BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, February 28, 2011

WATENDAJI WA VIJIJI, MITAA KOROGWE WAZEMBE KUKIONA!


MKUU wa wilaya ya Korogwe, Erasto Sima amewataka wananchi kumtaarifu juu ya watendaji wa serikali za vijiji wanaokiuka sheria na taratibu kwa kushindwa kuitisha mikutano mikuu ya vijiji.

Ametoa agizo hilo baada ya kukabidhi baiskeli 122 zenye thamani ya Sh milioni 15.2 kwa watendaji wa vijiji vinavyounda Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kupitia mradi wa kusaidia utekelezaji wa utawala bora katika serikali za mitaa.

Mradi huo unafadhiliwa na Mpango wa Ushirikiano wa Ujerumani na Tanzania wa kuimarisha utawala bora ngazi ya jamii (SULGO-GIZ).

Alisema ukwepaji wa kuitishwa kwa mkutano mkuu wa kijiji au mikutano mingine ya kawaida ikiwemo ya kutoa taarifa za mapato na matumizi ya kijiji unaofanywa na baadhi ya watendaji katika serikali za vijiji ni ishara ya wazi ya ukiukwaji wa misingi ya utawala bora katika jamii.

Alisema wananchi wana wajibu wa kumpa taarifa awashughulikie watendaji wa namna hiyo.

“Nimejulishwa kwamba pamoja na msaada huu wa baiskeli mradi wa SULGO-GIZ tayari umewajengea uwezo kuhusu majukumu na uwezo wa halmashauri za vijiji ikiwemo kanuni za kuandaa, kuendesha mikutano mbalimbali ya vijiji,” alisema na kuongeza:

“Mikutano hiyo iwasaidie kuandaa bajeti na mipango ya maendeleo kwa lengo la kuhakikisha misingi ya utawala bora naya kidemokrasia na isimamiwe ipasavyo ili kuharakisha maendeleo lakini kinyume na matarajio, baadhi yenu bado mnaendelea kulalamikiwa na wananchi kwamba hamuitishi mikutano inavyostahili na kusababisha wananchi kuchelea kushiriki kuchangia maendeleo yao”.

Mkuu huyo alisema hatasita kumchukulia hatua za kinidhamu Ofisa Mtendaji yeyote wa kijiji na kata ambaye atabaini kuwa ameshindwa kusimamia misingi ya utawala bora.

Aliwataka watendaji hao kutumia baiskeli kuwafikia wananchi katika vitongoji mbalimbali wakati wa kuhamasisha, kutekeleza miradi ya maendeleo na hasa wanapoanza maandalizi na kusambaza taarifa za mikutano ya kijiji.

Na: Anna Makange
, korogwe

Wednesday, February 23, 2011

Tuesday, February 22, 2011

TAARIFA YA MSIBA PONGWE, TANGA!

Familia ya Mr. & Mrs Ally Mwinyikombo ya hapa Tanga, Pongwe inatangaza kifo cha kijana wao Mbwana .A. Fungo kilichotokea mjini Dodoma. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kuja hapa Tanga kwa mazishi inafanywa.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote popote pale walipo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Ameen.

Sisi tulikupenda, ila Allah alikupenda zaidi.

TOP C KUIWAKILISHA TANGA KWENYE TUZO ZA KILI!



Msanii wa muziki wa kizazi kipya Top C anayetokea Tanga ametajwa kwenye tuzo za Kili 2011 katika category mbili tofauti ambazo ni WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA pamoja na MSANII MPYA ANAYECHIPUKIA yaani (UPCOMING ARTIST).

Top C kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Lofa' uliotengenezwa pale Sharobaro Records chini ya Producer Bob Junior! Unyesha uzalendo kwa kumpigia kura Top C punde mchakato huo utakapoanza.

19. MSANII MPYA ANAYECHIPUKIA (UPCOMING ARTIST)

SAM WA UKWELI

LINAH

SAJNA

BOB JUNIOR

TOP C

***************


22. WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA

SINA RAHA-SAM WA UKWELI

LOFA-TOP C

NABEMBELEZWA-BARNABA

ROBO SAA-AMINI

BORA NIKIMBIE-LINAH

*****************


TAREHE 1 MARCH 2011 RAIA NA MASHABIKI WA MUZIKI WATAANZA KUPIGA KURA.

*TAREHE 24 MARCH 2011 MAJAJI WATAHAKIKI KURA.

*USIKU WA UTOAJI TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2011,YAANI JUMAMOSI YA TAREHE 26 MARCH 2011

Monday, February 21, 2011

MWIZI APONEA CHUPU CHUPU KUFA TANGA!

Kijana mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, ameponea chupuchupu kufa baada ya wananchi wenye hasira kali kumshushia kipigo. Kijana huyo ambaye alikuwa ameiba simu ya mkononi aina ya Nokia, alikumbwa na dhahama hiyo siku ya jana majira ya saa kumi katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani hapa jijini Tanga.

Katika purukushani hizo, baadhi ya wananchi walichukua jukumu la kumkimbizia kijana huyo katika kituo kidogo cha polisi kilichopo hapo stendi baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na huenda akapoteza maisha.

Katika picha wananchi wakimkimbiza mwizi ambaye alikuwa anapelekwa katika kituo cha polisi.

Baada ya kuhakikisha yupo mikononi mwa polisi. Mmoja baadaa mwengine alirudi na kuendelea na shughuli zake.




Thursday, February 17, 2011

WAKULIMA TANGA WAINGIZWA MFUMO VOCHA ZA RUZUKU

WAKULIMA 47,294 wa Wilaya za Korogwe, Muheza, Kilindi, Handeni na Lushoto mkoani hapa, wameingizwa katika mpango wa kupata mbolea unaoratibiwa kwa mfumo wa vocha za ruzuku.

Wakulima hao wa mahindi na mpunga watanufaika kwa kulima hekari 18,918 na kati ya hizo mpunga utalimwa kwenye hekari 874 na mahindi hekari 18,044.

Kwa mujibu wa Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Tanga, Lameck Tungu ili kukamilisha utaratibu huo kwa msimu wa kilimo wa 2010/2011, tayari uongozi wa mkoa umekabidhiwa vocha 141,878 zenye thamani ya Sh bilioni 2.6 na zimegawiwa katika wilaya husika.

“Kwa kuzingatia mgao huu, tayari mkoa umekwishakabidhi vocha wilayani na maandalizi ya awali ya matumizi yake yameanza ili pembejeo hizo zianze kutumika katika msimu wa masika wa 2010/2011, kwa maeneo yenye skimu za umwagiliaji,”alisema.

Alitaja aina za pembejeo zitakazogawanywa kupitia mfumo huo kuwa ni mbegu ya mahindi OPV, mbegu ya mpunga, mbolea ya kupandia (DAP) pamoja na mbolea ya kukuzia (UREA).

Katika msimu uliopita wa 2009/20101 wilaya tatu tu za Lushoto, Muheza na Korogwe zilizonufaika na vocha 5,400 za pembejeo zenye thamani ya Sh milioni 94.2.

Pembejeo hizo zilitumika katika mashamba ya wakulima 2,655 walioko katika skimu za umwagiliaji zilizopo Kitivo (Lushoto), Mombo (Korogwe) na Muheza.



TANGA YAONGEZA UZALISHAJI WA CHAKULA

MKOA wa Tanga umefanikiwa kuongeza zaidi ya tani 374, 118 za chakula zinazotosheleza mahitaji ya wakazi wake kwa mwaka 2010/2011.

Hatua hiyo imetokana na wananchi kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo kuhamasika na kuaongeza uzalishaji wa mazao hayo baada ya mavuno ya ndizi na majimbi kubadilishwa na kuwa katika hali ya ukavu na kufikia tani 903,222.

Ofisa Kilimo wa Mkoa, Lameck Tungu alisema hayo wakati akiwasilisha mada ya hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2009/2010 katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika jijini hapa.

Alisema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, hali ya chakula katika halmashauri zote tisa za mkoa huu ilikuwa nzuri kutokana na kutokuwepo kwa maeneo yaliyopata upungufu wa chakula tofauti na mwaka juzi.

“Mwaka jana katika msimu wa kilimo wa masika, tulilenga kulima na kutunza mazao ya chakula katika hekari 556,326 ambazo zilikadiriwa zitoe mavuno ya chakula ya tani 1,316,812.

Hadi kufikia mwisho wa msimu huo, mkoa ulikuwa umelima na kutunza hekari 429,095 ambazo zimetoa tani 951,928 sawa na asilimia 72 ya uzalishaji uliolengwa,” alisema.

Kwa mujibu wa Tungu, mkoa huo unakadiriwa kuwa na wakazi 1,858,492 na hivyo mahitaji ya chakula kwa kiwango cha juu cha kujitosheleza katika msimu wa mwaka huu ma wavuno yanakadiriwa kufikia tani 529,104.

“Tunaamini chakula cha ziada kitasaidia kutosheleza mahitaji ya wakazi iwapo tu watakitumia kwa uangalifu mkubwa, tunawashauri waepuke uuzaji holela, wakihifadhi vizuri na wasijaribu kukitumia kwa shughuli za kutengeneza pombe za asili,” alifafanua Tungu.

Alisema pamoja na uzalishaji huo, tathmini ya hali ya chakula inaonesha kuwa wakazi wa vijijini takriban 69,585 wamezalisha chakula cha kutosheleza mahitaji yao ambayo ni tani 19,710 huku wakazi wengine wapatao 221,480 wa mijini ambao jumla ya mahitaji yao ni tani 63,072 wakikabiliwa na upungufu wa chakula.

Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, aliwataka wajumbe hao kuhakikisha chakula kinahifadhiwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuongeza uhakika wa chakula.


Na Anna Makange, Tanga


Wednesday, February 16, 2011

HERI YA SIKU YA MAULIDI!!

Anko Mo Blogspot inawatakia waislamu wote heri ya siku ya Maulidi. Amen

Monday, February 14, 2011

WAJA LEO WARUDI LEO!!

Salam.......waja leo waondoka leo! Kitu cha RAHA LEO!!!

HAPPY VALENTINE'S DAY WADAU WOTE!

Anko Mo Blogspot inakutakia siku njema ya wapendanao. Happy valentine's Day!


Friday, February 11, 2011

DULLY SYKES BAND INAKUJA!!


Dully Sykes Band a.k.a "The Brothermen" kila siku ya Alhamisi watakuwepo pale Galapo Masai Club Ilala kwa kiingilio cha 5000/= kuanzia saa tatu usiku. Pia siku ya jumapili watakuwa pale Leaders Club sambamba kabisa na Twanga Pepeta. Punde tu wataanza kuja mikoni na wamejipanga kuanzia mkoa wa Tanga, hivyo wakazi wa Tanga kaeni mkao wa kula. Ni hayo tu!

HAPPY BIRTHDAY DJ ROGGER KISS!

Anaitwa Mohammed Hatib maarufu kama Dj Rogger Kiss wa redio Breeze Fm pamoja na Club Lacasa Chica zote za jijini Tanga. Amezaliwa siku kama ya leo. Hongera sana kaka na Mungu azidi kukupa uhai na mafanikio katika kazi zako.

Wednesday, February 9, 2011

IFAHAMU TANGA YACHT CLUB!

Tanga Yacht Club was founded on 1st May 1944 when a number of local businessmen and government officials formed a limited company. The certificate of incorporation was issued by the registrar of companies in Dar es Salaam on 7th June 1944. Founder members of the club in that time were G. Tirant, A.R. Pain, R.C. Jerrard, W. Bain, A.A. Phibbs, P. Roach and D. McQueen, all of them, as usual in that time, of male origin. The first two stated objectives of the company were:

To promote boating, yachting and sailing at Tanga and the vicinity of Tanga. For this purpose to acquire or take over the effect and liabilities of the present unincorporated club known as Tanga Yacht Club. This unincorporated club consisted of a small number of local people one of whom was G.W. Hatchell, a magistrate, who became the clubs first commodore in 1941.

But the club was really started before 1941 by Emil Hartmann, a local building contractor, who arrived in Tanga about 1936. As far as it is known Emil Hartmann owned the first boat to be moored at the club. It was named “Lorraine” after his original home.

Hartmann and Hatchell were friends and often went fishing together. He also wrote an article on fishing around Tanga and the adjacent coast, which was published in “Tanganyika Notes and Records” in 1954.

Other members at that time were Eldred Hitchkock and Abdulla Karimjee, both of them were later knighted for their services to the country and the sisal industry. Alee le Maitre, also a member at that time, and G.W. Hatchell were awarded the OBE for similar services.

The club premises at that time consisted of a clearing carved from the cliff to the left of the present steps as one enters the club. A small club house was built on what is now the paved area.

When the new club was formed in 1944 many new members were attracted and more boats, both power and sail began to appear. As the time went on and the club prospered and could afford it, the present structures were built up. The paved area was done by courtesy of Amboni Estates. A water color painting showing the club in 1949 was done by Mrs. A.

Budge and is still hanging in the bar. The polished paneling behind the bar was a gift of a member who spent more time at the bar than he did at his job. He said he was tired of staring at a whitewashed wall. The oil painting of a sailing race behind the bar was done by Mrs. Joan Wadhan, wife of a member.

Organized sailing was started about 1944, when members donated various trophies to be competed for. Reciprocal sailing matches between Tanga, Mombasa and Dar es Salaam became annual events. None appear to have occurred since 1979.

A number of Osprey class dinghies were made available for members to purchase during the 1950’s and good use was made of them. The dinghies changed hands many times as members left the club. Not many of them are serviceable today. Since 1983 there do not appear to have been any organized sailing apart from windsurfers and catamarans.

Fishing became very popular during the 1970’s and Ian Moncrieff, a former port pilot, arranged for the club to be accepted as a member of the International Game Fishing Association and the Game Fish Union of Africa. Subsequently, some club member's catches appeared in the annual records of the IGFA and until today the club still holds two records, one for a garfish of 4.1kg, caught in November 1969 by Alois Zorten on a 37 kg line and the other for a Giant Trevally, locally known as Karautesi of 54.8kg, caught in October 1970 by Mrs. Polly Mosgard on a 24kg line. Fish were much more plentiful in those days and huge catches were made almost every weekend.

A local merchant bought the catches from members at 50 cents per pound. On one occasion he had to take three trips with his truck to remove the catch. Most of the profit was spent by members over the bar that same evening. The biggest fish, ever brought in by a club member was a Black Marlin of 113.25kg caught by Attilie Torriani in December 1974 on a 37 kg line. Not so many fish are brought in these days, but that is no reflection on the skill and patience of those few fishermen who still keep trying as recent photographs still show.


Monday, February 7, 2011

MWANA FA- NI KWELI ALIANZIA TANGA!

MwanafalsafaMwanafalsafa / Mwana FA ('First Philosopher')

Mwanafalsafa started performing on stage in 1993 at school in Tanga region. Early influences -- even at primary school age -- were his brothers, Chine Black and Kasir, known as Quite Gangasters Chronic. Mwanafalsafa formed the crew Black Skin with his schoolmates Robilus and Getheerics in 1995. In 1996, he came third in the Tanga region hip hop competition.

Mwanafalsafa returned to Dar es Salaam in 1998 and studied A-levels at Ununio Islamic High School, where he majored in Physics, Chemistry and Mathematics. After completing A-level studies he started to work seriously at his music career in 2000. In 2003, he was voted best hip hop artist with his track 'Alikufa Kwa Ngoma' -- an anti-AIDS song -- at the Kili Music Awards, Dar es Salaam.

Album releases: Mwanafalsafa and Toleo Lijalo -- include songs discussing AIDS, spiritualism, love songs and dance-beat songs.

He has worked with various producers, including Bonie Love (Mawingu Studio), Pfunk (Bongo Records), Master Jay (MJ Records).

HAPPY BIRTHDAY SOPHIA BYANAKU NA DJ BOB NASS!!

Aanaitwa Nasr Thabit maarufu kama Dj Bob Nass wa Breeze Fm Radio ya hapa jijini Tanga. Amezaliwa siku kama ya leo. Hongera kaka kwa kuzaliwa upya na Mungu akuongoze vyema katika harakati zako za kupambana na maisha.

Anaitwa Sophia Byanaku, dada yetu mpendwa nae amezaliwa siku kama ya leo pia. Hongera dada kwa kuzaliwa upya siku kama ya leo. Mungu akuzidishie uhai zaidi. Amen

Friday, February 4, 2011

PWEZA NIGHT CLUB! NDIO SEHEMU YA KWENDA UKIWA JIJINI TANGA

Je wewe ni mkazi wa Tanga, au ni megeni umefika Tanga na hufahamu sehemu ya kwenda kujirusha siku ya leo na wikiend nyengine zote..!!?? Usidanganyike, sehemu ya kwenda ni moja tu. Ni pweza Night Cub iliyopo pale Chuda relini zamani La Club Tanzanite. Ni Club mpya ya kisasa jijini Tanga. Muziki mzuri kutoka kwa Ma'dj wa kali huku ukipata vinywaji kwa bei ya kawaida kabisa. Njoo tufurahi kwa pamoja ndani ya Pweza!!

Pwezaaa!!

SPECIAL THANKS FROM UMABE ARTS COMPANY!


On behalf of my General Manager Azma Mponda and Product Manager Victor Mrisho (Producer Kita) We are taking this Great Opportunity to thank you for your Great support and Effort to make our company moving on, May God Bless you Today and always, we are together in all ways, stay in touch and all the Best.
Regards,
Fredy Njeje
Project and Design manager
Umabe Arts Company
www.umabearts.blogspot.com

'UNANIDATISHA' WA ASHRAFF MAUNDI

Wednesday, February 2, 2011

UNAMFAHAMU HUYU....!!??

Ni maarufu sana hapa Tanga....!

Tuesday, February 1, 2011

BWANA MISOSI ATOA SHUKRANI!

Align CenterMsanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea Tanga Bwana Misosi ametoa shukrani zake kwa wale wote waliokuwa nae bega kwa bega katika msiba wa baba yake mzazi......."Mambo vipi ndugu wapendwa, napenda kutoa shukrani zangu kwa wote waliojitokeza kwenda kumpumzisha baba yangu kwenye shamba la mungu (Nyumba ya Milele) na wote tulioshirikiana kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki kigumu na shukrani zangu za dhati ziende kwa PROF JAY, FID Q, CHIEF RUMANYIKA (SOGGY DOGGY), ABDALAH MWAIPAYA na DR CHENI na hata waloshindwa fika ila kwa upendo walitoa pole zao.
Tunatoa shukrani na ahsante kama wanafamilia na Mungu awabariki sana.