BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, June 21, 2011

KITABU CHA 'YALIYONIKUTA TANGA' KINAKUJA KAA TAYARI!!……Kwa mujibu wa yule dereva teksi, tulikuwa tayari tumekwishafika katika eneo alilolitaja kuwa ni Four Ways, moja kati ya eneo maarufu linalokutanisha barabara nne mahali pamoja. Nilitulia tuli mule garini.

Pamoja na kwamba kulikuwa ni usiku lakini niliweza kuona baadhi ya majengo yaliyokuwa pembezoni mwa barabara kutokana na taa za gari zilizokuwa zikimulika wakati tunaikaribia kona ya kuingia upande wa kushoto, kitendo ambacho kingefanya tuiache ile barabara tuliyokuwa tunakuja nayo.

Jengo moja lenye ghorofa tatu lililojengwa vyema likiwa na ukurutu wa rangi ya manjano, lilikuwa upande wa barabara ya pili kulia kwetu. Kulikuwa kimya, taa zikiwa zimewashwa kila upande wa jengo, huku wadudu aina ya kumbikumbi wakiwa wanaruka ruka juu ya zile taa. Hapakuwa na mtu pale nje.
Mbele tena kwa upande wa ile barabara, kulikuwa na jengo jengine lenye ghorofa nne likiwa limepakwa rangi nyeupe. Chini ya jengo hili palikuwepo na fremu tano za maduka, sikufahamu yalikuwa maduka ya nini lakini palionekana penye biashara nzuri, yote yalikuwa yamefungwa wakati ule.

Watu watatu waliokuwepo nje ya lile jengo, niliwahurumia sana kutokana na ubaridi mkali ulioambatana na upepo uliokuwa unavuma. Wawili kati yao walikuwa wamejibanza kwenye moja ya viambaza vilivyoko pale. Walijifunika makoti huku wamelalia maboksi.

Mwengine ambaye niliweza kumuona vizuri alikuwa amekaa kwenye kiti, amevalia gwanda za rangi ya buluu huku ameshikilia rungu kwa mkono wake wa kulia. Ni mwanamke!!! Tena bila shaka alikuwa ni mlinzi.................................


KAA TAYARI, KINAKUJA HIVI KARIBUNI!!

No comments:

Post a Comment