BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, June 21, 2010

'MECHI ZA UGENINI' NGOMA MPYA YA ROMA FT JOSE MTAMBO!!

Mkali wa Hip Hop kutokea Tanga Town, Rymes Of Magic Attraction a.k.a ROMA, ameachia ngoma nyengine mpya inayokwenda kwa jina la 'Mechi Za Ugenini' aliyomshirikisha Jose Mtambo, ikiwa imeitengeneza pale Tongwe Record.

Roma ambaye pia amewahi kutajwa kwenye tuzo za Teen Extra Award za Clouds Fm, mpaka sasa anatamba na ngoma zake nyengine kama na 'Mr President' pamoja na 'Pastor' ambazo hadi sasa bado zinafanya vizuri kunako vituo vya redio.

Isikilize ngoma hiyo mpya ya 'MECHI ZA UGENINI' hapo kulia juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!


ANNA KIWAMBO NDIO MISS TANGA 2010!!!!

Mnyange wa Miss Tanga 2010 Anna Kiwambo akiwa katika uso wa furaha punde tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika mchakato huo uliofanyika katika hoteli ya Tanga Beach Resort iliyopo Sahare, Miss Tanga 2010 imeandaliwa na 5 Brothers Entertainment.

Anna Kiwambo akiwa na washindi wengine, mshindi wa pili alikuwa ni Jari Mure, wa tatu ni Zuleha Mrisho. Nafasi ya nne alichukua Asia Gumbo na nafasi ya tano alinyakua Grace Joseph.

Matonya aki'show love kwa Miss Tanga 2010.

Hii ndio Tano Bora ya Miss Tanga 2010. Majaji walifanya kazi nzito hadi kufikia hapa.

Hii ilikuwa kumi bora.

Warembo wa Miss Tanga wakiwa wamejipanga na vazi la jioni.

Walimbwende katika show.

Miss Tanga 2010- its a wonderful event!!

Katika hali iliyofanya mashabiki wengi wainuke kwenye viti vyao na kushangilia, ni pale Aziza Khalifa ambaye pia ni Miss Pangani 2010 alipotangazwa kuwa mnyange wa Miss Talent Tanga 2010. Miss Pangani 2010 iliandaliwa na blog hii.

Aziza akiwa kwenye uso wa furaha baada ya kuvishwa taji la Miss Talent.

Matonya alikuwepo, japokuwa alipiga show dakika za mwisho.

Ney wa mitego karibu tena Tanga. Ulifanya kazi nzuri kaka.

Mrembo aliyekuwa anamaliza muda wake Glory Chuwa ambaye ni Miss Tanga 2009 akiwa katika tabasamu nono.

Glory akitoa neno la mwisho kwa watu wliohudhuria Miss Tanga 2010.

Kulikuwa na burudani nyingi....huyu jamaa anafanya yoga hapa! Alishangaza watu kwa staili zake za kujikunja.

Hapa sikujua alikaaje jamani..alikuwa anatembea kama yule mdudu tandu!!

Tanga Beach Resort ipo full..maswala ya misosi kwa waliokaa VIP ilikuwa safii!

Majaji wakiwa makini na kazi yao.

Lilian Mdachi akiwa amemkumbatia mshiriki wa Miss Tanga 2010, pamoja na mkali wa kiduku- akida a.k.a kijogoo.

Nilipenda washereheshaji walivyovaa, ulikuwa ubunifu wa hali ya juu. Walivaa kipwani hasa.

Watu wakipata burudani.

Huku ni karibu na back stage...tulikuwa wengi eneo hili.

Wadau wa mashindano ya urembo jijini Tanga, Benedict Kaguo ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la majira, na pia mtangazaji wa redio Mwambao Fm ya jijini Tanga. Halikadhalika Oscar Assenga, mtangazaji wa Mwambao Fm na pia ni mwandishi wa gazeti la Bingwa.

Nyuma ya stage...Amina aliyenyoosha mkono. Ndie alikuwa ni mwalimu wa Miss Tanga. Walimu wengine ni Mariam Bandawe na Oliver, hawapo pichani.

Swahiba wangu wa ukweli..Dj Bob Nass wa Breeze Fm Radio ya jijini Tanga akiwa na mshkaji wake.

Daaah! Huyu jamaa anaonekana ni mnoko ile mbayaa- tazama alivyoishika hiyo Camera..! Ila kazi nzuri, anatokea Sofia Production.

Friday, June 18, 2010

TANGA UNIQUE HERITAGE!!!

The colonial administration buildings, the attractive public buildings and commercial cum residential buildings which are all a century old or more make Tanga built up heritage unique. These buildings are still in use.

There are many buildings like, Katani House, Old Tanga School, Bombo Hospital cliff Block, mkonge Hotel, Eckenforde Teachers college, Eckenforde Secondary school, Palm court. The British era public buildings are newer in design mostly built after WORLD WAR II, where as German era buildings are large and grandiose, making their presence felt where ever they stand. Most of these building have been put in productive use to date.

Usambara court house

Urithi Museum

Tanga Library

Book Shop Office

MISS TANGA 2009 GLORY CHUWA KUKABIDHI TAJI KESHO!

Miss Tanga 2009 Glory Chuwa akiwa katika pozz pamoja na Rechal Mlaki namba mbili na Yasmini Zachari namba tatu. Glory anamaliza muda wake siku ya jumamosi ya tarehe 19/06/2010 ambayo ni kesho pale Tanga Beach Resort ambapo Miss Tanga 2010 anatarajiwa kupatikana.

Anko Mo Blogspot ilimtafuta Glory na kumuuliza jinsi anavyojisikia kuachia taji alilodumu nalo kwa mwaka mmoja. "Happy Because somebody else has to wear it and experience while working on it, sad because i just have to give it out" alisema glory ambaye kwa sasa yupo pale chuo mlimani jijini Dar es salaam akisomea Public Relations and Advertising.

"Unawaambiaje warembo watarajiwa wa Miss Tanga" lilikuwa swali jengine kwa Glory, "In my time we used to say BEAUTY WITH PURPOSE, the beauty thing goes with awareness (kujitambua who are you, what do U wish and what does the society want from U) Wajue sababu ya wao kushindana, and what the future holds, thats it!" alisema Glory ambaye wakati naongea nae alikuwa yupo safarini kuja Tanga kukabidhi taji.

Thursday, June 17, 2010

PANGANI YA LEO...!

Mandhari ya bahari ya hindi wilayani Pangani...! Wageni wengi hufurahi mazingira haya. Karibuni wote!

Wednesday, June 16, 2010

'NAHISI NAOTA MPAKA SASA'- AT

Ikiwa ni siku chache tu zimesonga tangu msanii huyu ajinyakulie tuzo ya wimbo bora wa kolabo aliofanya na Stara Thomas wa 'Nipigie',msanii Ali Ramandani Ali 'AT'...anasema kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata kwa kipindi kifupi...hakika bado anajiona kama yupo ndotoni.

AT...anasema hajawahi kufikiria hata siku moja kama anaweza kuwachanganya wapenzi wa muziki kwa singo moja tu ya 'Nipigie' ambayo inaendelea kutamba katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini.

"Mafanikio ya singo hiyo yamenifanya niwe na kiburi, najiona ninaweza muziki pia ndoto zangu za kuwa mmoja wa watawala katika fani hii zipo mbioni kutimia."

"Napata shoo za kufa mtu mpaka nyingine nazikataa, yaani naringa najaa kiburi, kutokana na wimbo huo," anasema AT.

Mwanamuziki huyu mwenye asili ya Pemba lakini amejikita zaidi kwa wajanja 'Dar es Salaam', anasema hatua aliyofikia ni kubwa na kwamba anawatetemesha wakali wengine.

"Wakati nilipoanza muziki wengi hawakuamini kama ningefanya vema, sasa wengi wanakubali sikuwa nikifanya utani."

AT,ambaye anadai ametoka katika familia ya kimasikini anasema matunda ya wimbo huo yamemfanya atunze wazazi wake waliopo Zanzibar na vilevile anaishi vema pamoja na mchumba wake (hakutaka kumtaja jina).



"Nimetoka kwenye familia ya kimasikini, hilo silikatai, nalikubali tena kwa moyo mmoja, napopata mafanikio anajiona mwenye amani zaidi."

..."Ingawa siwasaidii wazazi wangu katika kila kitu lakini nawapa kile kidogo ninachokipata kutokana na muziki hasa wimbo wa 'Nipigie'," anasema AT.

Anasema ingawa yeye ni mtu wa watu lakini wimbo huo umemfanya atembee mabega juu zaidi.

"Kuna maringo ya kujisikia na ya kujiamini, mimi nina maringo ya kujiamini ndiyo maana ni mtu wa watu napenda kukaa uswahilini kujichanganya na watu kwa sababu hao ndiyo wanaonifanya niwe juu,"anasema AT.

AT ambaye ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya tisa wa familia yao anasema hakuna kitu kizuri kama kujichanganya na wadau mitaani kwani hao ndiyo wanaofanya wasanii wawe juu siku zote kwa kununua CD zao na kuingia kwa wingi kwenye shoo zao.

Mwanamuziki huyo aliyezaliwa miaka 26 iliyopita katika Hospitali ya Mwembeladu, Zanzibar anasema mwanamuziki hatakiwi kudharau watu mitaani kwa sababu ya kuwa nyota.

AT pia anaamini amepata Tuzo ya Muziki ya Kili kutokana na ushirikiano alioupata kutoka kwa watu wa mitaani.

Akieleziea wimbo huo anasema: "Wazo wa la kuimba 'Nipigie' lilinijia kama masihara na sikujua kama wimbo ungepanda chati kiasi cha kunipatia tuzo."

AT, anatarajia kuzindua albamu yake iliyobeba jina la 'Nipigie' yenye nyimbo 14 hivi karibuni. Albamu hiyo ina vionjo vya sauti za wanamuziki kama Nyota Ndogo, Nameless, Ngoni, Shircom, Stara Thomas,Tina, Hadija Kopa na Joti pia inamiondoko mbalimbali, kama ya Zuku, miondoko ya Afrika Magharibi na mchanganyiko wa lugha ya Kiswahili na Kiarabu.

"Wimbo huo umenifanya nikutane na watu wazito ambao sikutegemea kukutana nao katika maisha yangu ya muziki, namshukuru Stara Thomas kwa kushirikiana nami," anasema AT.

Na mwanamuziki huyo anasema anatarajia kuachia singo nyingine kali ambayo anaamini itakuwa na mafanikio makubwa.

Mbali na nipigie AT ameimba nyimbo kama Wanimaliza,Mapenzi,Raha Zako, Kwanini,Yamini,Vijana,Utaona Noma,Ziro na nyinginezo.

Baadhi ya nyimbo zake zimefanywa kwa maproducer wakali kibao kama kwa Benjamin wa Mambo jambo, Marco Chali na wengine kibao.

TUJIKUMBUSHE NA 'KACHIRI' YA THE KILIMANJARO!

Tuesday, June 15, 2010

'NAUMWA' NGOMA MPYA YA DNJ FAMILY

Msanii anayefanya vizuri katika anga ya muziki wa Bongo Flava kutokea Tanga ambaye kwa sasa maskani yake ni kule London nchini Uingereza Tizzle, akiwa na washkaji zake Damuz, Josh, D wanaotengeneza kundi la DnJ Familiy, wameachia ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la 'Naumwa'.

Akiongea na Blog hii Tizzle amesema kuwa, wameamua kuunganisha nguvu kwa pamoja na washkaji zake ili kila mmoja aweze kuonyesha kipaji chake na kufanya muziki wa bongo flava uzidi kujulikana kimataifa.

Tayari msanii huyo anatamba na ngoma yake ya 'Nameless' aliyomshirikisha Damuz, ambayo aliitengeneza pale Mzuka Entertanment Rec iliyopo East London chini ya producer Josh.

Pamoja na kuwa wanne katika kundi hilo lakini 'Naumwa' imefanywa na Tizzle, Damuz na Josh studio ikiwa hiyo hiyo Mzuka Rec. Kila la kheri kundi la DNJ Familiy.

Kabla ya kwenda nchini Uingereza Tizzle alikuwa anaishi pale Majani Mapana na baadae kuhamia Bara Bara ya 15.



Monday, June 14, 2010

'MBWELA'- CHIFU WA KWANZA WA WAZIGUA KUTIA SAINI MKATABA NA DK. KARL PETERS!

Dk. Karl Peters (kati) akiwa na wenzake Dk. Karl Juhlke na Joachim Graf. Huyu Dk. Karl Peters ndiye aliyewaingiza mkenge babu zetu wakati wa kuingia ukoloni wa Ujerumani nchini kwa kuingia katika mikataba ya kilaghai na watawala wetu wa jadi.

(Mbwela, Chifu wa Wazigua mkoani Tanga, ndiye aliyekuwa mtawala wa jadi wa kwanza kutia saini mkataba na Dk. Karl Peters mwaka 1884.)

Haya na mengi mengineyo yanayohusu historia ya nchi hii yanapatikana katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar ambako kwa sasa ukarabati wake unakaribia tamati ili kuifanya sehemu hiyo isiwe tu ya makumbusho bali sehemu ya kukutania wadau wakubwa kwa watoto, wake kwa waume kwa shughuli mbalimbali ikiwemo utamaduni, sanaa na mengineyo.

Makumbusho hiyo ya Dar (katikati ya jiji karibu na IFM na sio Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama kama ambavyo wengi wamezoea kuchanganya) hivi sasa inajulikana kama Makumbusho na Jumba la Utamaduni - Museum and House of Culture.

Asante MICHUZI

MITAA YA TANGA CITY LEO MCHANA!!!

Maeneo ya katikati ya jiji la Tanga.

Hii ni barabara ya kuelekea Ridoch..

Maeneo ya karibu na benki ya CRDB

Bustani nzuri barabara za jiji la Tanga.

Hapa ni karibu ya ofisi za TTCL na Dar Worth.

Kuelekea Four Ways

Ofisi za Posta

MAZOEZI YA MISS TANGA 2010 NI MOTO WA KUOTEA MBALI!!

Warembo wa Miss Tanga 2010 wakiwa kwenye mazoezi makali ya show pamoja na mwalimu wao Akida a.k.a Kijogoo kwenye ukumbi wa Splendid hapa jijini Tanga. Shindano la kumsaka mnyange wa Miss Tanga linatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 19 mwezi huu kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort ikiwa imeandaliwa na 5 Brothers Entertainment.

Warembo wakiwa makini mazoezini.

Hao warembo wawili hapo mbele ni Miss Pangani 2010 Aziza Khalifa na mshindi wa pili wa kitongoji hicho Aisha Athumani wakiwa mazoezini. Miss Pangani 2010 iliandaliwa na Anko Mo Blogspot.