wa Tovuti za Mikoa kwa Mikoa yote ya Tanzania bara. Ambapo tovuti hizi zimezinduliwa rasmi na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda tarehe 19 Februari 2009 halfla hiyo imefanyika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro

Wasi wasi wangu ni kwamba hadi sasa mkoa wa Tanga hauna tovuti tangu waziri mkuu Mizengo Pinda atangaze nia yake hiyo Februari 2009. Pichani mkoa wa Morogoro ukiwa tayari umepatiwa tovuti yake....humo kuna kila kitu kinachohusu mkoa huo. Sisi Tanga hadi lini..>>????

Pichani tovuti ya mkoa wa Kagera, tovuti ya mkoa wa Tabora na tovuti ya mkoa wa Dar es salaam. Tunaomba mkuu wa mkoa wa Tanga Saidi Kalembo ulitazame hili. Mkoa wako hadi sasa haujapata tovuti.

Thursday, July 15, 2010

'TANZANIA' -YA MKALI ROMA

MUHEZA HIYO MZEEEEEEEEEEEEEE!!!

Restaurant maarufu wilayani Muheza WHITE HOUSE! Ipo barabarani kabisa.

Kituo cha kuweka mafuta.....ipo kona ya kuingia stendi kuu ya mabasi.

Mgahawa....

Kuelekea Amani....

Mchuuzi wa machungwa....twende kazi!!

Boda boda za pikipiki kila kona ya muheza na Tanga nzima.

Hapa ni kona ya kuingia stendi kuu kama ukitokea Segera.

Mitaa ya Muheza..

Wednesday, July 14, 2010

'BINADAMU' UNTOUCHABLE FT KASSIM- MKALI MWENGINE WA HIP HOP KUTOKA TANGA

'FIGHTER'- NGOMA MPYA YA ZAYUMBA

Jana nilitumiwa wimbo mpya na mshkaji kutokea hapa Tanga- Malick Zayumba! Sikiliza ngoma yake hapo pembeni kulia palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Ngoma inaitwa 'Fighter' imetengenezwa pale Bard Number record chini ya producer Riz Mocko. Tayari Zayumba anatamba na ngoma yake nyengine inayoitwa 'Najiamini' ambayo amemshirikisha Kaju kaju.......kichwa chengine cha Hip Hop kutokea Tanga City hicho.

Tuesday, July 13, 2010

BENEDICT KAGUO, OSCAR ASSENGA WAPEWA TUZO.

MWANDISHI wa gazeti la Majira Mtangazaji wa Radio Mwambao Fm ya jijini Tanga, Benedict Kaguo 'Father K' kulia akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Entertainment Nassor Makau ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kufanikisha Mashindano ya Miss Tanga yaliyoandaliwa na Kampuni hiyo.

Hafla hiyo fupi iliyofanyika juzi kwenye makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Ring street hapa jijini Tanga. Shindano la kumsaka mnyange wa Miss Tanga yalifikia tamati kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort ambapo Anna Kiwambo aliibuka kidedea.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Bingwa na mtangazaji wa Mwambao Fm Radio Oscar Assenga akikabidhiwa cheti cha ushiriki na kufanikisha mashindano ya Miss Tanga 2010 kutoka kwa Mkurugenzi wa Five Brothers Entertainment Nassor Makao ofisini kwake kwenye hafla hiyo ilifanyika na kuhudhiriwa na watu wachache

Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Entertainment Nassor Makau akimkabidhi cheti cha ushiriki Mwaandaaji wa Miss Usagara 2010 Asia Msangi katika makao makuu ya Kampuni hiyo Mtaa wa Ring jijini Tanga.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Entertainment Nassor Makau katikati akijadiliana jambo na waandishi mahiri wa sanaa ya urembo Benedict Kaguo kushoto na Oscar Assenga Mwandishi wa New Habari Co-operation wachapishaji wa gazeti la Bingwa nje ya ofisi ya kampuni hiyo mtaa wa Ring jijini Tanga.

'UNAPOCHEZA NA MIMI'- CHIWA FT YORAM NA FAT ZINGA



Video ya vijana wa Kitanga.....

ROMA FUNIKO BOVU FIESTA YA ARUSHA!

Mkali wa Hip Hop kutokea Tanga Rymes Of Magic Attraction a.k.a ROMA alipiga bonge la show na kuacha midomo wazi wakazi wa Arusha wakati wa show ya Fiesta iliyoandaliwa na Clouds Fm....

Fiesta ambayo hufanyika kila mwaka, safari hii imekuja na JIPANGUSE RRRARAAAAAAAA!! Inatarajiwa kuja tanga siku ya jumamosi ya tarehe 24 mwezi huu. Kaa tayari joo!

Monday, July 12, 2010

STENDI KUU YA MABASI KOROGWE- BADO IPO KWENYE MATENGENEZO!!

Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoni hapa wilayani Korogwe bado ipo kwenye matengenezo. Stendi hiyo maarufu kama Manundu, inatarajiwa kumaliziaka hivi karibuni.

Katapila likiwa kwenye utengenezaji wa stendi hiyo.

Kwa sasa stendi imehamishiwa huku eneo la Babylon ama Mwembeni.

Stendi ya Korogwe kwa sasa

Harakati huwa haziishi maeneo ya stendi

Korogwe hiyo!

Hapa ni karibu na stendi ambayo ipo kwenye matengenezo kwa sasa, Manundu

KUMRADHI KWA KIMYA KIREFU WADAU!!

Habari wadau...Ni siku takribani tano nimekuwa kimya. Naomba radhi kwa kimya kirefu, kutokana na tatizo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wangu. Network ilikuwa shida karibu nchi nzima.

Monday, July 5, 2010

UHURU MAONI- HASSAN WA LUSHOTO!

TANGA TOWN LEO ASUBUHI!!

Karibu na mabanda ya papa

Mitaa ya komesho.

Mabawa Polisi

Njia ya kuelekea Magomeni.

St. Joseph Commercial School...........

Jengo la CCM karibu na barabara ya 20.

Makutano ya barabara...njia ya kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Tanga kwa Baiskeli....karibu na msikiti wa Mabawa

MWAMBAO FM- KITOVU CHA BURUDANI JIJINI TANGA!!

Mtangazaji mahiri wa redio Mwambao ya jijini Tanga Benedict Kaguo akiwa studio. Kaguo ni mkali kwenye maswala ya habari na pia anatangaza kipindi cha ZILIPENDWA kila jumamosi jioni.

Sekei Hassan a.k.a Dj Passion utampata kwenye Tanga Flava, Tz Most Wanted na Indian Flava.

Mamaa Leyla Totii a.k.a Top In Town....utampata kwenye Jipe Raha mambo ya taarab na miduara.

Keisha Ridhwan....moja kati ya watangazaji mahiri ndani ya Mwambao Fm. Utampata kwenye Misosi 'Meza Ya Chakula na Vinywaji'

Wa kwanza ni Fatuma Rajab- utampata kwenye Ukimwi Na Jamii. Akiwa na Sekei Hassan na Leyla Totii

Benedict Kaguo na Leyla Totii wakiwa studio. Hawa ni baadhi tu ya watangazaji wa redio Mwambao Fm. Wapo wengi...endelea kutembelea Blog utakuja kuwaona.

Friday, July 2, 2010

MADJ WANAOFANYA VIZURI JIJINI TANGA!!!

One Love!!!! Dj Bob Nass akiwa na Djs wengine wanaofanya vizuri jijini Tanga, wa kati aliyevaa shati la maua ni Dj Roger Kiss wa Breeze Fm na Dj Rachy Kuty wa Club Lavida Loca!

Thursday, July 1, 2010

VICHEKESHO VYA KING MAJUTO WA TANGA!!!

MFAHAMU FRESH JUMBE MKUU!!!

Fresh Jumbe Mkuu Waziri Kungugu Kitandamilima alizaliwa tar. 19 Oktoba, 1968 katika hospitali ya Ngamiani iliyopo katikati ya jiji la Tanga, Tanzania. Anatoka kwenye familia ya watoto nane, wanne wa kiume na wanne wa kike.

Wazazi wake wote wawili wametokea wilaya ya Pangani mkoani Tanga. Mama yake anatokea katika kijiji cha Bweni kinachoangalia mto Pangani na baba kwenye tarafa ya Mkwaja kijiji cha Buyuni kitopeni kilichopo mpakani kabisa kati ya wilaya ya Pangani na Bagamoyo.

Akiwa Tanga sehemu anayoiita nyumbani ni Makorora “Mti Mkavu” karibu kabisa na shule ya msingi Makorora ambayo ndipo alipoanzia elimu yake ya msingi kabla ya kuelekea Bakwata Sekondari kwa ajili ya elimu ya sekondari.

Fresh Jumbe ni mmojawapo wa wanamuziki wanaofanya muziki wa dansi akiwa nchi za nje. Na inaaminika kuwa analiwakilisha taifa lake katika nyanja za muziki huo vilivyo. Rasmi anafanyia shughuli zake za muziki nchini Japan. Lakini awali alikuwa na baadhi ya bendi za muziki huo kama vile Sikinde, Msondo, Bicco Stars, Safari Sound na nyingine nyingi tu. Kwa hakika Fresh Jumbe ni mojawapo ya majina ambayo washika dau katika medani za muziki hawawezi kuyasahau.

Tangu akiwa mdogo Fresh Jumbe alikuwa na ndoto ya kuwa mwimbaji. Kipindi fulani wakati akiwa bado katika shule ya msingi kule Tanga, aliwahi kuapa kuwa maisha yake ya ukubwani, kama yatakuwa ni ya kimasikini au ni yakitajiri au vyovyote vile, basi yatakuwa yametokana na miziki.

Aliapa kuwa uimbaji ndio utakaoongoza maisha yake. Kwahiyo ndoto yake hiyo nilianza kuifuatilia mapema tu akiwa bado mdogo kabisa na matokeo yake ni kuwa, mpaka leo maisha yake ni muziki na muziki ndiyo maisha yake.



Jumbe alivutiwa sana na marehemu Marijani Rajabu kutokana na utungaji wake, uimbaji wake na ufanyaji wake wa kazi akiwa jukwaani alimfanya atake kuwa kama yeye.

Mwingine ni kaka yake binamu "Marika Mwakichui" ambaye alikuwa mwimbaji wa bendi ya Tanga International ya Tanga. Yeye pia alikuwa mwimbaji mzuri na ndiye aliyempandisha kwenye jukwaa kwa mara ya kwanza ili aimbe baada ya kugundua uwezo wake wa kuimba akiwa bado yuko darasa la sita.

Alimpa moyo sana na kumwambia kuwa yeye anaweza kabisa kuimba kuliko hata baadhi ya waimbaji wakubwa wa wakati ule. Hivyo shukrani za dhati zikamwendea ndugu huyo kwa msukumo na msaada aliompa na kumfanya ajiamini na aingie kikamili kwenye muziki mpaka kufikia alipofikia leo hii.



Mnamo mwaka wa 1988 akiwa katika bendi ya Safari Sound "Ndekule", Taasisi ya Kuhifadhi Mazingira ya Tanzania kupitia chama cha muziki wa dansi Tanzania "CHAMUDATA" iliteua baadhi ya watungaji iliyoamini kuwa ni watungaji wazuri, ili watunge nyimbo mbili za uhifadhi wa mazingira ili zikawakilishe nchi ya Tanzania kwenye Tamasha la kuhifadhi mazingira la Afrika katika siku ya mazingira duniani. Kwa wakati huo kwa upande wa Afrika, tamasha lilifanyika mjini Nairobi, Kenya.

Jumbe alikuwa mmoja kati ya walioteliwa kutunga nyimbo hizo. Walioitwa katika katika utunzi huo alikuwa Cosmass Chidumule, marehemu Hemedi Maneti, Jah Kimbute, marehemu Eddy Sheggy, marehemu Jerry Nashon "Dudumizi" na wengine kadhaa.

Walipewa maelekezo ya kila mtu kutunga nyimbo moja ya mazingira. Pia walielezwa ni masuala gani muhimu yanayotakiwa kuzungumzwa kwenye hizo nyimbo. Wakapewa wiki mbili za kutunga nyimbo. Pia waliambiwa kuwa, haya ni mashindano na washindi wawili watakaopatikana, yaani watakaotunga nyimbo mbili za kwanza zitakazokubalika zaidi na Taasisi ya Mazingira ya Tanzania, watapata zawadi ya pesa na pia wao ndiyo watakuwa wawakilishi wa nchi kwenye hilo tamasha la mazingira huko mjini Nairobi. Kwa bahati nzuri, nyimbo yake ikawa namba moja na ya Cosmass Chidumule ikawa ya pili.

Zawadi zikatolewa kwa washindi na pia wakapelekwa Nairobi kuiwakilisha nchi kwenye tamasha hilo. Hilo ndilo lilikuwa chimbuko la wimbo wa "Tuhifadhi Mazingira" na ndiyo wimbo pekee uliyomleta juu katika masiha ya muziki.