BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, June 29, 2011

NINAOMBA KURA ZENU ZA DHATI


Habari wadau wa vijimanbo vya tanga, natumai wote ni wazima wa afya tele, kama hivyo ndivo basi sote tumshukuru Mungu muweza wa yote. Nakuja mbele yenu siku ya leo kwa kusudi moja tu ambalo kwa hakika tutashirikiana kwa pamoja na naamini tutafanikiwa. Ni muda mrefu tangu tuwe pamoja tukipashana habari za Tanga na hata zile zinazojiri kutokea nyje yaTanga, ndugu zangu watanzania wenzangu na wale wote wanaotokea Tanga.

Kuna hii kitu inaitwa TANZANIAN BLOG AWARDS 2011, natumai mmeisikia. Lengo la kuandika waraka huu kwenu ni kuwaomba kura zenu ili Blog yenu ya vijimambo vya tanga iweze kuibuka kidedea katika mchakato huo ambapo imechaguliwa kwenye category kadhaa ambazo ni Best Informative - Entertainments, Best Entertainments, Best News, pamoja na Best Music.

Mambo yote haya ukiyatazama kwa kina yapo kwenye Blog hii na nimatumaini yangu mnayafurahia sana. Jinsi ya kupiga kura BONYEZA HAPA kisha tazama upande wa kulia utaona vipenge kadhaa pamoja na nilivyokutajia kisha piga kura yako palipoandikwa http://ankomo.blogspot.com ukishabonyeza kwenye kile kiduara unabonyeza palipoandikwa VOTE, na hapo utakuwa umeipigia kura Blog yako.

NASHUKURU SANA NA NIMATUMANI YANGU NITAPATA KURA ZENU. NAOMBENI SANA!!


No comments:

Post a Comment