BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, February 23, 2010

'SITAKI TENA LAWAMA, NIMEPATA MCHUMBA'- HEMED

Hemed Suleyman a.k.a Hemed kijana aliyetikisa jumba la project fame kwa mwaka juzi ameibuka na kutangaza kuwa amechoshwa na kesi za kutembea na wake za watu ambazo zinamharibia sifa yake na sasa ameamua kuoa na siku za hivi atamtangaza mchumba wake ambaye atakuwa mkewe mtarajiwa.

Akichonga na hivi karibuni ambaye kwasasa amejikita zaidi kwenye mambo ya filamu amesema amepokea lawama nyingi na kesi kibao kuhusu kutembea na wake za watu lakini sasa ndio utakuwa mwisho.

“Nimeshapata mchumba na soon nitamweka wazi kila mtu amjuwe, hizi kesi zisizoisha sizitaki tena, lawama mtaani ya kuwa natembea sijui na demu wa fulani au mke wa mtu nimechoka nazo, sana sana zinaniharibia sifa yangu tu kila kukicha” alisema Hemed.

Hemed ambaye alikuwa mmoja wa wakilishi kwenye lile shindano la kuibua vipaji la Afrika Mashariki maarufu kama Tusker Project Fame aliingia kwenye masuala ya mziki mwaka jana na kufanikiwa kutoa baadhi ya nyimbo ambazo zilitingisha kama NINACHOTAKA na ULISEMA, yuko chini ya kituo cha kukuza vipaji cha THT.



No comments:

Post a Comment